Riwaya: Kijijini kwa Bibi

MTUNZI ; ALEX KILEO.

RIWAYA ; KIJIJINI KWA BIBI.

SEHEMU YA KWANZA.

___________
MWANZO
____________
"njoo uingie bado gari iko wazi hii,
mama kaa vizuri hapo mnatosha
watu wawili",ilikua sauti ya mpiga
debe aliyekuwa anaita abiria katika
stendi kuu ya daladala mkoani Dodoma(Jamatini).
Ni dhairi kabisa mpiga debe huyo alikuwa amechoka kutokana na njaa na jua kali, pia muonekano wake ulijidhirisha alivyochoshwa na maisha. Mdomoni alikuwa na sigara iliyokuwa inawaka na aliipeleka mdomoni kila alipogida kipakiti cha konyagi kilichokuwa na nembo ya kichwa cha jogoo, na kila alipogida konyagi hiyo aliimeza kwa tabu huku sura yake akiwa anaikunja kama anaumia koo. Alivaa shati na suruali ya rangi ya bluu iliyopauka na zaidi suruali yenyewe aliivalia chini ya makalio na kufanya kuonekana kwa nguo yake ya ndani iliyokuwa na rangi isiyoeleweka kutokana na kuvaliwa kwa muda mrefu au kukosa maji yenye sabuni ya unga kwa muda mrefu.
Na kichwani alikuwa na kofia ya kapelo yenye picha ya mmea kwa mbele na uso wake ulipambwa na macho makubwa malegevu yenye rangi nyekundu, alikuwa na pua pana ilienea vizuri juu ya mdomo wake uliokuwa mwekundu kama umeunguzwa na kemikali au moto, na masikioni alikuwa amevaa heleni ya duara kama mtoto wa kike na miguu ilikuwa na raba nyekundu ya kupanda iliyonakshiwa na mchoro wa nyota uliozungukwa na neno lililoandikwa "allstars".

Ndani ya daladala mojawapo pale
stendi anaonekana kijana mmoja
mtanashati, ingawa sio sana ila
mpangilio wake wa mavazi na usafi
ndo vimemfanya aonekane wa kipekee kuliko vijana wengine
ndani ya ile daladala.
Mpangilio wake mzuri wa mavazi ilitosha kumjua kabisa huyo kijana ni aina ya vijana wa kileo wanaokwenda na wakati. Alikaa kiti cha nyuma kabisa cha daladala huku masikioni akiwa amevaa headfones kubwa kama mpigaji mziki wa disco.

Baada ya muda wa dakika ishirini, ile daladala ilijaa kabisa na Dereva akaiwasha na safari ikaanza.

Ilitumia mwendo wa dakika 30, ile
gari ilisimama mbele ya majengo
marefu(ghorofa) yaliokuwa
yameandikwa UNIVERSITY OF
DODOMA.

kijana akatelemka na kumlipa konda nauli kisha akashika njia iliyokuwa ikielekea kwenye ghorofa lililokuwa na rangi nyeupe, alipolifikia alipanda ngazi mpaka ghorofa ya tatu na kuingia katika chumba ambacho inaonekana anaishi humo,

'niaje kayoza,? vipi umepata body
spray ya chastity,'" wenzake ndivyo
walivomlaki namna hiyo,hakujibu
kitu akawatupia begi,

"Alafu sio ustaharabu huo, muwe mnajifunza kusalimia ndipo muulize shida zenu" Kayoza aliongea huku akitoa shati
lake akabaki na vest iliyoruhusu kifua
chake kionekane kwa ufasaha zaidi, alafu akajitupa kitandani akachua
simu yake aina ya HTC desire,
akaenda upande wa ujumbe mfupi
wa maneno ambao kulikuwa na ujumbe mfupi uliongia muda mrefu uliopita ila hakuonekana kuujali, akaona huo ndio muda wa kuangalia huo ujumbe, alipousoma aliishia kutabasamu kwa dharau huku akisikitika, kisha akaandika
"usipoteze
muda wako kunifikiria, sina mpango
wa kuwa na mahusiano ya kimapenzi
muda huu" akautuma ule ujumbe katika jina alilosevu
KICHECHE.

"Vipi umekula" Rafiki yake mmoja alimuuliza huku alivaa fulana,

"Tayari, sasa nitaendaje mjini alafu nisile?" Kayoza alijibu huku akiutupia mto chini ya kitanda,

"Poa basi, mimi ndio naenda kutafuta msosi" Rafiki yake huyo aliongea huku akifungua mlango,

"Haina noma, Acha nijipumzishe kidogo" Kayoza alijibu.

Siku iliyofuata ilikua sikukuu ya
kitaifa, kwa hyo wanafunzi wengi
hawakuwa na ratiba ya kuingia
darasani.

Kayoza alichelelewa
kuamka hiyo siku, aliamka saa nne
asubuhi, akaingia bafuni, alipomaliza
kuoga akarudi katika chumba chao, ile kuingia ndani akakunja sura
ghafla baada ya kumkuta ndani msichana ambaye hakuwa akimpenda,

"mambo kayoza", ilikua sauti ya binti mrembo ambae
anawakimbiza wanawake wenzake
kwa uzuri wa umbo na sura, alikua
katika tatu bora katika shindano la urembo lililoshirikisha vyuo vyote vilivyopo Dodoma.

Huyu binti anaitwa Stellah
Malingumu, ni msichana wa miaka ishirini na moja ambaye alikuwa mwanafunzi chuoni hapo akichukua shahada ya ualimu katika masomo ya sayansi.

"poa, umeamkaje?",Kayoza akajibu
huku akijilazmisha kujua hali ya stellah ingawa hakutaka,

"aah safi, mbona meseji yako uliyonitumia jana sikuielewa?", Stellah nae akamtupia swali,

"kwani niliiandika kwa kutumia lugha
ya kichina?", Kayoza badala ya kujibu
nae akauliza, tena kwa jeuri,

" Ok, yaishe", stellah akaamua
kukatisha mabishano,

"Samahan naomba utoke nje mimi
nataka kuvaa", kayoza akaongea kwa
ustaharabu wa kinafki,

"mimi naondoka moja kwa moja, ila
naomba jioni tukutane mjini katika
maeneo ya nyerere square", Stellah
akamwambia Kayoza,

"kuna ishu gani?, alafu jioni, si bora
ingekua mchana ningekuja",Kayoza
akajibu. ,

"usiwe na wasiwasi mpenzi, kama
unahofu njoo hata na marafiki
zako",Stellah akamalizia huku akitoa tabasamu murua.

