Riwaya: Oooh Roletha!

Mchumba

JF-Expert Member
Jul 27, 2012
277
261
SEHEMU YA KWANZA

Roletha, mtoto mdogo sana wa miaka 7 anayeishi na baba yake tu ambaye ni mgonjwa mahututi wa kansa ya utumbo mwembamba, anapitia machungu mazito ya maisha katika umri wake huu, machungu ambayo hata mtu mzima hawezi kuyahimili.

Pamoja na kuwa mama yake mzazi yupo hai na ni mzima wa afya, Roletha anageuka kuwa ndiye mama na mlezi wa baba yake ambaye kutwa anashinda kitandani kuuguza ugonjwa wake.
Kutokana na ugumu wa maisha na mabalaa mengine, anajikuta anakosa fursa ya kwenda shule , pamoja na kukosa fursa hiyo lakini anakuwa na uwezo wa kusoma, kuandika pamoja na uelewa mzuri wa hesabu.

Fuatilia Riwaya hii ya kusisimua ya maisha ya mtoto huyu.
==============================================
12994300_1151040954914776_8150657095426270668_n.jpg

“sasa baba kwanini usiende Hospital ?” lilikuwa ni swali la Roletha kwa baba yake ambaye alikuwa hoi kitandani kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya utumbo mwembamba.

“mwanangu Hospitali nimekwenda mara nyingi sana, sitakiwi mimi inatakiwa fedha !” baba yake na Roletha alitoa jibu hilo kwa mwanaye huku akihangaika kujigeuza pale alipokuwa amelala.

“duh hivi madaktari ni wachache hospitalini baba ! hatuwezi kumpata ambaye siku hiyo atakuwa hana kazi tumuombe akutibu ?” Roletha aliendelea kumuhoji baba yake huku akijisikia huruma sana kwa jinsi alivyokuwa amedhoofu.

“walaaa wakati wewe unawaza kumpata daktari mmoja, kuna wagonjwa wengine kama mimi wamezungukwa na madaktari zaidi ya saba mwanangu !” Roletha kila mara alipokuwa akisikia majibu hayo kutoka kwa baba yake alizidi kujisikia uchungu sana moyoni mwake.
“sasa baba mwisho utakuwa ni upi, kama hali yenyewe ndio hii ?” Roletha alihoji huku akijikaza asitoe machozi mbele ya baba yake.

“hahaha mwanangu ! ndio unataka hadi kulia, ntapona tuu ! mbona we ukiumwa kichwa au tumbo huwa unapona mwenyewe, kwanini nisiwe mimi mwanangu ?” baba yake alijaribu kumfariji mwanae kwa kumuongopea kwamba ugonjwa wake ni wakawaida tu kama yalivyo magonjwa mengine, wakati siku zote alikuwa akijua yupo kitandani akisubiri muujiza wa Mungu au kifo chake tu.

“haya baba mimi nakupenda sana, basi tulale !” baada ya jibu hilo Roletha alimuomba baba yake walale kwa kuwa giza, usiku ulikuwa ushatamalaki, na bila kinyongo baba yake alikubaliana na mwanaye.

Roletha na baba yake walikuwa wakilala katika chumba kimoja, hii ilitokana na umasikini mkubwa waliokuwa nao, kwani hata nyumba waliyokuwa wakiishi ilikuwa na vyumba viwili tuu, yaani sebule ambayo ilikuwa haina kitu na zaidi ikifanyika kama jiko na chumba hicho walichokuwa wakilala, nyumba yenyewe hiyo ilikuwa ni hisani tu ambayo baba yake na Roletha alipewa na boss wake kajieneo wakati hali yake ya ugonjwa ikianza kumvaa.
Sababu ya kupewa ilikuwa ni kwamba mwenye eneo hilo aliamua kuuza eneo lake hivyo alijikuta akishikwa na imani na kuamua sehemu ndogo ya eneo hilo kumuachia ndugu huyo na hayo ni baada ya kufanya kazi ya ulinzi kwake kwa muda mrefu.

Kila mara ulipofika usiku wa manane baba yake na Roletha alikuwa akishtuka usingizini na kulia sana huku akimtizama mwanaye, swali kubwa lililokuwa likimtesa kichwani mwake ni, ni nini hatima ya mwanaye baada ya kifo chake ?
Aliamini kwa ugonjwa aliokuwa nao ni lazima tuu atakufa, ikiwa wenye fedha wanashindwa kumudu vipi yeye masikini tena na hospitali washamwambia amechelewa !

