Ridhiwan anapewa escort; Kwanini?

Hawana tofauti na Ben Ali wa Tunisia hili halikubaliki hata kidogo kwani hii nchi sio ya kifalme...
 
Nijuavyo mimi watoto wa marais wengi tu duniani(wanaounda first family) hupewa ulinzi na ama polisi,jeshi,secret service ama chombo chochote kinachosimamia usalama wa viongozi kwa nchi husika(ikiwa ni pamoja na kuwa na motorcade yenye escort ya walinzi) so Ridhwan kama mmojawapo wa watoto wanaounda first family ulinzi ni stahili yake...

Mkuu heri ya mwaka mpya!!
Uklipotea sana...
 
Wakuu sijui ninyi mtazichukuliaje habari hizi, kwangu mimi naziona ni habari za kusikitisha. Habari kutoka chanzo cha habari cha kuaminika kutoka Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Mwalimu Nyerere (JNIA), zinasema kuwa kijana, mtoto wa mkulu, Ridhiwan, kaonekana uwanjani hapo, ikisemwa kuwa ana safari yake binafsi, kwenda Dubai.

Nachelea kulia. Naomba nijikaze kiume, kijasiri ili niweze kulisema hili, naomba niwezeshwe, maana sasa nchi inakoelekezwa, aaaagh, basi wahenga na Mungu wanajua...KAPELEKWA UWANJA WA NDEGE NA ESCORT AKIWA KATIKA GARI YA IKULU, lenye ngao na polls mbili lakini HALIKUWA NA BENDERA. Mbele kulikuwa na gari ya escort ya king'ora na nyuma gari ya usalama, so the source said.

Kuna mengine tutayaongeza. Kuna kazi nafanya mara moja wakuu, just kuanzia hiyo. INASKITISHA JAMA, THIS IS EXTREMEEEEEEEEE

Endelea kulalamika... wajanja wanakula bata... nenda kafanye kazi!!:coffee:
 
Kwangu mie sioni tatizo. Familia ya Rais inahitaji kulindwa. Suala la kupelekwa na escort ya polis na usalama ni jambo ambalo siyo tatizo kubwa. Maana ukiwa Rais, unaongeza idadi ya maadui. Ukilindwa wewe tu, adui zako watakukosa na wakimpata mke au mtoto, hasira yao huishia hapo. Hivyo, maadam Rais wetu alishapewa Ukuu na Tume Feki ya Uchaguzi, basi hatuna budi kukubali na hayo!! Hofu yangu ni kutumia Gari lenye Nembo ya Ikulu.
 
Nijuavyo mimi watoto wa marais wengi tu duniani(wanaounda first family) hupewa ulinzi na ama polisi,jeshi,secret service ama chombo chochote kinachosimamia usalama wa viongozi kwa nchi husika(ikiwa ni pamoja na kuwa na motorcade yenye escort ya walinzi) so Ridhwan kama mmojawapo wa watoto wanaounda first family ulinzi ni stahili yake...

Happy New Year Cousin...
 
Binafsi sina tatizo juu ya kupewa escort Riz1. Tatizo ni jinsi gani wanatumia mali ya umma kwa fujo. Fikiria, hata kama ana threats Je, gari moja ya Polisi isingetosha? Hapa si ulaya Bwana! Atumie mali ya watanzania kwa kiasi, hapo tutamwona kidogo mstaarabu.
Mtoa mada ameona jumla ya gari 5 zikimpeleka riz1 uwanja wa ndege! hebu fikiria jamani... Kweli tunamwonea wivu?

Riz1, ungetuliza mapepe kwani sisi si wapiga kura wako. Shuka huko ulipo matawini!
 
Nijuavyo mimi watoto wa marais wengi tu duniani(wanaounda first family) hupewa ulinzi na ama polisi,jeshi,secret service ama chombo chochote kinachosimamia usalama wa viongozi kwa nchi husika(ikiwa ni pamoja na kuwa na motorcade yenye escort ya walinzi) so Ridhwan kama mmojawapo wa watoto wanaounda first family ulinzi ni stahili yake...

Duh! Nisaidie mkuu hivi kwa sheria za kimataifa na serikali ya Tanzania mtoto ni mtu mwenye umri gani? Ridhiwan bado ni mtoto?
 
Tunapoteza muda humu ndani kujadiliana na watu wasiojua taratibu za mambo ya ulinzi na usalama wa viongozi na taratibu zake matokeo yake watu wanachangia kishabiki zaidi na kulinganisha taratibu zetu na za ulaya na hata marekani.