"Mimi sio mpenzi wako Stellah, rekebisha kauli zako" Kayoza alimuonya Stellah huku akiwa amekasirika,

"Sawa, nisamehe kwa hilo. Kwa hiyo jioni utakuja ama?" Stellah aliuliza tena,

" Jioni ya saa ngapi?", Kayozaakauliza,

" saa moja na nusu tutakua pale tunawangojea, nitakua na Tausi",

"Poa, haina noma, nitakuja", Kayoza
akakubali mwaliko. Kama angejua

"Peke yako au?" Stellah aliuliza,

"Vipi kwani, mbona maswali mengi?" Kayoza aliuliza huku akiwa amehamaki,

"Inatakiwa nijue ili nipange ratiba zangu za matumizi vizuri" Stellah alijibu kwa upole,

"We panga unavyojua wewe, maana mimi nije peke yangu au na wenzangu hayo hayakuhusu na gharama zangu au wenzangu pia hazitokuhusu" Kayoza aliongea macho yakiwa makavu,

"Basi baba, hatugombani hapa" Stellah aliongea huku akitabasamu,

"Haya nenda nje mimi nivae" Kayoza alimwambia stellah,

"Kwani ukivaa mbele yangu kuna ubaya gani?" Stellah aliuliza kwa utani,

"Wewe mpumbavu nini?" Kayoza aliongea huku akimsukumia Stellah nje na kubaki ndani peke yake akisonya kwa hasira huku akiufikiria mualiko aliopewa na Stellah..

Ila angejua ambacho kitamtokea, basi asingekubali ule mwaliko.......

******ITAENDELEA******

the Legend☆
 
RIWAYA : KIJIJINI KWA BIBI.

MTUNZI : ALEX KILEO.

SEHEMU YA PILI.

______________
ILIPOISHIA.
_______________
"Inatakiwa nijue ili nipange ratiba
zangu za matumizi vizuri" Stellah
alijibu kwa upole,

"We panga unavyojua wewe, maana
mimi nije peke yangu au na wenzangu hayo hayakuhusu na gharama zangu au wenzangu pia
hazitokuhusu" Kayoza aliongea
macho yakiwa makavu,

"Basi baba, hatugombani hapa"
Stellah aliongea huku akitabasamu,

"Haya nenda nje mimi nivae" Kayoza
alimwambia stellah,

"Kwani ukivaa mbele yangu kuna
ubaya gani?" Stellah aliuliza kwa
utani,

"Wewe mpumbavu nini?" Kayoza aliongea huku akimsukumia Stellah
nje na kubaki ndani peke yake huku akisonya kwa hasira huku akiufikiria mualiko aliopewa na Stellah..

Ila angejua ambacho kitamtokea,
basi asingekubali ule mwaliko.......

_____________
ENDELEA.
_____________

"Mpuuzi kweli huyu manzi" Kayoza aliendelea kuongea peke yake huku akivaa kaptula kabla hajashtuliwa na mtu aliyekuwa anasukuma mlango ili aingie ila alishindwa kutokana na ule mlango kufungwa kwa ndani,

"Bado hujaondoka tu?" Kayoza aliuliza kwa hasira,

"Fungua bwana" Sauti nene ya kiume iliongea kutoka nje na ndipo Kayoza akauendea mlango na kuufungua na wakaingia rafiki zake wawili, mmoja aliitwa Omary na mwingine alitambulika kwa jina la Denis,

"Vipi wewe unajifungia fungia mchana, au ulikuwa na Stellah?" Denis alimuuliza Kayoza,

"Umejuaje?, alikuwepo hapa muda si mrefu" Kayoza alijibu huku akijitupa kitandani,

"Kwa hiyo mlikuwa mnafanya mambo flani nini?" Omari aliuliza huku akicheka,

"Muda wote unawaza ujinga tu, hivi ni lini utakuwa wewe?" Kayoza alimuuliza Omary kwa hasira,

"Huyu sio bure, zile tetesi hata mimi naanza kuziamini" Omary aliongea huku akimgeukia Denis,

"Tetesi gani?" Kayoza aliuliza kwa hamaki huku nae akimgeukia Denis,

"Maneno tu ya watu" Denis alijibu huku akionekana hataki kulizungumzia hilo,

"Maneno gani sasa, si uniambie" Kayoza aliongea huku akiwa bado anamuangalia Denis,

"Mchane, usiogope, huyu ni rafiki yetu na ni lazima chochote kinachosemwa juu yake tumwambie" Omary alimsisitizia Denis,

"Niambie hata wewe kama Denis hataki kuniambia" Kayoza aliongea huku akimgeukia Omary,

"Bwana mimi sipendi kuficha, uko nje habari zimeenea kuwa wewe ni shoga, eti haiwezekani tokea uanze kusoma hapa mwaka wa tatu huu haujawahi kuonekana na mwanamke sehemu yoyote ile" Omary aliongea huku akitazama chini na kumfanya Kayoza nae ainame chini huku akiwa na huzuni sana,

"Mimi siamini kama wewe unaweza kuwa shoga, ila nahisi labda una tatizo jingine, tueleze rafiki yetu, usiogope" Denis aliongea kwa lengo la kumfariji Kayoza ambaye bado alikuwa kichwa chini huku akiwaza,

"Tunasaidiana mambo mengi. Sisi ni ndugu sasa na sio marafiki tena, tatizo lako ndio tatizo letu, kwa hiyo Sema kama una tatizo tuone kama tutaweza kukusaidia" Omary nae alimsihi Kayoza awaeleze,

"Sina hamu ya kuwa na mwanamke wala kufanya mapenzi na sijui ni kwa nini?" Kayoza aliongea kwa huzuni huku akiwa bado kichwa chini,

"Ila ulishawahi kufanya mapenzi kipindi cha nyuma?" Omary alimuuliza,

"Tokea napata akili sijawahi na wala sina hamu kabisa" Kayoza alijibu,

"Umeshawahi kwenda hospitali?" Denis alimuuliza,

"Nimeenda mara nyingi sana na naonekana sina tatizo" Kayoza alijibu,

"Na kwa waganga wa kienyeji umeshawahi kujaribu?" Omary aliuliza,

"Kila nikipanga Mipango ya kwenda kwa waganga, uwa siku ikifika najikuta napuuza au kinaweza kutokea kitu kingine kitachoharibu huo mpango" Kayoza aliwaeleza wenzake,

"Basi ilo jambo tutalifuatilia vizuri, sio bure" Denis aliongea huku akisikitika,

"Stellah alikuwa anasemaje?" Omary aliamua kubadilisha maada,

"Alafu nilishasahau, amesema jioni tuonane mjini" Kayoza alijibu,

"Kwa hiyo leo unatuacha, utalala huko huko au utarudi?" Omary aliuliza,

"Amesema tuende wote watatu" Kayoza alijibu,

"Aisee mimi leo sina hela, kwa hiyo sitoenda, si unajua leo wikiendi so ukienda mjini inabidi ujipange" Denis aliongea huku akitabasamu,

"Amesema gharama zote zake, sisi tuende kama tulivyo" Kayoza aliongea na kufanya wenzie wafurahi,

"Basi poa, ngoja nilale kidogo ili chakula kishuke" Denis aliongea huku akijilaza kitandani,

"Ila usiku tutarudi, hatutalala mjini" kayoza alisema,

"Mimi sitorudi, nitaunganisha clab moja kwa moja, leo wikiendi bwana. Au wewe Denis nawe utarudi?" Omary aliuliza huku nae akipanda katika kitanda chake cha juu,

"Tutajua uko uko" Denis alijibu kivivu huku akiwa amesinzia.