Wakati huo akikumbwa na hali hiyo pia mwanaye alipokuwa akishituka naye alijikuta akiikumbwa na hali hiyo hiyo huku akijutia, umasikini na hali ya baba yake, na kila mtu alikuwa akijitahidi kujificha ili tuu kutokumfadhaisha mwenzie.
Roletha pamoja na utoto wake alikuwa ashazoea kukaa njaa na siku akishiba basi chakula ni uji kama si uji basi watashindia chai na siku kitu hali ikiwa njema basi chakula kizuri ni ugali na dagaa wa uswahilini ambao washakaangwa ili kusevu matumizi mengine ya kupika.

Shughuli kuu aliyokuwa akiifanya Roletha ni kuomba omba ndipo aendeshe maisha yake na ya baba yake, pamoja na yote hayo Roletha na baba yake walikuwa wametengwa na majirani kama ujuavyo masikini hana rafiki.
Na sababu ya kutengwa ilikuwa ni familia ambayo haishiriki shughuli za kijamii, kama misiba, harusi nk.

Japokuwa sababu ilikuwa ni ufukara uliokubuhu lakini watu hawakuwaelewa na kuwashutumu kwamba ni watu ambao hawatoi hata michango ya misiba wakati wao wanaishi, lakini si hivyo tuu majibu ya Roletha pia watu wengi walikuwa hawapendezwi nayo, hakuwa na jeuri bali alikuwa ni mtoto ambaye ana uwezo wa kujenga hoja kiasi kwamba hata mtu mzima ukajikuta unabaki mdomo wazi.
Laiti angekuwa ni mtoto wa tajiri basi angeonekana kama ana akili sana ila kwa kuwa ni mtoto wa fukara alionekana ni mtoto jeuri na mwenye kiburi.

Tatizo kubwa la Roletha lilikua anazijua haki zake lakini ukweli ni kwamba Roletha alikuwa na heshima pia alikuwa ni mtoto ambaye hawezi kutukana hata kwa kusema mjinga.

Baba yake ilikuwa ni kila siku ambayo anaachiwa uhai alikuwa akiitumia kumfundisha mwanaye kujiamini, kuelewa, kujihami, kujali na kuilewa dunia na mambo yake yote, masomo hayo japo yalikuwa ni zaidi ya umri wa Roletha lakini yalikuwa ni zaidi ya masomo ya elimu ya kawaida.
Roletha pia alikuwa na kichwa kizuri kunasa mambo, alikuwa na uwezo akasikia kitu na akakirudia kukisema kama kilivyo bila ya kuacha hata neno moja.

Huyo ndio Roletha mtoto mzuri kuanzia sura, fikra na muonekano tatizo lake ni moja tuu anaishi katika maisha ambayo ni magumu pasina mfano.
Watoto wa mtaani kwao walizoea kumuita "ombaomba ombaomba hilo!", lakini kila walipomuita hivyo wala hakujisikia vibaya zaidi ya kucheka tu huku akiwajibu majibu ambayo wenzie hao walikuwa wanashindwa kuelewa kutokana akili zao kuwa changa,

“hamjawahi kuomba, sijawahi kwenda shule nani ana faida ikiwa hamjui hata kuumba silabi” mara zote Roletha alikuwa ajibu hivyo bila kujali makelele ya kuzomewa na watoto wa mtaani, pamoja na hayo hakupenda jambo hilo amueleze baba yake kwa kuwa alijua akimwambia litamfanya azidi kujisikia hovyo zaidi kwa yale ambayo mwanaye anakumbana nayo atokapo nyumbani.

Hatimaye kama utaratibu wa siku ulivyo giza lilikuwa linatokomea na mapambazuko ndio yakawa yanaanza, Roletha akiwa bado katika usingizi mzito, baba yake alikuwa akifungua macho huku akimshukuru Mungu kwa kumuamsha salama kwani kila mara alipokuwa akilala hofu yake ilikuwa ni kama ataiona kweli siku inayofuata.

“Roletha…… Roletha…. Roletha amka mwanangu ?” baba alikuwa akimuamsha mwanaye kwakuwa kulikuwa kumekucha.
“mmmmh !” Roletha alikuwa akiamka huku akijinyosha kutokana na uchovu wa usiku kucha.

