Revealing: Nani wametoa vibali vya kuishi/kufanya kazi kwa watu hawa?

Danniair Tuwaache wachina wapige kazi, maana watanzania ni kama miungu watu, mtu unamtafuta fundi akufanyie kazi, sasa wewe unageuka mtumwa, yaani kama anakufanyia bure, na kazi yenyewe haina viwango, naomba nitoe mfano niliwahi kumpigia simu fundi selemala aje nyumbani nimpe kazi, alikuja baada ya wiki, kazi ilikuwa ni kutengeneza shelf ya kuweka viatu, nikamwambia nahitaji kubwa, akasema nimpe elfu 30, nikampa,

basi kila nikipiga simu kumuuliza kama iko tayari mara anasema ameenda kuzika, mara naimalizia, hiyo ilikuwa mwezi wa pili, tukasumbuana sana mara nyingi nikifika kiwandani kwake na kumpigia simu kwa pesa zangu mara nyingi, aliponambia ipo tayari nikaenda nilivyoiona yaani ni kituko nikaondoka bila kuaga hadi leo sijaichukua, na fundi hata hajajiuliza kwanini niliamua kuiacha sasa ni mwezi wa saba,

nikaamua kuisamehe sababu niliona nitaendelea kuumia kwa kumpigia simu na kuchoma petrol kwa kitu ambacho sitakipenda, nikaamua kwenda dukani kununua shelf za kichina dukani mbili na kila moja inauzwa elfu 12, mbili kwa elfu 24, kumbuka fundi wa kitanzania nilimlipa elfu 30, na akanisumbua sana hatimae akanitengenezea kituko ambacho ningekiweka ndani ungekuwa ni uchafu.

sasa hawa ndio aina ya wajasiliamali wa kitanzania ambao mtoa mada anataka waachwe peke yao bila ushindani wa kibiashara,
hivi ujiulize kwanini wachina wanapata kazi zote hizo? ukweli ni kuwa sisi u-capitalism wetu ni uchwara kama alivyowahi kuandika Ayoub Rioba katika moja ya makala zake

ndugu zangu itachukua muda sana kufanya biashara ktk kiwango kitakachowaridhisha wateja na kukubalika na kila mtu
yangu hayo tu
 
Last edited by a moderator:
  1. umesahau wale WAZUNGU CIA wa TANESCO
  2. umesahau wale wazungu wa THT na CLOUDS
  3. umesahau waarabu/wayemen wanaojiita wa saudia wa HOME SHOPPING CENTRE
  4. umesahau waZanzibari
  5. umesahau Malawi wiliopo mpaka Jeshini kwetu
  6. umesahau Waingereza wanaijidai kufundisha kiingereza kumbe wanazuga tuu
  7. umesahau wa Zaire wanaojifanya wanenguaji
  8. umesahau wa Ethiopia ambao hata sijui wanafanya nini hapa mjini
  9. umesahau wa Somali ambao wanafanya hizo kazi unazolilia
  10. umesahau wa Marekani na kutuletea kundi la CIA kwa mgongo wa Peace corps
  11. umesahau wa kuwa Mtwara wamejazana hao wote usiowataka kwa sabau wote nyie mnataka kuzuga na vidigrii vya kufoji huku hatuna wataalam wa gesi


acha hizo

mimi naona bora tuu hawa wageni waje tena kwa wingi. Tumezidi uzembe. Hivi how hard is it kutengeneza traffic lights?
 
BORGIAS Seems that tuli assume majukumu makubwa ya africa na udnia kw au jumla huku tukiwa bado saana.Sasa tumejiweka kuwa vulnerable sana.Sasa vita na malawi si tunajipeleka kuuwa askari wetu?Kwani the enemy within atakuwa palipo roho yetu.Yote haya tuliyajua kipindi cha kupigana na makaburu na mabeberu.Sasa tumejiweka machinjioni.Vijana wetu wanaangalia zaidi virushwa vya kila siku vya kupata bia, kuzaa na kuendehsa magari mjini basi.Vyote hivyo navyo si hata endelevu.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: bdo
Wabongo kazi za kujiajiri hatuwezi wengi tukishapata ka-degree kamoja kutwa kucha na bahasha unatafuta kazi za kuajiriwa.Kwani kabla hao wachina na wahindi hawajaja kwanini nyie wabongo msizifanye hizo shughuli.?

Tafuta frem na wewe fungua uwape ushindani kama unaweza. WACHA KULALAMIKA WACHINA WANATOA HUDUMA NZURI SANA.

Hili nalo neno ingawa linauma kwa kichwa kweli.
 
Wachina linapokuja suala la kitaifa huwa kwao hata haki za binadamu si kitu na mara nyingi haki za binadmau ani adui yao linapokuja suala la maslahi ya taifa.