********************

Mida ya saa moja kasoro jioni, Kayoza,
Omary na Denis walikua maeneo ya
mjini katika foleni ya ATM. Ilipofka
zamu yao kayoza akaingia ndani,
akatoa pesa, kama elfu hamsini
akatoka na kuungana na wenzake,

"oya wakubwa, mi naona twendeni
kwanza tukale kwa sababu huyu
demu mimi simuamin amini,
anaweza kuwa katenga bajeti ya
kunywa tu, akijua sisi tumekula", Kayoza alikua anawaambia wenzake,

"acha uboya we mtoto wa mama, alipokwambia uje saa moja alitaka tuje tupige nae msosi wa jioni, huyo du si
anajua ratiba zetu za msosi wa
usiku, kuwa tunakula saa tatu, kwa hiyo alijua saa moja tutakuwa bado hatujala" Omary aliongea huku akiwa anatafuna karanga.

Mara simu ya kayoza ikaanza kuita mfukoni,
akaitoa mfukoni kisha akaiangalia
kwenye kioo cha simu, jina lililoonekana wakati huo lilisomeka KICHECHE.

'huyo Stellah anapiga" Kayoza aliwaambia
wenzake ambao walikuwa
wanamuangalia,

"usilembe bishoo wewe, pokea simu uongee na mtoto mzuri", Omary
alimsisitiza Kayoza baada ya kuona anajishauri kupokea simu.

Kayoza akaipokea ile simu, kisha
akaweka sura ya umakini,

"Mambo..",Kayoza alimsalimia Stellah,

"poa, mko wapi?",Stellah alimuuliza Kayoza kupitia simu,

"tupo hapa benk, tunakuja",Kayoza
alijibu,

"mbona simu ilikuwa inaita muda mrefu hivyo?",Stellah alianza
kulalamika namna hyo,
"nimeiweka sauti ndogo mno, alafu
hapa ATM kuna utulivu sana na watu wako wengi sana, kwa hiyo ilinibid nisogee mbali kidogo ili niipokee simu yako" Kayoza
akamdanganya Stellah,

"ok.. poa, sisi tumeshafika
tunawasubir nyinyi" Stellah
akamtaharifu Kayoza,

"sisi tutachelewa kidogo kwa sababu tunaenda kula kwanza", Kayoza
akatoa udhulu,

"mambo gani sasa, nyie njooni tu, hivyo vyote nimevitayarisha",Stellah akawaka,

"poa, ndani ya dakika kumi tutakuwepo hapo" Kayoza akaongea kisha akakata simu.

"Haya waungwana twendeni
tukawachune hao vicheche, mida ya
saa nne tuwateme tukajiachie clab
mpaka kuche" Kayoza akawaambia wenzake,

"Vicheche? Kwani yuko nani?" Omary aliuliza,

"Yuko na Tausi" kayoza alijibu,

"Basi twendeni tukakae nao alafu baadae tunaenda zetu clab" Omary aliongea,

'nyie nendeni tu uko club mimi lazma nikalale
na mmoja wao" Denis aliongea na wenzake wakacheka.

"Jamaa mroho kweli" Omary alimtania Denis huku akiendelea kucheka,

"Wamekwambia wapo wapi?" Denis alimuuliza kayoza,

"Wapo Nyerere squarre" kayoza alijibu huku wakivuka barabara inayoelekea wanapokwenda.

Walipofika nyerere square,
wakamuona kwa mbali stellah na rafiki yake aitwae Tausi,

"Leo kazi ipo" sauti nzito ilipita kwenye masikio ya Kayoza na kushindwa kuelewa inatokea wapi, na cha ajabu Denis na Omary hawakuweza kuisikia sauti hiyo....

******ITAENDELEA******

the Legend☆
 
RIWAYA : KIJIJINI KWA BIBI.

MTUNZI : ALEX KILEO.

SEHEMU YA TATU.

______________
ILIPOISHIA
______________
Walipofika nyerere square,
wakamuona kwa mbali stellah na
rafiki yake aitwae Tausi,

"Leo kazi ipo" sauti nzito ilipita
kwenye masikio ya Kayoza na
kushindwa kuelewa inatokea wapi,
na cha ajabu sio Denis wala Omary aliyeweza kuisikia sauti hiyo....

_________________
MUENDELEZO
_________________
"Jamani hamsikii sauti yoyote ya kutisha?" kayoza aliwauliza wenzake baada ya kuwaona kama hawasikii anachokisikia yeye,

"Sauti gani?" Denis aliuliza,

"Sauti nzito inakwaruza masikioni" Kayoza alijibu na wenzake wakaishia kucheka,

"Acha mawenge wewe, au unapata uoga kukutana na Stellah?" Omary aliongea huku akimcheka kayoza,

"Acha ujinga, mimi sijamuongelea Stellah hapa, naongelea ishu nyingine" Kayoza aliongea baada ya kutofurahishwa na maneno ya Omary,

"Yaishe basi, kifupi sisi tunasikia sauti za magari tú na hatusikii sauti nyingine. Au sio Ommy?" Denis aliuliza huku akimgeukia Omary,

"Ndio maana ake" Omary alijibu huku akicheka.

Wakiwa wanaendelea na mwendo, kwa mbali waliweza kuwaona Stellah na Tausi , ila walikua nje ya sehemu husika.