Baada ya kuamka kama ilivyokuwa kawaida yake baada ya kuosha uso wake, alichukua kiporo chake cha uji na kunywa kisha safari ya kuelekea katikati ya mji ikawa inaanzia hapo kwani huko ndiko alikokuwa akikutumia kama ofisi yake kwa ajili ya kuomba.

“badae baba ! uji wako nimekuachia mi naenda !” Roletha kila asubuhi alikuwa akitumia lugha hiyo kwa baba yake utafikili anakwenda kazini vile, huku baba yake kila akisikia kauli hiyo moyo wake ukimuuma sana na akijisikia hata shida kujibu kauli ile ya mwanaye.

“Mungu akulinde mwanangu, usichelewe kurudi ikifika saa tisa na nusu anza kurudi, pia kuwa makini na pikipiki sawa” Roletha alikuwa ni msikivu sana pia alikuwa na uwezo hata wa kumsoma mtu kwa muonekano wake na kuweza kutambua nini kinachomsibu.

“niko makini baba ! usiumie sana haya yataisha siku moja” ndio lilikuwa jibu la mtoto huyo kisha akafungua mlango na safari ikaanzia hapo.

Hiyo ndio ilikuwa ratiba ya kila siku ya mtoto huyo, akiwa na safari hiyo alikuwa akikutana na makundi ya watoto wenzie wengi wakielekea shule, na hapo ndipo alipokuwa akikutana na kadhia ya kukashifiwa pia kutukanwa.

“ahaa ombaomba !” ilikuwa ni sauti ya mtoto mmoja katika ya kundi akiwa anaelekea shule.
“unapenda ehee twende tukaombe wote basi” Roletha alijibu huku akitabasamu na kumtizama mtoto mwenzie huyo.

“we kijinga nini ! nani akaombe, ntakuzaba !” mtoto huyo alikuwa akiongea huku akimsogelea Roletha.
“basi nisamehe kaka !” Roletha alijaribu kujitetea kwa kuwa alijua mwenzie tayari amekasirika.
“nani kaka ako nani !” Roletha kabla hajajibu lolote mkono wa mtoto yule ulikuwa ushatua shavuni kwake, kiasi kwamba alijikuta akiona nyota maana mtoto yule alikuwa amemzidi sana kimuonekano alikuwa ni kama mtoto wa darasa la nne hivi.

“ubabe na shule wala haviendani, nenda kawaulize waliomaliza wababe wao wa enzi hizo walipo !” Roletha alitoa kauli hiyo kisha akaendelea na safari yake huku machozi yakiwa yamemlenga na hasira ikiwa imemkaba na kujaza kifua, hata hivyo mtoto yule hakutosheka alichokifanya ni kumuongeza kumpiga mtama mmoja na Roletha alipoinuka alimsindikiza na kibao, mtoto wa watu wala hakujibu kitu zaidi ya kuendelea na safari yake tuu huku moyoni akitamka maneno ambayo yalikuwa ni kama laana kwa mtoto yule aliyekuwa akimpiga.

“Eeehe Mungu kama kweli upo na umtizame huyu hapa hapa duniani kabla ya siku ya mwisho” Roletha alikuwa akiwaza hayo huku akijifuta chozi ambalo alishindwa kustahimili kulivumilia.

Njia nzima mtoto Roletha hakuwa mwenye furaha zaidi ya kutembea akiwa na masononeko pamoja huzuni, na alikuwa akitembea umbali mrefu sana kwani nyumba yao ilikuwa nje ya mji na sehemu aliyokuwa akitakiwa kufika kila siku ni katikati ya mji ambapo ilikuwa ni zaidi ya kilometa 8.

Tofauti na watu wengine walivyokuwa wakifikiri kwamba mtoto huyo alikuwa akikaa chini na kuomba au kuvizia magari na kuomba, haikuwa hivyo Roletha alikuwa akikusanya watu na kuanza kufanya mambo ambayo watu walikuwa wakistaajabu na wakati wakimshangaa alikuwa anaweka kopo lake na kutaka asaidiwe.
Kwa mfano watu walikuwa wakistaajabu kuona mtoto mdogo akijieleza kuwa ana uwezo wa kusoma, na kweli wakiandika kitu alikuwa anasoma tena bila ya kutetereka, si hivyo tuu Roletha alikuwa akiwashangaza watu pia alipokuwa akijipambanua kwamba ana uwezo hata wa kuimba tebo, na watu walikuwa wakifikili labda kama kanatania hivi ! walipojaribu kuchagua tebo ambazo ni ngumu kwa rika lake kama tebo ya tisa mtoto alikuwa anaimba tu huku watu wakipiga makofi utafikili wanasikiliza hutuba ya mwanasiasa.