Warusi nao walitumia sana malaya wa kwao na watoto mayatima waliopelekwa US kuweza jenga base ya espsionage na mapandikizi ya viongozi nje ya nchi.Wachina,wahindi, thai, Soviet countries na nchi nyingine amabyo imefikia mahalia pa kutoangalia tena haki za watu kama yalivyo maslahi ya taifa au ya wkaubwa wachache.hawa malaya watapata access kwa kila raia muhimu wa nchi.Mawaziri, wana usalama, wafanya biashara wakubwa, wake zao,, watoto wao etc na mwisho wa siku watajenga base ya kusaidia china vyema zaidi.Kwa ujumla uhalifu hunenepa sana katk hizi biashara,kwani ahta ungana silaha zinauzwa vyema deal ikichezwa katk madanguro na macasino.

Mkuu Nicholas: nimekupata, hii ni elimu mpya ambayo hata sijawahi iwaza kabla, tukiacha utani na masihala - basi naona kama kweli njia hii itatumika au inatumika, basi Tanzania imekwenda yote, na ninadhani kwa wao (wageni) ni uzalendo wa hali ya juu kwa nchi zao, hivi hata sie tunaweza fanya hivi kwa taifa letu? nabadiri nia yangu ile, thanks mkuu sijui kama wengine wanafahamu hili?thanks
 
halafu mtawasikia wakiendelea kusema CCM itaendelea kutawa so what? ili iweje? by Msigwa
nafasi za ajira wameziacha zikachukuliwa na wageni wao na vitambi vyao haiwahusu.
 
Nenda k'koo kaone wachina wanavyofanya kazi za wazawa mpaka kupiga picha za paspot na kuuza vyombo na mapazia.

Haya ndo matokeo ya serikali dhaifu.

Serikali imara ingeweka vigezo vya kumruhusu mgeni kuja kuwekeza nchini, mfano awe na mtaji usio pungua 100m kiasi kwamba anaweza kuajiri wabongo. Hii ni kuacha nafasi ya uwekezaji wa mdogomdogo kwa wabongo wenyewe wenye mitaji midogo ya vikoba, Saccos, NMB, Access Bank, Kiinua mgongo, nk.

Waulize jamaa zako waliojichimbia Marekani na Uingereza, je hizo kazi wanazofanya hakuna wenyeji wa nchi hizo wa kuweza kuzifanya? Halafu mtu huyu ndiyo wa kwanza kuwahi foleni WesternUnion na MoneyGram kwenda kupokea fedha kutoka kwa ndugu zake Ulaya wanaoishi kama wageni lakini yeye ndiyo mstari wa mbele kupiga vita wageni.
 
System nzima imeoza. Ni mpata tuondokane na hii CCM ndipo tutakapoweza kuikomboa hii nchi. Kwa vingine tutalia tu!!
 
Wana JF,

Imefika wakati sisi wenye nchi tuseme ni akina nani, (tuwataje kwa majina pamoja na mambo mengine wanaofanya haya):

-Wanawanyima wazawa ajira na kuwapa wageni (hasa waasia) na wapi walipo. mf. masonara waasia weusi waliofungiwa mtaa wa Indira Ghandhi tujue ni nani (M-tz) kawapa kibali cha kufanya kazi hizo.

-Wachina wanaofanya kazi cha kuchoma magrill badala ya wazawa mf.kampuni ya Hu Tuo iliyoko Msasani. Je, sisi hatuwezi kazi hizo au tumalize madigirii yetu na kwenda kuajiliwa huko kwani nyumba karibia zote zinazojengwa Dar grill zinatengenezwa na wachina. Vile vile frem karibia zote ktkt mwa jiji zinarembeshwa na wachina!!!!!

- Wachina wanaosukuma mikokoteni nani kawaleta humu Tz kufanya hayo? Tunawajua: Jf tuwekeeni nafasi maalumu tuwataje hawa wa-Tz wenzetu wapenda rushwa huku wakituangamiza kwa kuwathamini wageni na kudhalilisha wazawa. Hawa wa-tz wasio na utu wenye kuangalia mifuko yao wakiisahau jamii yao nyuma.

-Waasia waliojificha huko viwandani keko/chang'ombe (nasikia sijawaona).

-Wakenya na waganda eti kwa kuwa wanajua kiingereza kutupita.

-Wachimba madini yetu, mf. nasikia huko Morogoro kuwa wanaojiita wamisionari lakini usiku ni wachimba madini yetu. Tuwataje kwa majina ili kumsaidia rais na kuzilinda mali zetu.