"Sasa mbona wapo nje?" Omary aliuliza kwa mshangao,

"Labda wamekaa nje ili tuwaone kiurahisi" Denis alijibu.

wakina kayoza walipowafikia
wakapeana salamu,

"jaman twendeni sehemu
nyingine, hapa hata hapaeleweki" Stellah aliongea baada ya salamu,

"kwani hapa kuna nini?, kayoza akauliza?" Kayoza aliuliza kiubabe ubabe,

" Jamani shem hapa
wamesema mda umeisha" Tausi
ndivyo alijibu namna hyo,

"We mpuuzi nini, nani Shemeji yako?" kayoza aliuliza kwa hasira,

"Nini wewe, Acha fujo Kayoza, huwezi jua labda Shemeji yako kwangu" Omary aliongea huku akimcheka Kayoza,

"Huyu mwenzenu vipi, mbona ana hasira za karibu hivyo?" Stellah aliuliza huku akimtazama Dennis,

"Mzoeeni tu huyu mshkaji wetu" Denis alijibu huku akitabasamu,

" sasa tunaelekea wapi?" Kayoza akauliza,

"Mhm...mi hata cjui ni sehemu gani nzuri kwa hapa mjini usiku huu" Stellah akajibu,

"Mi naona twendeni hapo
Saturnight bar" Denis akatoa mwelekeo,

"Bar tena?" Kayoza aliuliza kwa mshangao kwa maana yeye hatumiagi kilevi,

"Bar hata soda zipo" Omary alijibu huku akionekana kumpuuza Kayoza,

" hiyo Saturnight ni mbali kwani ili tuchukue taxi?" Stellah aliuliza,

"Ahaa wapi ni hapo tu nyuma ya TRA" Denis akajibu na mwisho wote
wakakubaliana waende hapo Suturnight Bar.

Walipofika wakakuta
watu wengi sana na hii ni kutokana na mpira wa ligi kuu ya uingereza
ilikua inaonyeshwa pale nyakati za usiku,

"Kwa hiyo tufanyaje? Maana naona kote kumejaa na hakuna nafasi" Tausi aliuliza,

"Ebu subirini kidogo" Denis aliongea
kisha akaingia ndani akatumia mda
kama wa dakika kumi hivi hivi, kisha akatoka,

"jamani eee, nimeongea na wahusika
wakasema kama tunahitaji sehemu
tulivu, tunaweza kuchukua chumba
kimoja tukawa tunakitumia ila lazima
tukilipie, wenzangu mnasemaje?" Denis aliongea baada ya kutoka ndani,

"haina shida tena ndo vizuri" Stellah
akajibu,

"Mhm, kwani jaman
tutatumia mda gani kula na hayo maongezi kiasi kwamba mpaka tuchukue chumba?" Kayoza akauliza,

"Boy acha maswali ingia utengeneze shavu, leo tuifanye siku kuu" Omary akasema.

Baada ya mvutano
wa hapa na pale, wakakubaliana
kuingia mule ndani, wakaagza
chakula cha kutosha na vinywaji pia,
so ikawa kula na kunywa, paka
wakawa wako hoi kwa ulevi. Ila wakati wote huo Kayoza alikuwa anakunywa soda. Ila mwisho wenzake walimrubuni na kujikuta akionja bia moja, katika hali ya ajabu kabisa, alijikuta anazima kwa bia moja tu mpaka wenzake wakamshangaa.

Baada ya wote vilevi kuwakolea, vibweka vikaanza mara Stellah amkumbatie
kayoza, mara omari amtukane denis
kisa tausi.

Ilipofika saa 7 usiku, mhudumu
akawaambia anataka kufunga kwa
hiyo waondoke, ila wao wakadai
watalala pale pale na waongezewe
chumba kingine, Mhudumu akawapa
ufunguo wa chumba kingine ambacho kwa makubaliano yao hicho chumba wangeenda kulala Denis, Omary na Tausi.

Stellah akawaomba wote watoke abaki yeye
na kayoza, kipindi hicho kayoza hajielewi amepoteza kujitambua kutokana na bia moja aliyokunywa, tena ukizangatia ndio ilikua mara yake ya
kwanza kunywa pombe.

Walipotoka tu wakina Denis, stellah akafunga
mlango haraka, akajitahidi kumbeba
kayoza paka kitandani, alafu Stellah
chap chap akavua nguo kisha akawa
anamvua kayoza, huku akiamini hiyo siku ni moja kati ya siku bora kabisa ya kutimiza moja ya ndoto zake, kulala na mwanaume anayempenda.

Alitumia dakika
tano kukamilisha zoezi zima, kisha akapanda kikatandani na kuanza kumchezea Kayoza kimahaba, ila kuna hali aliiona, kila baada ya dakika moja mwili wa Kayoza uliongezeka ubaridi kiasi kwamba akawa kama chupa ya soda iliyotoka ndani ya friji.

Stellah aliliiona hilo ila alitaka kupuuzia kutokana na hamu zake za kimwili. wakati akiwa bado anaangaika, ghafla bin vuu kayoza aliamka mithili ya mshale huku macho yake yakiwa meupe na kiasi kwamba mboni hazikuonekana, macho yakawa
yanang'aa tena kama tochi, Stellah ndipo akapata mshtuko,

"Vipi tena Kayoza?" Stellah aliuliza huku hofu ikianza kumtawala, lakini kayoza hakujibu kitu na badala alitoa tabasamu moja la ajabu na kufanya meno yake yaonekane na kwa kasi ya ajabu yale meno yakaanza kurefuka na kuwa makubwa kama ya mnyama anayefahamika kwa jina la ngiri.

Stellah akiwa kama amepatwa na
mshango au bumbuwazi, alijikuta ameganda Pale pale kwa kihoro huku akiwa hana nguvu kutokana na tukio analoliona.

Mwishowe akajikaza na kuanza kujiondoa ndani ya shuka kwa lengo la kukimbia,

"Unaenda wapi usiku huu, huogopi kutoka nje na giza hili?" Kayoza alimuuliza huku akiwa katika hali yake ile ile,

"Naenda chooni mara moja" Stellah alijikuta anajibu bila kutegemea huku mwili ukiwa unamtetemeka,

"Nisubiri nikusindikize" Kayoza akaongea huku nae akiwa anashuka kitandani, Stellah akahisi ni bora kukimbia kuliko kumuamini huyo kiumbe wa ajabu. Akiwa anaanza kukimbia, Kayoza aliruka na kutua mbele yake, Stellah akataka kupiga kelele, ila alichelewa, tayari mkono wa Kayoza ulikuwa mdomoni kwa Stellah kumziba asipige kelele na huku mdomo wa kayoza ukiwa shingoni mwa Stellah na yale meno makubwa yalitumika kuung'ata mshipa mkubwa wa damu na Kayoza akaanza kuinyonya hiyo damu huku akitoa muungurumo wa ajabu uliosikika kwa sauti ya chini. Alipomaliza kazi ya kufyonza damu ya mwili wa Stellah, aliuachia ule mwili na kudondoka chini ukiwa hauna tena uhai, ndio ukawa mwisho wa Stellah, mwanaume aliyedhani wa ndoto za maisha yake ndiye mwanaume aliyempotezea ndoto za Maisha yake.

Kayoza aliuangalia ule mwili kwa dakika chache na yeye nguvu zikamuishia akapoteza fahamu na kuanguka chini pembeni ya mwili wa Stellah.