Lakini siku ambazo mambo kama hayo hayakujipa ilikuwa inambidi aingie naye tu mtaani kuomba kama watoto wengine, na huko ndiko alikokuwa akizidi kuumia sana na kuhisi watoto wenzie wote nao wana shida zinazowakabili kama yeye.

Ilipokuwa imefika mida ya saa tisa Roletha kama kawaida yake ilikuwa ni muda wa kurudi nyumbani, na wakati huo alianzisha safari yake kama kawaida japokuwa alikuwa na fedha hakufikilia kupanda gari kwa kuwa alijua hata fedha aliyonayo haimtoshi kabisa.

Alipokuwa amekaribia mitaa ya nyumbani kwao alipitia dukani na kununu unga, na baada ya hapo alipita sehemu akanunua mkaa kisha safari ya kuelekea nyumbani kwao ikawa imepamba moto huku akifurahi kweli kwamba anakwenda kukutana tena na baba yake !

Ghafla furaha yake ilingia dosari baada ya kukutana tena na mtoto yule yule ambaye asubuhi ya siku hiyo alimpa kipigo, hakuogopa alichokifanya ni kuongoza mbele tuu huku mtoto yule akimzuia kwa mbele kama anataka kumfanyia ukorofi vile, na kweli ndio ilikuwa nia yake alipofika jilani tuu alianza kumzingira kama mtu anayemzuia kupita hivi ?

Roletha wala hakusema kitu zaidi zaidi ya kuhama pande na mtoto yule akizidi kumzingira tu, baada ya kuhangaishana kwa muda mrefu mtoto wa watu masikini alijitahidi kutumia nguvu ili kupenya lakini hakuweza kufanikiwa kwa kuwa mkubwa wake alikuwa na nguvu zaidi, katika purukushani za hapa na pale mwishoe unga aliokuwa ameshika mtoto yule ulimwagika wote baada ya mfuko aliobebea kupasuka.

Roletha alijikuta akishikwa na hasira na alimtizama mtoto yule takribani kwa dakika mbili na baada ya hapo alimng’ata mtoto Yule kwa nguvu sana huku akikaza sawasawa meno yake bila kujali kipigo alichokuwa anapokea huku mgongoni, na vile tumeno twake tulivyokuwa tumechongoka mtoto aliyekuwa ameumwa alipiga kelele sana ! kiasi kwamba mpaka mama yake anafika pale tayari damu zilikuwa zikimvuja mwanaye.

Mama yule kuona tuu mwanaye yuko vile wala hakutaka kuuliza alichokifanya ni kumkamata mtoto wa watu na kuanza kumtandika makofi, huku akimuagiza mwanaye akalete kiboko, Roletha kuwa ombaomba ilikuwa akihesabika kama mtoto mtukutu sana, mpaka kiboko kinafika pale Roletha alikuwa kimyaa wala hakuwa na la kusema lolote na mama yule alianza kumshushia viboko mfululizo utafikiri anapiga paka mwizi vile.

Roletha alikuwa na uchungu sana alimatamani alie kwa sauti ili naye baba yake asikie aje kumnasua pale ! lakini baba yake ndio huyo hata akiamka anaweza tumia nusu saa kufika pale, mama yule alipohakikisha fimbo ile imepasuka pasuka kidogo ndio moyo wake ukaridhika na kumuachia Roletha, hata hivyo mtoto wa watu hakuhangaika kukimbia zaidi zaidi alipoachwa ndio kwanza alianza kujiokotea mkaa wake ili tuu ukawasitili na baba yake, huku kila bonge aliloinua juu akililipa kwa chozi lake lililokuwa likidondoka chini na baada ya hapo safari ya kuelekea nyumbani ikaanza huku Roletha akiongea peke yake kwa jinsi alivyokuwa amechanganyikiwa na kipigo kile.