- n.k, n.k, n.k...
Ndugu yangu hata ukiwataja hao haitakusaidia kwani unaweza kukuta watu hao ni mawakala wa viongozi wetu, kwani unafikiri waliingia humu kwa kupiga mbizi? waliingia kweupe na jua la utosini likiwaka! Kwa maana nyingine wapo hapa ki-halali?!
 
HR Manager wa NIC BANK TANZANIA LIMITED (Mhindi na certificate ya usecretary), pia kuna Muchiri (Mkenya) ni wabaguzi kinyama. Kila kukicha wahindi wanaajiriwa kwa mishahara minono ila Mtanzania anakula clerk wages hata kama una Masters.
Mzalendo JR,
Lengo la biashara siku zote ni faida zaidi na zaidi. Sasa hebu tutafakari. Inakuwaje mfanyabiasha anayetaka faida zaidi na zaidi amwajiri mtu atakayemlipa mshahara wa juu na amkatae yule wa mshahara wa chini? Hapa ndio inabidi tuwe wakweli, perfomance ya watanzania ni ndogo kwenye kazi (wavivu) na mbaya zaidi ni wezi. Huo ndio ukweli. Ndio maana hawa wafanyabiashara wako radhi kulipa mshahara mkubwa kwa wageni.
 
Mkuu Nicholas: nimekupata, hii ni elimu mpya ambayo hata sijawahi iwaza kabla, tukiacha utani na masihala - basi naona kama kweli njia hii itatumika au inatumika, basi Tanzania imekwenda yote, na ninadhani kwa wao (wageni) ni uzalendo wa hali ya juu kwa nchi zao, hivi hata sie tunaweza fanya hivi kwa taifa letu? nabadiri nia yangu ile, thanks mkuu sijui kama wengine wanafahamu hili?thanks

Ninachojua ni kwmaba kuna makabila bongo dada wakiolewa basi huwapelekesha waume zao hadi mashemeji na wakwe wanalia kuwa kamwekea ndugu yao limbwata.Mume hufanya kila kitu upande wa mwanamke.Ila sijaona wengie wakifanya vitu kama hivyo kwa taifa.

Na sijaona wanaume wakioa wageni kuweza waconvince wahamishie projects TZ, wengi hubanwa kwa woga na siku za mwisho huanza ishi kwa hofu ya kurudishwa bongo.Kwa ujumla hatuna malengo wengi wetu.Wachache ndio huja na viproject vya kizushi na kuta media haraka haraka na baadaye huishia kama mshumaa.Sijasikia Serikali ikisaidi wabongo kufungua migodi nchi kama south,kongo, na kwingineko huku serikali aikwafuatilia ili wakidhurika iweze watetea, na pia kwa jinsi CCM wanavyoponda nchi bila kuwajibika achili ambali kujiwajibisha nani atapambana kwa faida ya nchi aliyoicha imeoza hivi?Wengi wanajua ukisaidia projects za serikali unaweza kufa au kurudi na kilema na ukakuta hela zimeliwa na hakuna w akumuuliza hata upate mafao.Na kama ukikuta hazijaliwa kupewa ni kama wazee wetu waliopigana vita vya dunia na mkoloni kuwalipa,leo wanapigwa hadi mabomu ya machozi.Anayway nawahurumia usalama wa taifa wanaotetea CCM wakati soon wataikuta imekufa na mwajii mpya atawaambia mahesabu yao yalishalipwa na mfu wa CCM alifia guest house akifanya mapenzi na binti katika ziara iliyolindwa na usalama wa taifa.Na inawezekana mlinzi wa zamu wa siku ya kifo ndiye aliyekosa mafao yake.
 
  • Thanks
Reactions: bdo
Mzalendo JR,
Lengo la biashara siku zote ni faida zaidi na zaidi. Sasa hebu tutafakari. Inakuwaje mfanyabiasha anayetaka faida zaidi na zaidi amwajiri mtu atakayemlipa mshahara wa juu na amkatae yule wa mshahara wa chini? Hapa ndio inabidi tuwe wakweli, perfomance ya watanzania ni ndogo kwenye kazi (wavivu) na mbaya zaidi ni wezi. Huo ndio ukweli. Ndio maana hawa wafanyabiashara wako radhi kulipa mshahara mkubwa kwa wageni.

Nami nafikiria kuwa na marketing wakenya na wahindi, nina experience watanzania wanapenda kudanganywa sana, kujiendekeza sana, na kutafuta sifa ka kutaja kuwa wamenunua kwa watu hao.Watakao implement project ni wazungu na wachina,wabongo watatoa ushirikian 1000+% huku wakijichekesha hovyo.

Hata TRA wakiweka waokota kodi wa nje watapewa kodi sana, imagine mzungu anakwenda mdai dhaifu kodi?sasa akiw amzungu demu aliyepiga Kimini halafu ana confidence kubwa.Usishangae wakilipa mpaka faida juu ya kodi.