Asubuhi Kulipokucha, Kayoza aliamka huku akiwa na uchovu usio wa kawaida, ila alijishangaa akijikuta amelala chini huku akiwa mtupu hana nguo na pia alihisi mdomoni ana harufu ya damu ila alipuuza huku akiamini labda alijing'ata usiku, kitandani hakukuwa na mtu. Akapeleka mikono chini ili ainuke, hapo ndipo alipohisi amegusa mwili wa mtu, akapeleka macho yake Pale alipohisi amegusa mtu, ndipo alipoweza kumuona Stellah akiwa amelala tena akiwa mtupu na shingoni alikuwa na damu, hapo akashtuka, akajivika ujasiri na kumgeuza, akakuta alama ya meno kwenye shingo ya Stellah, Kayoza akajikuta anatema mate kutokana na zile alama za meno zilizotengeneza kidonda kikubwa shingoni kwa Stellah. Kayoza alipotema mate alishangaa kuona mate yake yametapakaa damu, akaona sasa hiyo kesi ni yake.

"mama yangu, kumeshaharibika hapa" kayoza aliongea baada ya kuhisi kuwa inawezekana Stellah amekufa na hakuna mwingine atayekamatwa zaidi yake.

Akaona njia sahihi ni kukimbia hakutaka kujua hata wenzake wapo wapi.

Akaamua kuvaa fasta ili
akimbie mule ndani kabla mtu yoyote hajajua tukio alilolifanya, mara akasikia
sauti ya mtu akigonga mlango,

*****ITAENDELEA******

the Legend☆
 
RIWAYA KIJIJINI KWA BIBI.

MTUNZI ALEX KILEO.

SEHEMU YA NNE.

________________
ILIPOISHIA..
________________

"mama yangu, kumeshaharibika
hapa" kayoza aliongea baada ya
kuhisi kuwa inawezekana Stellah
amekufa na hakuna mwingine
atayekamatwa zaidi yake.

Akaona njia sahihi ni kukimbia
hakutaka kujua hata wenzake wapo
wapi.

Akaamua kuvaa fasta ili
akimbie mule ndani kabla mtu
yoyote hajajua tukio alilolifanya,
mara akasikia
sauti ya mtu akigonga mlango......

_________________
MUENDELEZO
_________________
Kayoza akakaa kimya, sio kwamba hakuisikia hodi inayopigwa, ila alipigwa na ganzi kutokana na kuhisi kuwa mtu yoyote atakayeingia ni lazima amuhisi kuwa yeye Kayoza ndiye aliyemuua Stellah.

Mgongaji akaongeza nguvu ya ugongaji.

"Nani?" Kayoza aliuliza kwa sauti ya juu kidogo iliyoambatana na kitetemeshi,

"Mimi Tausi" Mgongaji mlango alijibu huku akiacha kugonga kwa kuamini amesikiwa na watu waliopo ndani,

"subiri kidogo au sema una shida gani?" Kayoza akauliza,

"Niruhusu niingie bwana, maswali ya nini?" Tausi aliongea,

"Ongea shida yako bwana, sio lazima uingie ndani" Kayoza aliongea huku akiwa hataki Tausi aingie ndani,

"mwambie Stellah anipe hela nikanunue mswaki na dawa" Tausi akasema, Kayoza akakimbilia suruali
ya stellah akaikota kisha akaisachi,

"mh..hamna kitu'' Kayoza akajisemea peke yake, kisha akasogea mlangoni

"kasema hana" Kayoza aliongea kwa sauti ya juu kidogo,

"khaa jamani hela
zote zile za kwenye pochi kazimaliza jana!?, Tausi aliuliza kwa mshangao.

Kayoza ndio akagutuka na kupepesa macho mule chumbani, ghafla akainama chini ya meza ilipokuwa pochi ya Stellah, akaichukua pochi
akatoa noti ya shilingi elfu kumi, akaenda hadi mlangoni, akaufungua mlango kidogo,

"mambo" Kayoza
akamsalimia Tausi,

"safi, vipi stellah
bado kalala?" Tausi aliuliza baada ya kujibu
salamu huku nafsi yake ikiwa na amani,

"yuko macho ila anaona
uvivu kuinuka kitandani" Kayoza alijibu huku akitabasamu.

"Na wewe uko poa?" Tausi alimuuliza Kayoza,

"Niko Poa, unaweza kuniambia nini kiliendelea baada ya mimi kunywa pombe jana?" Kayoza alimuuliza Tausi,

"Jana ndio nimejua kuna watu wana vichwa vibovu" Tausi aliongea huku akicheka,

"Unamaanisha nini?" Kayoza aliuliza,

"Yaani wewe ulikunywa bia moja tú na ukazima kabisa. Yaani kabia kamoja tu?" Tausi aliongea huku akiendelea kumcheka Kayoza,

"Baada ya hapo?" Kayoza aliuliza,

"Sisi tuliondoka na kuwaachia chumba. Sasa labda wewe ndio uniambie baada ya hapo mlifanya nini?" Tausi aliuliza ila kiutani,

"Na wakina Omary walielekea wapi?" Kayoza aliuliza,

"Jana tulichukua chumba kingine baada ya wewe kuzidiwa" Tausi alijibu,

"Kwa hiyo wewe ulilala na wakina Denis?" Kayoza aliuliza,

"Ndio, ila hatukufanya kitu" Tausi alijibu huku akijisikia aibu,

"Poa, Acha mimi nirudi kulala kidogo" Kayoza aliongea,

"Inaelekea mlikuwa na shughuli nzito jana usiku" Tausi aliongea huku akicheka,

"Ebu fuata kilichokuleta, kama huna cha kuongea ni bora uondoke" Kayoza aliongea huku akifunga mlango na kumuacha Tausi akiendelea kucheka.

"Hutaki kusifiwa?" Tausi aliuliza huku akiwa amefungiwa mlango kwa nje,

"Kwanini usijisifie wewe uliyelala na wanaume wawili?" Kayoza aliuliza huku akiwa ndani,

"Acha maneno yako ya kipuuzi" Tausi aliongea kwa hasira,

"Kwani yako ndio ya maana?" Kayoza nae aliuliza,

"Ebu muamshe Stellah nimsalimie shoga yangu" Tausi aliamua kubadili mada,

"Nimekwambia amelala, Kwanini huelewagi wewe?" Kayoza aliuliza kwa hasira huku akiwa ndani,

"Nilijua amelala na ndio maana nikakwambia muamshe, au mtu anayeamshwa ni wa aina gani?" Tausi alihoji huku akiwa nje,

"Ebu nenda bwana, mtaongea baadae akiamka" Kayoza aliongea,

"Ujue mimi ni shoga yake?, ebu muamshe nimuulize kitu" Tausi alikazania utasema alikuwa anajua kuwa Stellah hayupo tena duniani,

"Mimi boyfriend wake, nimesema muache apumzike" Kayoza aliongea kwa mamlaka,

"Umesema wewe nani wake?" Tausi aliuliza,

"Boyfriend wake" Kayoza alijibu,

"Leo ndio umekubali kujiita boyfriend wake, si ulikuwa unajifanya humtaki?" Tausi aliuliza huku anacheka,

"Hayakuhusu" Kayoza alijibu na kufanya kuwa kama wanasutana,

"Kwa hiyo ndio umegoma kumuamsha?" Tausi aliuliza huku akimcheka Kayoza,

"Nenda dukani, ukirudi utakuta nimemuamsha" Kayoza alijibu ili tu Tausi aondoke.

