Rhoda Kunchela, Mbunge wa CHADEMA Katavi akamatwa na Polisi, anyimwa dhamana

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,765
218,383
Jeshi la Polisi Mkoani Katavi linamshikilia na kunnyima dhamana Mbunge wa Viti M ( 685 X 640 ).jpg


Rhoda Kunchela ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Katavi amekamatwa na jeshi la polisi mkoani humo na amenyimwa dhamana

Bado haijafahamika sababu za kukamatwa kwake, lakini inadhaniwa kwamba sababu ni ile ile ya siku zote ya polisi kujihusisha na ulinzi wa CCM kufa na kupona.

======

Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Katavi (CHADEMA) ambaye pia ndio Mwenyekiti wa Chama mkoani hapo, Rhoda Kunchela anashikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani Mpanda kwa kosa la kukiuka masharti ya dhamana yake.

Mwanzoni mwa mwezi Januari, mwaka huu, Kunchela na Viongozi wengine wa chama hicho walikamatwa na Jeshi la Polisi Mpanda baada ya kuuvamia Mkutano wa hadhara wa Mbunge huyo na wananchi kwa madai ya alifanya mkutano bila kuwa na kibali.

Mkutano huo uliofanyika katika Viwanja vya Maridadi Kata ya Majengo Manispaaa ya Mpanda, Polisi walivamia na kuchukua computer mpakato (laptop) iliyokuwa ikitumika kurushia matangazo. Mkutano huo ulilenga kusikiliza kero za wananchi kabla ya kwenda Bungeni.

Baadaye viongozi hao waliachaiwa na kwa dhamana ambapo miongoni mwa masharti waliopewa ni kuendelea katika Kituo Kikuu cha Polisi Mpanda wakati uchunguzi wa kesi yao ukiwa bado unaendelea.
 
Police wa Tanzania wanatia huruma mno...kufanya kazi kwa maagizo ya CCM....

Wengi wao ukiwahoji wanasema..ndiyo hivyo kaka tunatii amri za wakubwa... CCM ndiyo kila kitu msitulaumu sisi jamani...tuna familia pia na haya mengine yanasikitisha kwa kweli.
 
Pale manunuzi yanapokwama.. Meya wa Moshi nae anapitia kipindi kigumu sana.. Siasa zimeshikwa na washamba, wasiokuwa na historia wala talanta ya siasa..
 
Yote hayo ni hofu iliyozaa chuki kwa upinzani bila kuwa na hoja! So nguvu ndio zima moto kwao.

Tatizo upinzani nao hawajielewi, sijui wanapewa nn na kusahau matamko na nia yao ya kuwa wapinzani. CCM pasua kuchwa CHADEMA umiza kichwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
DJkus,

Siwezi kuwalaumu opposition on this wanapita njia ngumu sana. Na hiyo process inapanda chuki kwenye jamii.Sasa hivi watua hata kuaminiana kumepungua sana.Kuleta very un health speculations. Chukulia mitazamo kwenyehoja mbali bila hata kuangalia undani watuwanachukua upande.
 
Back
Top Bottom