“Hivi kweli ameshindwa hata kuona unga uliotapakaa mahali pale ! basi sawa nimekosea mimi ! lakini ananipigaje vile kweli ameshindwa hata kunitizama kwa umri !” Roletha alikuwa akiongea peke yake huku akivuja machozi tuu katika mashavu yake na akielekea nyumbani kwao.

Itaendelea.....
 
SEHEMU YA PILI.

Roletha alikuwa akitembea huku njia nzima akifadhaika kwa maumivu makali aliyoyapata kutokana na kipigo pamoja na hasara aliyoingia ya kuharibiwa bidhaa zake alizoninunua tena kwa fedha aliyipata kwa tabu sana.

Alipofika nje ya nyumba yao alijitahidi kujipukuta na kujifuta alama zote za machozi pamoja na kujikaza na maumivu aliyokuwa nayo kwa wakati huo,lengo likiwa ni moja tuu kumficha baba yake kuwa amekutana na balaa katika mizunguko yake kwakuwa alijua kuwa kitendo cha baba yake kuyajua hayo pengine kingemuongezea maumivu zaidi na kujuta mwanaye kujihusisha na utafutaji wa pesa hali ya kuwa yeye ni mgonjwa na hana namna hivyo aliamua kuvumilia tuu, huku akiingia ndani kwa kucheka cheka.
“umeshindaje baba yangu ?” Roletha alimuuliza baba yake huku akijibaraguza.

“safi tuu mwanangu ! nashukuru umerudi salama !” babaye alimjibu, huku Roletha akiwa na muonekano tofauti na siku zote wa kutokaa jirani na baba yake, kitu kilichofanya baba yake kumuongeza swali jingine !

“kulikoni leo mwanangu mbona leo kama haupo sawa ?” Roletha baada ya kusikia tuu swali hilo alipatwa na mashaka kidogo kuhisi pengine baba yake ameanza kumshitukia.

“hamna baba nilikuwa navuka barabara nikamwaga unga, nataka nikanunue tena tupike kwa ajili ya usiku ?” baada ya baba yake kusikia hivyo wala hakupata mashaka tena na kumuacha mwanaye aendelee na mambo yake.

Moja kati ya vitu ambavyo alikuwa akivifanya siku zote mtoto Roletha ni kila alipokuwa akitoka katika shughuli zake ilikuwa ni lazima baadhi ya fedha afiche na hata bila ya kumwambia baba yake ! na sababu kuu ya kufanya hivyo alikuwa akiamini tuu ipo siku atatimiza fedha hizo na kumpeleka baba yake hospitali, hivyo fedha hizo alikuwa hazigusi hata kidogo labda tuu itokee baba yake kazidiwa basi ndio atatoa na kwenda kununua dawa ambazo zilikuwa ni kwa ajili ya kupunguza maumivu tuu.

Kitendo alichofanyiwa siku hiyo aliona ni bora akatoe fedha yake hiyo kidogo kwa ajili ya kuongezea kiasi alichokuwa nacho ili akanunue tena mahitaji kwa ajili ya chakula.

Baada ya kufanya hivyo na kukamilisha mapishi walikuwa wamekaa huku akila na baba yake chakula cha usiku na jikoni ukichemka uji kwa ajili ya asubuhi atapotoka pia baba yake kikiwa ndio chakula chake cha asubuhi na mchana wakati ambao mwanaye huwa kuhangaikia chakula cha siku inayofuata.

Na hata baada ya kula kilichokuwa kikifuata kwa Roletha ni kufanya usafi, japo kuwa siku zote alikuwa akifika mchovu lakini ilikuwa ni lazima akimaliza kupika na kula, shughuli inayofuata ni usafi, hivyo alikuwa akitumia muda huo kuosha vyombo, kusafisha mazingira na kufua nguo zake na za baba yake na baada ya hapo ndio huelekea kulala.

“najivunia sana wewe mwanangu !” ilikuwa ni sauti ya baba yake Roletha baada ya mwanaye kumaliza kazi na kurudi ndani kwa ajili ya kulala.

“kwanini baba !” huku akijiweka tayali kwa ajili ya kulala.
“sina jibu zuri la kukwambia zaidi ya kukusifia u mvumilivu Rol wangu ?” Baba yake alikuwa akimpa wasifu baada ya kuona jinsi mwanaye alivyo na moyo wa kutochoka.