Baada ya tausi kuridhika na majibu ya Kayoza aliondoka na kuelekea
dukani.

Kayoza akaona hiyo ni nafasi nzuri ya kuuficha mwili wa Stellah,Akauchukua mwili wa
stellah na kuuingiza chini ya kitanda, na kisha akaenda bafuni na kukuta kuna taulo zimetundikwa ukutani, akaichukua moja kwa ajili ya kwenda kufutia damu iliyomwagikia sakafuni.

Akaichukua na kurudi nayo chumbani, sasa wakati anaangaika
kufuta damu sakafuni mara mlango
ukafunguliwa ghafla, alikua ni Tausi, alipoziona zile damu sakafuni alionekana kushtuka sana,

"vipi kuna usalama kweli?" Tausi aliuliza,

"upo shem" Kayoza alijibu huku akizuia hasira zake kutokana na Tausi kuingia bila hodi,

"Hizo damu za nini sasa?" Tausi aliuliza,

"Stellah alijigonga kidogo ukutani ndio damu zikawa zinamtoka puani"
Kayoza akatumia uongo kujibu,

"stellah mwenyewe kaenda wapi?" Tausi akauliza tena,

"kaenda kuoga" Kayoza akadanganya tena.

"Acha na mimi nikaoge" Tausi aliongea huku akinyanyuka ili aondoke, wakati ananyanyuka akadondosha dawa ya
meno, ikabidi ainame ili aiokote, ile kuinama tu, kwa ajili ya uchovu pia
na hangover alizoamka nazo akajikuta anapiga mweleka mtakatifu
puh, hadi chini, sasa akawa anajigeuza geuza pale chini, mara
macho yake yakagota chini ya uvungu wa kitanda,

"khaa naota au?" Tausi akajikuta amelopoka.
Ni kitendo bila
kuchelewa, Kayoza akaruka hadi
shingoni kwa tausi, ila hapa hakumnyonya damu ila alimkaba
shingoni kisawa sawa mpaka binti wa
watu akatoa shuzi zito alafu akatulia
kimya, hakutaka kumuua ila alitaka kumzuia tú asipige kelele na matokeo yake yakawa ni kuua bila kukusudia. Kayoza akazidi kuchanganyikiwa, Akauchukua mwili wa
Tausi nao akauingiza chini ya kitanda, Kayoza akawa kama chizi kwa maana alikuwa anazunguka tú ndani bila kujua anachofanya.

Baada kama ya dakika ilisikika hodi nyingine,

"Nani?" Kayoza aliuliza huku jasho la uoga likimtoka,

"Mimi muhudumu" Sauti ya kike ilijibu kutoka nje,

"Unasemaje?" Kayoza aliuliza,

"Nauliza kama mnajitaji kufanyiwa usafi chumbani kwenu" Mhudumu aliongea huku akiwa nje,

"Hapana hatuhitaji" Kayoza alijibu,

"Pia kama mtahitaji supu au chai vinapatikana pia" Mhudumu alizidi kuongea,

"Tukihitaji tutakuja wenyewe kuagiza" Kayoza alijibu huku akikereka kutokana na maswali ya huyo muhudumu,

"Alafu pia kama chupa za soda au bia chumbani kwenu, naziomba" Mhudumu aliongea pale nje ya mlango,

"Acha ujinga msichana, ujue huo ni usumbufu unatufanyia katika starehe zetu, au ndio mmefundishwa hivyo na bosi wenu ili nikitoka nikamuulize?" Kayoza aliongea kwa hasira baada ya kuchoshwa na maswali ya Mhudumu,

"Basi samahani kaka yangu, usiende kumwambia bosi wangu" Mhudumu aliongea huku akiondoka haraka haraka mlangoni mwa chumba alichokuwamo Kayoza.

Mhudumu wakati anaondoka, koridoni akapishana na Denis na Omary ambao nao walikuwa wanaelekea katika chumba alichokuwepo Kayoza, walifika mlangoni na kuingia bila hata kupiga hodi.

"bishoo vipi unambonji paka saa tano,
au binti kakupa vitu hadimu?" Omary
aliingia kwa staili hyo, ila kayoza hakujibu, alionekana ana mawazo
sana,

"vipi kaka mbona hivyo? Sie tuliechangia demu tuko poa hatuna
mawazo, we uliejilia mzigo wa peke
yako umeshika tama" Denis akaongeza neno tena, pia kayoza
hakujibu na wenzie wakawa wanaishangaa hiyo hali na mwisho wote wakakaa kimya. Mwishowe baada ya
ukimya mrefu,

"tunaweza kwenda au kuna kitu mnangoja?" Kayoza aliuliza,

"warembo wako wapi?" Denis nae akauliza,

"nimeua" Kayoza akajibu kwa kifupi,

"tunajua umeua Stellah, Tausi tumeua sisi"
Denis akasema uku neno kuua akijua kayoza kamaanisha ni kitendo cha kufanya mapenzi,

"au wameenda kupata supu moto?" Omary akatupia swali tena,

"wako chini ya kitanda" kayoza akajibu huku dhahiri uso wake ulionesha amechanganyikiwa.

Kwa kuwa Omary alikaa kwenye kochi, yeye
ndio akawa wa kwanza kutupia macho chini ya kitanda, aliona Stellah na Tausi wakiwa chini ya kitanda, ila hakuamini alichokiona, ilibidi asogee mpaka ilipo miili ya wakina Stellah na kuhakikisha mwenyewe kwa macho yake kuwa wale wanawake wawili tayari ni marehemu.

"Mungu wangu, umeua kweli" Omary aliuliza huku akiwa anasimama, Kayoza kuona hivyo nae allisimama na kwenda alipokuwa Omary na kumkaba shingo....

******ITAENDELEA******

the Legend☆
 
RIWAYA KIJIJINI : KWA BIBI.

MTUNZI : ALEX KILEO.

SEHEMU YA TANO.