Wabongo wajinga sana wanazikataa kazi bora za wabongo kwa hila huku wameshalipa fedha zote ili watoe tender kwa hawa wageni kwa gharama kubwa zaidi.Kila anayeingia antafuta pa kujidai kuwa kaleta kipya kwa gharama mpya.Sikatai kuw akuna vimeo wa kibongo mabo ni wababishaji ktk kufanya kazi waliopata kwa kuzibia wengine.Ila kuna shida pia kwa wanaonunua hizi huduma.Usishangae mbongo akiwa na gadget kibao za electronics.Zote zikiwa versions zilizofuatana na zilizonunuliwa kwa bei ya kuingia sokoni,ila zote mtumiaji hajawahi tumi ahta robo ya tools zilizopo ndani na bado kiu ya kutaka latest haijaisha.Hao ndio kama wazee wa hammer, na wengine wengi ktk serikali ya magamba.SI ajabu wasira ana internet kila computer, nyumbani, ktk simu, ipad, offisini , modem zote, na zote zimewekwa hela ila pengine baada ya kucheki facebook,jamii forum na website za porno kamaliza,hata website ya office yake kiserikali na binfsi hajui hata ni lini zipo offline.
 
bongo bangala
bongo shamba la bibi
acha tujitanue jamani enh?
mbona nyie mko wengi majuu mnaosha vyoo na kukaba watu?
 
Wana JF,

Imefika wakati sisi wenye nchi tuseme ni akina nani, (tuwataje kwa majina pamoja na mambo mengine wanaofanya haya):

-Wanawanyima wazawa ajira na kuwapa wageni (hasa waasia) na wapi walipo. mf. masonara waasia weusi waliofungiwa mtaa wa Indira Ghandhi tujue ni nani (M-tz) kawapa kibali cha kufanya kazi hizo.

-Wachina wanaofanya kazi cha kuchoma magrill badala ya wazawa mf.kampuni ya Hu Tuo iliyoko Msasani. Je, sisi hatuwezi kazi hizo au tumalize madigirii yetu na kwenda kuajiliwa huko kwani nyumba karibia zote zinazojengwa Dar grill zinatengenezwa na wachina. Vile vile frem karibia zote ktkt mwa jiji zinarembeshwa na wachina!!!!!

- Wachina wanaosukuma mikokoteni nani kawaleta humu Tz kufanya hayo? Tunawajua: Jf tuwekeeni nafasi maalumu tuwataje hawa wa-Tz wenzetu wapenda rushwa huku wakituangamiza kwa kuwathamini wageni na kudhalilisha wazawa. Hawa wa-tz wasio na utu wenye kuangalia mifuko yao wakiisahau jamii yao nyuma.

-Waasia waliojificha huko viwandani keko/chang'ombe (nasikia sijawaona).

-Wakenya na waganda eti kwa kuwa wanajua kiingereza kutupita.

-Wachimba madini yetu, mf. nasikia huko Morogoro kuwa wanaojiita wamisionari lakini usiku ni wachimba madini yetu. Tuwataje kwa majina ili kumsaidia rais na kuzilinda mali zetu.

- n.k, n.k, n.k...

Mkuu hapo kwenye RED!
Naendelea kuamini umesahau au umeteleza kidogo. Kuwataja majina huwezi kumsaidia huyu rais wetu na wote tunalijua hili. Kwanini?:

  1. Alisema anawajua wala rushwa kwa majina lakini anawapa muda wajirekebishe, hakuna hatua iliyochukuliwa na wote tunajua rushwa inaendelea kama kawaida.
  2. Akasema apelekewe majina ya wauza unga, na waungwana wakayapeleka akaishia kupiga madongo kwenye sherehe za dini akisema hata nyie viongozi wa dini nanyi niwauza mihadarati.
  3. Akasema ameishapewa majina ya wahujumu uchumi pale TSCAN, mpaka leo ndo hivyo!
  4. Asema jamaa wa KAGODA hawajulikani, watu wakashusha nondo zao lakini wapi?!!!!!!!!!!
  5. Mifano ya kupewa majina ni mingi watu wakiandika hapa kurasa 2 zitajaaa......!
Mkuu ni kwa mantiki hiyo naendelea kuamini kuwataja kwa majina sikweli kuwa utakuwa unamsaidia rais wetu.

Nakumbuka mkuu wa mkoa wa Dar enzi hizo "LUKUVI" alijiapiza kuwashughulikia hao waamiaji uwasemao lakini hatukusikia hata mmoja kaguswa! Kuna siri zaidi ya tujuavyo sie walahoi.

Tafakari.
 
Back
Top Bottom