Kwa kifupi ni kwamba kwa hapa nchini kwetu kabla ya kuchakachuliwa kwa katiba huko Zanzibar viongozi waliokuwa wanapata ulinzi na escort ya usalama wa Taifa ni wale viongozi top five (T5) yaani Rais mwenyewe JMT, makamu wake, waziri mkuu, Rais wa Zanzibar na waziri kiongozi wa Zanzibar ila kwa sasa kuna mabadiliko madogo yaliyofanyika Zanzibar ambapo kuna makamu wa Rais wawili na hivyo kufanya kuwa na T6 badala ya ile ya awali na hakuna kiongozi mwingine anayepewa escort ya usalama wa Taifa vinginevyo kuwe kama kuna hali hatarishi ya usalama au vitisho au machafuko anaweza kupewa ulinzi kulingana hali halisi na hiyo hutolewa na yule anayehusika na ulinzi wa Rais na ni kama pendekezo lakini haipo kwenye sheria zetu na ndiyo maana unaona marais waliotangulia walikuwa na watoto lakini hakuwa na matumizi ya mali na wafanyakazi kwa aina hii ya mkwere.
 
wanapewa ulinzi kutokana na threat level...escort ya magari matatu ni no no...mara nyingi wanapewa dereva na mlinzi na gari moja, huyo kikwete ana watoto nane sijui sasa kama wote wanapewa same treament si mzozo huo.

Niliwahi kushuhudia jinsi ulinzi wa first lady wa nchi jirani zetu hapa Africa Mashariki siyo Rwanda wala Burundi; ulivyokuwa mkubwa alipokuja kula dinner pale hoteli niliyokuwa nimefikia kwenye hiyo nchi. kwangu mimi it was a first experience maana walinzi tena wanajeshi siyo hawa polisi wetu visible na invisible. Maana hata kwenda kula ilibidi tupite kwenye scaning machine kufika restaurant nilipouliza walinishangaa saana; kwani ninyi nchini kwenu fisrt family hailindwi? Well sikuwa na jibu for sikuwahi ona nikajibu simply sijui kisheria lakini kwa macho sijawahi ona kama hivi. Lakini kwenye group langu kulikuwa na western citizen akaniambia ukiona hivi basi ujue crime level ni kubwa kwa nchi husika......

So tunachojifunza ni kuwa pengine crime level imeongezeka na risk inakuwa kubwa kwa families husika ku walk 100% free bila visible na invisible securities; swali ni je hii haisumbui vichwa vya viongozi kwamba if this will continue then haitaishia kwa first family bali even associated leaders families? kumbuka kuna Mbunge alisha wahi kuomba walindwe if am not misteken bunge lilopita (9). Na je hiyo average cost ya kumaintain those securities nchi yenye poverty level kama yetu itamudu? It tells a lot to the level of democracy na equity ya nchi husika. Badala ya kuona wivu I think we need to think more into those lines ili tuzuie hii hali kabla ugonjwa hauja anza rasmi, kwani prevention is better than cure; Leaders wake Up the country is going astray.
 
Assume the following:

  1. Habari hii ni sahihi
  2. Rizwan anastahili kupewa ulinzi kisheria za nchi
Je ni haki kutumia magari hayo matatu kwenye msafara wake?

Je siku nyingine wakimrusha kwa Helikopita itakuwa ni sahihi?

Inaingia akili kuwa usalama wa Rizwan unatishiwa kiasi hicho?

Huyu mtoa mada sioni kama angetueleza endapo angeona Rizwani akishuka katika gari ya Ikulu ampapo ndani yake kuna wanausalama kwasababu matumizi mabaya ya namna hiyo tumeyazoea. Nenda mashuleni utakuta STKs ndizo zinawapeleka watoto wa wakubwa shule!

REMEMBER
Wrong is wrong even if everybody does it and Right is right even if nobody does it!

Akhasanteee Mkuu!
Tanzania na Baadhi ya Watanzania utadhani wako usingizini kwenye majinamizi au wakiangalia riwaya au tamthiliya wanapojadii maswala nyeti yahusuyo mstakabali wa nchi.Utaona watu wanatetea kwa nguvu zote ujinga kama huu wa " watoto" wa viongozi! Hivi, mwanamme mzima mwenye mke na watoto bado tunamhesabia kuwa ni mtoto? Tanzania ni nchi inayoendekeza ukupe na utegemezi hasa katika ngazi za juu kwa sababu ya ufisadi! Kwanini tusione mtindo huo huo kwa "watoto" wa wakulima na wafanyakazi maskini ambapo tuone "wakirithishwa" ufukara wa wazazi wao? Sijui kama naeleweka hapa. Ninachotaka kusema ni kuwa UTAWALA NA MARUPURUPU YAKE HAUNA UBIA!" MARUPURUPU AU FRINGE BENEFITS KWA KIMOMBO NI "ASANTE" KWA MACHUNGU YATOKANAYO NA SHURUBA ZA KUTUMIKIA.SASA AKINA RIZIWANI TUNAWAPA ASANTE AU POLE KWA LIPI?YEYE SI ANAJIPATIA MSHIKO HUKO KWENYE UWAKILI KWA KUWABAMIZA WANYONGE? TUNAMPA TENA ASANTE?!loooh!
 