______________
ILIPOISHIA
______________

Kwa kuwa Omary alikaa kwenye kochi,
yeye
ndio akawa wa kwanza kutupia
macho chini ya kitanda, aliona
Stellah na Tausi wakiwa chini ya
kitanda, ila hakuamini alichokiona,
ilibidi asogee mpaka ilipo miili ya
wakina Stellah na kuhakikisha
mwenyewe kwa macho yake kuwa
wale wanawake wawili tayari ni
marehemu.

"Mungu wangu, umeua kweli" Omary
aliuliza huku akiwa anasimama,
Kayoza kuona hivyo nae allisimama
na kwenda alipokuwa Omary na
kumkaba shingo....

____________
ENDELEA...
____________

Denis akanyanyuka haraka mithili
ya gari inayowaisha mgonjwa
mahututi hospitalini, lakini kayoza
alikua na kasi mara mbili, akawai
mlangoni.."please Denis na Ommy, nawaomba
mtulie rafiki zangu, nahitaji msahada
wenu" kayoza aliongea kwa upole,

Denis ikabidi arudi na kufunua godoro na
kuziangalia zile maiti, huku akionekana ni mtu mwenye maswali
mengi kichwani, baada ya muda
kidogo akagutuka,

"imekuaje kaka?" Denis
akauliza huku akiwa bado anaziangalia zile maiti,

"Kwanza kubalini kuwa upande wangu, alafu nitawaambia ukweli" Kayoza aliongea huku akiwatazama wenzake kwa zamu,

"Tuambie kwanza nini tatizo?" Omary aliongea huku akijishika shingo kutokana na kabali alipigwa na Kayoza muda mchache uliopita,

"Mimi niko upande wako, na nitakuwa upande wako" Denis aliongea huku akimuangalia Kayoza aliyeonekana kuchanganyikiwa,

"Hata mimi niko upande wako, haya tuambie ilikuwaje?" Omary aliuliza,

"jamani nitawaambia tu,
cha muhimu tuondoke eneo hili haraka iwezekanavyo" Kayoza
akaongea kwa kuwasisitizia wenzake,

"Ok, fasta basi" Omari
akawaharakisha wenzake huku akionekana mwenye wasiwasi.

Wakavaa haraka, na wakawa wanaelekea nje. Wakanyoosha moja kwa moja mpaka mapokezi,

"Mbona Mpo peke yenu, wenzenu wako wapi?" Dada wa mapokezi aliwatania,

"Bado wanajipodoa, si unajua tena mambo ya wanawake?" Omary alijibu huku akicheka,

"Haya, nawasikiliza" Dada wa mapokezi aliongea,

"Tumekuja kulipia chumba" Omary aliongea huku akimkabidhi pesa Mhudumu,

"Sasa mbona ya chumba kimoja?" Dada wa mapokezi aliuliza baada ya kuzihesabu zile pesa,

"Hicho kingine watalipia wadada" Denis alijibu,

"Na wakikataa?" Dada wa mapokezi aliuliza ila kwa utani,

"Wakikataa itabidi muwazuie na wawasaidie kufua mashuka" Omary nae alitania huku wakianza kuondoka na kumuacha yule dada wa mapokezi akicheka.

Njiani kila mmoja
alikua anafikiria lake,

"Tunaenda wapi sasa?" Kayoza aliuliza huku akiwa hana muelekeo,

"Itabidi turudi kwanza chuo" Denis alitoa jibu lililomfanya Kayoza asimame ghafla,

"Hamuoni hatari iliyopo mbele yetu? Sasa tukirudi chuo si naweza kukamatwa?" Kayoza aliuliza huku akiwa bado amesimama,

"Acha ujinga wewe, hakuna hata mmoja atayetuhisi sisi tunahusika na vifo vile" Denis alimwambia Kayoza,

"Kwa hiyo?" Kayoza aliuliza,

"Kwa hiyo turudi chuo, alafu tuangalie upepo unaendaje na tukiona mambo yanaweza kuharibika basi ndio tutaangalia namna ya kupambana" Denis alimueleza Kayoza,

"Alafu hili suala ni letu sote, sio lako peke yako" Omary nae akaongezea maneno yalimpa nguvu kidogo Kayoza na kukubali kurudi kwanza chuo.

Walienda mpaka jamatini ambapo ndipo zilikuwa coaster za kuwapeleka chuo, wakatafuta usafiri ambao ulikuwa upo tayari kuondoka na wakaingia, baada ya muda mchache gari iliondoka.

Walipofika eneo la chuo wakaingia kwenye chumba chao, Denis na Omari wakaingia kuoga,
Kayoza akajitupa kitandani ila sio kwamba alitaka kulala, hapana, mawazo ndio yaliutawala ubongo wake muda wote.

Ilipofika mida ya saa 10 jioni, habari zikaenea
chuo chote kuwa kuna wanafunzi
wawili wa kike wamekutwa wamekufa
Katika nyumba ya kulala wageni, kwa denis na Omari hiyo habari kwao
haikuwa ngeni ila hofu waliyokuwa nayo mwanzo sasa iliwazidia kupita kiasi.

Usiku wa siku hiyo, Kayoza hakulala kabisa kila dakika
alikua anazunguka chumbani tu huku tukio la kumuua Tausi likimrudia kichwani mara kwa mara pamoja na sura ya Stellah, wakina Omary pia hawakulala ni
kutokana na uoga, walikua
wanaogopa kulala wakijua kuwa
kayoza anaweza kuwaua pia.

********

Kesho yake asubuhi wanafunzi
wakatangaziwa waende wakaage miili
ya wenzao, na utaratibu mzima
utakuwa katika hospitali kuu ya mkoa
wa dodoma inayoitwa jenero hospital(general).

"Jamani mimi nitaenda kuaga pia, maana ni watu ninaowafahamu" Omary aliwaambia wenzake baada ya kupata ratiba kamili ya kuiaga miili ya Tausi na Stellah,

"Kayoza na sisi itabidi tuende, haina haja ya kuogopa kitu ambacho hatujahisiwa nacho" Denis alimshawishi Kayoza,

"Hapana, nyie nendeni tu, mimi siendi" Kayoza aliwaambia wenzake,

"Ilo futa kichwani kwako, watu wote wanajua ulishawahi kuwa na uhusiano na Stellah, sasa usipoenda watu watakuchuliaje?" Denis alimwambia Kayoza,

"Hivi nyie hamuoni hatari iliyo mbele yetu?" Kayoza aliuliza huku akisikitika,

" hakuna hatari yoyote kwa sababu hakuna atayejua ni nani amewaua wakina Stellah" Denis alizidi kumueleza Kayoza,

"Na pia usipoenda haitakuwa picha nzuri kwa watu wanakufahamu" Omary alichangia na mwisho Kayoza alikubali kuambatana na wenzie ifikapo saa kumi jioni.