“ehee asante basi ………… niambie kesho nikifika mjini ni tumie kanuni gani ?” pamoja na uchovu huo lakini bado Roletha alikuwa akipiga hesabu za hiyo kesho yake jinsi ya kutafuta.
“mmmmh kesho, kesho sasa kanuni yetu ni siasa sawa !, ukifika inatakiwa uzungumzie changamoto za nchi hii ?” Roletha alikuwa akimsikiliza kwa umakini sana baba yake kwa jinsi alivyokuwa akimfundisha kuhusu changamoto za nchi yake, na baada ya hapo alimtajia majina ya viongozi wakuu wote huku akimwambia pia na majina ya wabunge, sambamba na wakuu wa wilaya huku akimtajia na mkuu wake wa mkoa.

Roletha aliweza kumeza mambo yote hayo na baada ya hapo baba yake alimtupia maswali mawili matatu, akajiridhisha kwamba mwanaye ameelewa somo, hivyo akajikuta akimruhusu alale ili tuu kujiandaa na hiyo kesho.

Kutokana na hali ya kutumia muda mwingi kukaa huku kila mara usingizi ukimpitia pitia, mara nyingi baba yake Roletha alikuwa akihakikisha mwanaye analala huku yeye akiwa bado macho, na ndio wakati huo aliokuwa akipata maumivu makali kila alipokuwa akiutizama uzuri wa mwanaye , halafu bado ni mtoto na ndiye anayemuhudumia, alijikuta akijisikia uchungu sana na macho yake yakimiminisha machozi, lakini hilo lilikuwa dogo, kubwa ni vile alikuwa akijua maisha yake yapo ukingoni halafu ana mtoto mdogo sana kama yule !

Mawazo yaliyokuwa yakimtesa ni je ni nani atamuachia mwanaye ? maisha ya mwanaye yatakuwaje baada ya hapo ? ikiwa mtaani tuu pale yeye yupo lakini wametengwa kwa sababu zisizo na msingi, hivi siku akifariki itakuwaje kwa mwanaye ?

Maswali haya mara zote alikuwa akilala bila ya kuyapatia majibu ! karibia siku zote usiku alikuwa akilia sana na sababu zikiwa hizo ? kwani kadri siku zilivyokuwa zinakwenda ndivyo ambavyo hali yake pia ilikuwa inazidi kuwa mbaya ?

Akiwa bado katika hali hiyo ghafla mwanaye alishitushwaa usingizini na sauti za baba yake kama analia vile, na kwakuwa baba yake pia hakuwa akipenda kuona mwanaye akiijua huzuni hiyo, alipogundua mwanaye kama anajipepesa pepesa hivi aliamua kujifanya amelala usingizi mzito.

“Baba………… unalia nini ?” Roletha alihoji huku akijiinua sehemu ile aliyolala, hata hivyo hakujibiwa kwa kuwa baba yake alikuwa akimuigizia yupo usingizini kabisa.

“we baba wewe ! babaaaaa, we baba ?” Roletha aliendelea kumuita baba yake huku akimtingisha kwa kuwa alikuwa na uhakika kwamba baba yake wala hajalala.

“mmmmh ! kuna nini mwanangu ?” baada ya mtoto kukazana ilibidi baba ajifanye akiitika kama ametoka usingizini vile.
“mbona unalia baba ! kuna nini ! si tulisema hakuna kulia lia hapa ndani lakini baba !” Roletha alikuwa akimkumbusha moja ya makubaliano yao ya enzi hizo wakati yeye akiwa mdogo na akilia kwa sababu ya njaa.

“mmmmh mbona sijalia mimi mwanangu ?” Baba yake alikuwa akijaribu kumuaminisha mwanaye kitu ambacho hajakifanya.

“nimekusiki jamani baba ?” Roletha alikuwa akiongea kwa unyonge huku akionesha huzuni sana.
“kama umenisikia basi nilikuwa ninaota ?” Baba yake aliongea kwa kujiamini kiasi kwamba mwanaye naye akaamini kuwa huenda ukweli ukawa hivyo.

Baada ya makubaliano hayo ukimya ukapita kidogo lakini hakuna kati yao ambaye alipitiwa na usingizi, hivyo wakajikuta wakitumbukia katika mazungumzo tena !

“hivi mwanangu ! siku ukirudi hapa nyumbani na ukakuta mimi sipo utaenda wapi ?” lilikuwa ni swali zito sana kwa Roletha huku baba yake akiuliza na kujua ni kwanini kamuuliza vile mwanaye.

“sijui ntafanyaje mimi ! lakini kama wewe ungekuwa mimi ungefanyaje baba ?” japo kuwa baba yake aliamini kuwa mwanaye bado upeo wake ni mdogo sana katika kung’amua mambo, lakini Roletha alikuwa amepata picha baba yake anamaanisha nini ! ila kwa wakati huo alijifanya hajaelewa kitu.

“ningekuwa wewe ! naenda kwenye yale majumba mazuriiiii au kwa watu matajiri, kisha nawambia naomba mnisaidie kazi mimi masikini, baba yangu kanikimbia ! nimebaki peke yangu ?” baada tuu ya kusema maneno hayo Roletha alijua nini baba yake alikuwa anakimaanisha hivyo badala ya kujibu mjadala ule alizalisha swali jipya ?

“baba unahisi utakufa baba yangu ? najua huwezi kunikimbia kwa jinsi unavyo nipenda ?” Roletha aliongea huku akianza kutokwa na machozi kwa kile alichokisikia kutoka katika mdomo wa baba yake, na baba yake alijikuta akipatwa na uchungu ule ule ambao ulikuwa ukimtesa mwanaye, hivyo walijikuta wakikumbatiana na mwanaye huku wote nyuso zao zikiwa na huzuni sambamba na machozi.

“hapana mwanangu nahisi unabeba mzigo ambao umekuzidi umri ! napenda kujua sana usalama wako mwanangu, basi tuu hujui mwanangu ?” baba yake aliongea huku akizidi kuumia na machozi yakizidi kumtoka kwa yale aliyokuwa akiyaona mbele yake kwa mwanaye na hali yake ilipokuwa imefikia.

“kwani baba ! mimi mama yangu yuko wapi ?” Roletha alimpelekea tena swali baba yake ambalo lilizidi kumfanya ajisikie vibaya kwani historia yake na mkewe haikuwa nzuri kwa mwanaye, hivyo kila siku alijikuta akiwa mzito kumwambia mwanaye, lakini siku hiyo ndiyo kwanza mtoto aliuliza yeye mwenyewe.

“mwanangu mama yako sifahamu hata alipo, sielewi chochote kutoka kwake, ila ninachojua tu ni masikini kama sisi na inawezekana anateseka zaidi yetu maana aliondoka akiwa hana hata pa kukaa” pamoja kwamba hakupenda kumweleza maneno yale mwanaye lakini alijikuta akitoa maelezo tu kwakuwa mwanaye alihoji.

“kwanini hufahamu aliko na kwanini aliondoka baba ?” Roletha alizidi kuhoji huku moyoni mwake akiamini kuwa familia yake ni kama ina mkosi vile.

“leo ntakueleza kwanini mama yako aliondoka, lakini sitakueleza kwanini sifahamu aliko !, mama yako tulikuwa tukipishana mambo mengi sana mwanangu, sina hakika sana kama sababu ilikuwa ni huu umasikini ? wakati ndoa inataka mtoke na uamuzi wa aina moja, bahati mbaya sisi tulikuwa tunapishana sana maamuzi, hapo ndio ulikuwa mwanzo wa migogoro ya familia yetu mpaka leo, sababu kila mtu alitaka kufuata lake !” Roletha na udogo wake wote ule alishindwa kuelewa nini maana ya ndoa mpaka wanakwenda tofauti ambayo inafanya wasijali hata uwepo wa yeye ambaye ni mtoto mdogo kabisa na hata maamuzi hakuwahi kuyatoa ! alijikuta akimezea maswali mengi sana aliyokuwa nayo muda huo.

“kwani baba ! mama ni mtu mbaya kwetu ?” Roletha aliishia kuhoji hilo tuu.

“hapana mwanangu mama yako si mtu mbaya hata kidogo !” Baba yake alimjibu kwa ufupi sana kwakuwa alijua ukimya wa mwanaye kwa akili alizonazo atakuwa ametengeneza maswali mengi sana.

“sasa kwanini hujui aliko ?” Roletha kwa mara nyingine tena alirudia swali lake lilelile la awali.

“hilo nimekwambia nitakueleza siku nyingine mwanangu, haya mambo ni mazito sana ! twende taratibu tuu utanielewa sawa !” baba yake pia alibaki na msimamo wake ule ule na kumfanya mwanaye atulie.

“sawa baba ! lakini niambie tena hivi sisi hatuna ndugu zetu ?” Roletha alikuwa na maswali ambayo yalikuwa na ujazo mzito sana tofauti na kimo na umri wake.

“Ndugu tunao tena wengi tuu mwanangu ?” baada ya kujibiwa swali lake akaunganisha na lingine ?
“sasa kwanini hawatusaidii baba ?”

Japokuwa ilikuwa ni usiku sana lakini baba yake alikuwa hana budi kujibu maswali yote ya mwanaye kwani alijua ni sehemu ya kumueleza ukweli juu ya maisha yake.

“mwanangu ndugu zangu si mfano wa kuigwa ! ni watu ambao maneno na vitendo vyao ni tofauti sijawahi kuwa na jema kwao, wakisikia una tatizo watasema mbona sijawaambia na hata ukiwaambia hakuna wanachokusaidia zaidi wataanzisha uongo kwamba u msumbufu, wakisikia wewe mgonjwa pia lawama ni kwako bado mgonjwa kuwa husemi, lakini cha kushangaza ni kwamba hata wao wakiumwa hawakwambii, walinilaumu siwatembelei wakati wao pia hawajawahi nitembelea, na hata nilipowatembelea kwa kuwafuata bado walilalamika kwamba siendi kuwachukua waje wapajue ninapoishi, wakati wao mimi hawakuja kunichukua nikapajue kwao zaidi ya jitihada zangu binafsi.

MWANANGU SIFA YA UNDUGU IMEBAKI TUU MKIKUTANA KUTAMBIANA HUYU NI MTOTO WA KAKA YANGU, HUYU NI MJOMBA WANGU, HUYU NI MTOTO WA SHANGAZI YANGU basi lakini sifa halisi ya upendo haipo tena mwanangu !” mpaka anamaliza kusema maneno hayo Roleth alikuwa akiumia sana na kuzidi kububujisha machozi maana alichokitafsiri pale ni kwamba mtu pekee wa kumsaidia baba yake ni yeye hakuna mwingine.

“sawa nimekulewa baba ? lakini si ungeniambia tu kwanini hujui mama aliko, siku nyingine tuseme mambo mengine ?” Roletha alitoa maelezo hayo huku akimuonea huruma sana baba yake.

“haina shida mwanangu, ni usiku sana naomba ulale kesho uwahi kuamka, halafu kesho ukirudi nitakueleza kwanini sifahamu mama yako alipo sawa !” Roletha aliambiwa maneno ya kubembeleza sana na baba yake na kujikuta akikubali jambo lile.
“sawa baba ! usiku mwema.

***********************************
Baada ya hapo haikuchukua muda mrefu wote walijikuta wakiingia katika usingizi mzito sana kwakuwa walichelewa kulala sana siku hiyo.

Pamoja kwamba walilala kwa kuchelewa sana lakini mapema sana kama ambavyo Roletha alikuwa ameuzoesha mwili wake, aliamka mapema na kuanza kujiandaa kwa ajili ya kuwahi katika shughuli zake za kupata kipato, ili kuendesha familia yao.

Baada ya kupata kifungua kinywa ambacho kiukweli hakikuwa kifungua kinywa kwani alikuwa akinywa uji baridi kila asubuhi, alimfata baba yake na kumuaga kwamba anatoka nyumbani, kama ilivyo ada baada ya kupata baraka ya baba yake mtoto Roletha alimuomba Mungu amsaidie sana ili apate pesa kwani kwa yale aliyoelezwa na baba yake kuhusu ndugu, yalimkaa sana kichwani ! na kila mara yalikuwa yakijirudia kichwani mwake kwamba ndugu ni msemo tuu ! hivyo jukumu la kumsaidia baba yake ni lake.

Baada ya sala yake Roletha alifungua mlango na safari ya kuelekea kati kati ya mji ndio ikawa imeanza kwa aina hiyo, huku akili yake ikiwaza njia za kupita zitazomfanya asiingie katika maumivu ya kipigo kama siku zingine .

Itaendelea......
 
Back
Top Bottom