Kwangu mie sioni tatizo. Familia ya Rais inahitaji kulindwa. Suala la kupelekwa na escort ya polis na usalama ni jambo ambalo siyo tatizo kubwa. Maana ukiwa Rais, unaongeza idadi ya maadui. Ukilindwa wewe tu, adui zako watakukosa na wakimpata mke au mtoto, hasira yao huishia hapo. Hivyo, maadam Rais wetu alishapewa Ukuu na Tume Feki ya Uchaguzi, basi hatuna budi kukubali na hayo!! Hofu yangu ni kutumia Gari lenye Nembo ya Ikulu.

Rais fisadi ..lazima watoto wake kulindwa.....kwa misafara...Nyerere yeye watoto wake tulikuwa tunaruka nao majoka rungwe au kwa arusha tulikuwa tunakutana na makongoro na dada yake Anna....muziki hakuna...kulala.....kila mtu anajuwa ni watoto wa Rais..na hakuna anayewafanyia fujo...na hasa wale wa kiume sometimes walikuwa wanagombana na watu kama vijana wengine na nothin happens...
watu wa secret service ..hutoa invisible protection kwa watoto...[what was required was just to know where are they at any given time ...ili hata mzee akiwaulizia mara moja wanajuwa wako wapi....kumbukeni enzi hizo hapakuwa na simu za mkono]...isitoshe wakati wa vita mwalimu alipeleka watoto wake mstarii wa mbele....sasa hii ya wazi kama vile amekuwa kiongozi its too much....
MWINYI nae hakufikia hapo...family yake waliishi low profile life beside mkewe ambaye alikuwa anatajwa japo alikuwa hapewi motorcase escort......Kina Abassi mwinyi watu walikuwa wanalewa nao kinondoni....huyu hussein alikuwa anapiga day worker pale kwa Prof Kairuki...
Mkapa watoto wake hawajawahi kuwa na mpambe..beside same arrangement ya secret service ambayo hata wao ni vigumu kujuwa wanafuatiliwa.....au tunaitwa they have invisible handlers...they were just having there bears without any worries at various pubs even when the time there father was at the centre of accusation...mama yao beside all hajawahi kuwa na motorcade......
Sasa what special is Rizwani ...mpaka awe na wapambe wa dhahiri..na juu yake awe na escort....what a waste...???
 
Hiyo ni dalili ya kutokubalika kwa jamii, watoto wa madikteta tu ndio huwa wanalindwa lakini siku zao zinahesabika nimeshasema hata mtoto wa Mubarak Gammal aliyekuwa anategemewa kumrithi baba yake leo yuko wapi na analindwa na nani amekuwa kama kuku wa kienyeji huko UK, give Ridhiwan time you will see him hanging on streets soon.
 
Kulikuwa na taarifa za kiintelijensia zikionesha kuwa angedhurika na hivyo Mkuu wa nchi angeathirika kisaikolojia na kuacha kushughulikia matatizo ya wananchi hivyo kuagiza yafanyike uliyoyaona mkuu. LOL.

You may be right if you are! except you are missing a point of whether Intelligence sources also warrant a "presidential facilities" to protect him?
 
Wivu wa kijinga huuu........ Ridhwan sio mtoto wa mkulima ni mtoto wa Rais wa nchi. Kwa hili umechemka.

Pole sana kwa mawazo mgando yaliyokosa mantiki. Nilichojifunza humu JF ni uhusiano uliopo kati ya tabia ya mwanaJF na jina lake la kiJF. There is a very good relationship. Kama huyu jamaa jina lake anaitwa 'Kandambili' sasa kuna haja gani hata ya kuchangia hoja yale wakati yeye anavaliwa na kukanyagwa na watu?
 
huyu ni **** acheni lumjadili. tujali mustakabali wa taifa letu, matatizo ya umeme nk. sana sana namtegemea sana pale kisutu 2016
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom