RFID TRANSPONDER: Teknolojia ya kupandikiza ‘chip’ kwenye mwili wa binadamu

Hashpower7113

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
1,353
2,137
Bila shaka umewahi kukutana sana na stori za watu kupandikizwa kifaa fulani cha mawasiliano mwilini, kisha kifaa hicho kikawa na uwezo wa kuwasiliana na kompyuta, kwa lugha nyepesi mhusika akawa na uwezo wa kuwasiliana na kompyuta kwa urahisi zaidi.

Pengine utakuwa umewahi kuona kwenye filamu za kipelelezi, hasa za Hollywood kuhusu teknolojia hii, lakini pengine unajiuliza, uhalisia wake ni upi? Ukiachana kwenye filamu, je katika maisha ya kawaida inawezekana mtu kupandikizwa ‘chip’?

Kama inawezekana, nini hasa kinachofanyika na teknolojia hii inafanyaje kazi? Ni kwa msingi huo ndiyo maana leo nataka tujadiliane kuhusu teknolojia iitwayo RFID (Radio Frequency Identification).

Hii ni teknolojia ya kupandikiza kadi ndogo sana ya mawasiliano (microchip) kwenye ngozi ya binadamu. Kadi hii huwa na ukubwa wa kama punje ya mchele na huwekwa katikati ya kidole gumba na kidole cha pili kwenye mkono wa kushoto au wa kulia, na wengine huipandikiza kwenye bega.
human-microchip-implant.png


Mwanasayansi wa kwanza kufanya majaribio ya kupandikiza kifaa hiki, alikuwa ni Kevin Warwick mwaka 1998 ambaye alikaa na kifaa hiki mwilini kwa muda wa siku tisa na alikitumia kufungua milango, kuwasha na kuzima taa pamoja na kurekodi matukio mbalimbali.

Daktari wa nchini Uingereza, Dr Mark Gasson naye alifuatia kufanya majaribio ya kupandikizwa kifaa hicho Machi 16, 2009 na mpaka leo bado anacho mwilini na kuleta mapinduzi makubwa ya jinsi mwili wa binadamu unavyoweza kuunganishwa na mifumo ya kompyuta.

Kifaa hicho kinachopandikizwa, kinakuwa na namna za utambulisho ambazo zinaweza kusomwa na vifaa vya kidijitali vinavyotumia teknolojia ya ‘Bar Code’ na huwa kimeunganishwa kwenye database yenye taarifa zote muhimu kuhusu mtu husika.

Kwa hiyo, mtu mwenye kifaa hiki mwilini, hahitaji kubeba kitambulisho chochote mwilini kwa sababu taarifa zake zote anatembea nazo mwilini.

Kama amepata matatizo ya kiafya, akifikishwa hospitalini, haraka chip yake itatoa taarifa zake zote na rekodi za ugonjwa, kama amepatwa na matatizo ya kiusalama, kama kutekwa au kupotea, taarifa zake zitaonekana kwenye vyombo husika mara moja, atakuwa na uwezo wa kufungua milango inayofungwa kwa namba maalum kwa kunyoosha mkono wake tu.

Atakuwa na uwezo wa kuwasha mifumo mbalimbali ya kielektroni bila kutumia kifaa chochote, ile chip yake ndiyo inakuwa kila kitu, akifika mahali kwenye mashine zinazoitambua, zinai-scan na kumpa ruhusa ya kufanya anachotaka kukifanya.

Kwa sasa, wanasayansi wapo katika jitihada kubwa za kuunganisha RFID Microchip na mfumo wa GPS (Global Positioning System) ambao hutumika kuonesha mahali kitu kilipo kwa wakati fulani kwa kuunganishwa moja kwa moja na intaneti.

Lengo hasa, ni kuongeza ulinzi kwa watu wenye kifaa hiki mwilini kwa sababu sasa watakuwa wakionekana mahali popote walipo duniani, tofauti na sasa ambapo vifaa hivyo huwa na uwezo wa kuonekana kwenye mashine maalum zikiwa umbali fulani tu.
maxresdefault.jpg


Kwa hiyo suala la kupandikizwa chip mwilini, si geni duniani! Tayari kuna watu wanaishi na hizo chip ingawa si kweli kwamba zinaweza kurekodi matukio yanayotokea au kutumika kwenye masuala ya ujasusi, badala yake zinaweza kuonesha mahali mtu alipo pamoja na taarifa zake muhimu, hasa kama zimeunganishwa kwenye mfumo wa GPS.

Inaelezwa kwamba kwa sasa teknolojia hii inauzwa ghali sana na ni watu wachache wanaoweza kumudu kuwa nayo wakiwemo viongozi wa mataifa makubwa wanaolindwa kwa karibu, lakini ni suala la muda tu kabla teknolojia hii haijaanza kusambaa duniani kote kwa bei ambayo watu wengi zaidi wataimudu.

Kama una mwanao mtukutu ambaye hataki kusoma, ukimuwekea ‘chip’ hii, utakuwa na uwezo wa kuona nyendo zake zote kuanzia asubuhi anapotoka nyumbani. Kama una mwenzi wako ambaye anapenda kuchepuka, pia utakuwa na uwezo wa kufuatilia nyendo zake zote, sehemu anazokwenda, watu anaokutana nao na kadhalika! Ni suala la muda tu! Yajayo yanasisimua sana.
british-companies-implanting-microchips.jpg
 
Wengi wata angamia kw kukosa maarifa Maaana Huko tuendako N hatar Wachache sana wataweza kujinasua kweny mitego ya mpinga kristo (lucifer)
Mpaka sasa wote tayari tumeshaingia, labda kama mkuu wewe hutumii simu wala vifaa vyovyote vya kiteknolojia! Tuache maandiko yatimie, hakuna namna!
 
Nikuukize ivii Anaetumia dawa za kienyeji na mchawi wote ni kitu kimoja?
Kw maono yangu tu Nazani Mtu yyte kwa sasa akitumia lugha nyepesi tu ya ushawishi ujoin freemason Utompinga Maaana Huna amin kwa kutumia simu au technology yyte Unakua Tayr upo ndani ya mfumo wak illuminat
 
Back
Top Bottom