___________________
SAA KUMI JIONI
___________________.

Wanafunzi wengi walijitokeza eneo la hospitali, pia Kayoza na
wenzake walifika kuaga miili ya wenzao. Eneo lote lilitawaliwa na vilio vya wasichana wa chuo pamoja na walimu wao wachache walioguswa na vile vifo.

* * * * * * * *

Baada ya wahudumu kukaa mda mrefu bila
kuona wakina stellah wakitoka, walipata wasiwasi kidogo na waliitana wenyewe kwa wenyewe na kuulizana bila kupata jibu la uhakika, na mwisho walipanga kwenda kuwaogongea, ila
walitaka kutumia njia ya kutaka kufanya usafi ndio iwe kigezo, wakanteua mwenzao mmoja akawagongee mlango.

Mhudumu alipofika mlangoni akagonga,
hakusikia jibu, akagonga tena kwa nguvu kidogo pia hakusikia jibu,
akarudi nyuma kidogo alafu akachungulia korido, hakuona mtu,
akaenda upande wa vyoo na bafu pia
hakuna mtu, akakata shauri ya kurudi kufungua mlango ambao ndani alikuwepo Stellah na Tausi, akanyonga
kitasa akazama ndani, akakuta hamna mtu,

"khaa! wametutapeli!" Mhudumu akashangaa moyoni mwake huku akiwa amejishika kiuno, wakati akiendelea kuwaza na kuwazua, mbele akaona suruali ya
kike iko chini pamoja na pochi, ndio akapata faraja kidogo,

"Hodi wadada" Mhudumu aligonga hodi ilihali ameshaingia ndani, lengo lake alitaka kujua wakina Stellah wapo upande gani, alijaribu kuita tena na tena bila mafanikio,

"Ebu Ngoja niwaokotee pochi yao" Mhudumu aliongea huku akiinama chini kuokota pochi, wakati anaokota ndio
akaona mkono wa mtu chini ya
kitanda, akashtuka, akasimama
akalinyanyua godoro kidogo, alichokiona kilipekea kupiga kelele
hadi akapoteza fahamu.

Alipopata fahamu alijikuta yupo hospital huku pembeni yake yuko polisi,

"habari
yako dada, unajisikiaje?" Polisi alimsalimia yule
mhudumu,

"nzuri" Mhudumu akajibu huku akishangaa mazingira yaliyomzunguka,

"unajisikiaje sasa, una nguvu
kidogo?" Polisi aliendelea kuuliza.

"najiskia vizuri" Mhudumu alijibu,

Polisi akatoa simu akapiga, baada ya
dakika mbili, akaja daktari na askari
mwingne, daktari akamuuliza
maswali mawili matatu mhudumu
kuhusu hali yake, kisha akampima
pima, alafu akamruhusu.

Akapelekwa kituoni kwa ajili ya mahojiano. Pale kituoni walimkuta askari mmoja kijana mdogo mdogo, mweupe ila alikuwa amevaa nguo za kiraia, kilichomtambulisa kuwa ni Askari ni saluti kadhaa alizokuwa anapewa na askari wengine. huyu polisi kijana jina lake ni Joel Minja, ila jina ambalo hutumiwa na wengi kumuita ni Sajenti Minja.

"Mkuu, binti mwenyewe ni huyu hapa" Askari aliyeongozana na Mhudumu wa bar alimuongelesha Sajenti Minja,

"Oooh vizuri, mpeleke kule katika chumba cha mahojiano, mimi nakuja" Sajenti Minja aliongea huku akimuangalia yule Mhudumu, kisha akaelekea nje ambapo alienda mpaka katika moja iliyokuwa imeegeshwa hapo nje na kuchukua simu, kisha akaelekea katika chumba cha mahojiano na kumkuta yule dada Mhudumu akiwa amekaa anamsubili.

"unaitwa nani mrembo?" sajenti joel Minja alimuuliza mhudumu.

"Sania" Mhudumu ndivyo alivyojibu,

"huna baba au ubini?
Jitambulishe majina yako yote matatu" Sajenti Minja akatia msisitizo,

"Sania Juma Baruti" Mhudumu akajibu,

"unakumbuka tukio lililosababisha
ukapelekwa hospitali?" Sajent Minja
akauliza tena.

Mhudumu akaelezea
mwanzo hadi mwisho.

"je unawakumbuka vijana waliongia
na hao mabinti?" Sajenti Minja akauliza,

"nikiwaona nitawajua" Mhudumu
akajibu kwa ufasaha kabisa. Baada ya mahojiano yule Mhudumu alipelekwa selo kwa ajili ya usalama wake.

Kesho yake mishale ya saa kumi jioni, Sajenti Minja akiwa na Askari wengine, wakamchukua Mhudumu na kwenda nae hospitali ili
akahakishe kama wale maiti ni wateja aliowapokea au sio wao

* * * * * * *

Baada ya wakina Kayoza kutoka kuaga
maiti, Omari akaaga anaenda msalani
kukojoa na kuwaacha kayoza na Denis wakitangulia kutoka na kwenda nje ya eneo la hospitali.

Omari alipotoka msalani akawa anaelekea nje kuwafuata wenzake, ndipo mbele yake akawaona Askari wapatao watano wakiwa wanaelekea upande aliopo huku wameongozana na msichana ambae hakuweza kumtambua kutokana na umbali ulikuwa kati yao, ila kadri walivyozidi kusogeleana ndipo sura ya yule msichana ilivyozidi kumjia, zilipofika hatua mbili kabla hawajapishana ndipo Omary alipopata mshtuko baada ya kugundua kuwa yule msichana ni Mhudumu wa ile bar ambayo Kayoza alifanya mauaji.

Omary aliuficha mshtuko wake ila sasa yule Mhudumu akawa anamuangalia sana Omary, Omary akatamani hata apotee ghafla kama upepo ila ilishindikana na akaamua aendelee tú kwenda mbele kiume.

Wale Askari na mhudumu walipomfikia Omary wakampita na kufanya Omary ashukuru Mungu baada ya kupishana nao.

Yule Mhudumu alipompita Omary, alihisi hiyo sura siyo ngeni kwake, alitembea hatua mbili kisha akasimama, ikabidi Askari wote nao wasimame, kisha Mhudumu akageuka na kumtupia jicho Omary ambaye nae aliwageukia na sura yake ikaonekana vizuri na Mhudumu na kumfanya Mhudumu atoe mguno wa mshtuko..

******ITAENDELEA******

Je dada Mhudumu wa bar amemtambua Omary?

Na kama amemtambua atamchoma?

Nini hatma ya kayoza baada ya mauaji aliyoyafanya?

the Legend☆
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom