Ripoti bado tu au kiini macho?

Magehema

JF-Expert Member
Aug 11, 2008
428
27
Wana JF, kuna tume iliundwa na aliyekuwa Waziri Mkuu ndugu Lowasa kufuatilia uimara wa majengo (ujenzi wa kufuata taratibu za kihandisi) mara baada ya kuanguka kwa jengo kule Changómbe. Mbali ya kuunda tume Mheshimiwa pia alimtimua Mhandisi wa Manispaa ya TMK. Ripoti yake vipi, bado haijatoka au ndo ilikuwa "sponging"?
 
No no no, ripoti ipo tayari, tunasubiri wafadhili ili tuifanyie upembuzi yakinifu.Baada ya hapo Mh. Pinda ataunda TUME kupitia matokeo ya TUME ya Lowasa, kabla haijapelekwa bungeni kwenye KAMATI ya ujenzi ambayo itatoa mapendekezo kwa Spika, ambaye ataikabidhi kwa Mh. Pinda ambaye atawapa wataalam wa ofisi ya Waziri Mkuu kwa mapitio kisha kuikabidhi kwa Mh. Rais. Mh. Rais ataikabidhi kwa TAKUKURU kuangalia kama rushwa ilikuwepo katika utoaji wa vibali. TAKUKURU itaunda TUME ya uchunguzi ikisaidiwa na TUME ya uhandisi ya halmashauri ya jiji............ I love TZ.
 
Ripoti nyingi tu zimetiwa kapuni kama zile
1. Mabomu Mbagala
2. Mapato ya Kituo cha Mabasi Ubungo
3. Ajali ya Mhe. Mwakyembe
4. Vinasasauti alivyowekewa Dr.Slaa
nk
 
Back
Top Bottom