Elections 2010 Returning officers: Makada wa CCM wanaodumaza demokrasia!

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234

Kufuatia maamuzi ya uonezi dhidi ya uteuzi wa wagombea wa upinzani yaliyofanywa na wasimamizi wa uchaguzi (Returning Officers) katika baadhi ya majimbo kutupiliwa mbali na Tume ya uchaguzi (NEC), jee watatoa maamuzi ya haki wakati wa uchaguzi wenyewe?

Hii ni issue ambayo imezungumzwa sana pamoja na kwamba tunaambiwa hawa maafisa wa umma (wakurugenzi wa wilaya/miji) hawaungi mkono vyama vyovyote vya siasa. Jee hii ni kweli wako neutral 100%

Tumeona jinsi maamuzi yao ya upendeleo yalivyopanguliwa na NEC kuhusu kuenguliwa awali wagombea wa Chadema kule Nyamagana na Singida Mjini. Siamini vile vile iwapo Takukuru inachunguza matukio hayo ambayo bila shaka yana harufu ya rushwa – hasa ukizingatia stature ya wagombea wale wa CCM katika hayo majimbo.

Na hii si mara ya kwanza. Mwaka 2005, returning officer wa jimbo la Tanga mjini, mama mmoja, alionyesha wazi wazi ukada wake kwa CCM baada ya kuonekana kumkampenia mgombea wa chama hicho – Bakari Mwapachu. Alitimuliwa na NEC, na serikali (ofisi ya Waziri Mkuu) ilimteua mwingine.

Swali hapa jee NEC ilishirikishwa katika uteuzi wa huyo returing officer mpya? Au Serikali ya CCM ilimtafuta kada wake mwingine na kumweka pale na kumkumbusha tu asikishabikie chama chake openly.

Mfano mwingine ni jimbo la Bukoba Mjini, mwaka huo huo 2005, pale ambapo returning officer alifanya haraka ya zimamoto kutangaza matokeo bila ya kuwepo mgombea wa CUF Wilfred Lwakatare (wakati ule) pamoja na kwamba Lwakatare alimsihi kwa simu asubiri dakika chache yuko njiani anakuja kwani alikuwa na matokeo tofauti kutokana na hesabu zilizobandikwa ukutani katika vituo.

Lakini hata hivyo, majukumu na mipaka ya utendaji wa hawa returning officers hayajawekwa bayana – inaonekana kama ni siri nzito ambayo daima inakinufaisha chama tawala.

Nasema hivyo kwa sababu sasa hivi inaonekana wao ndiyo wanachunguza na kuamua hapo hapo mambo mengi tu kuhusu taarifa za mgombea – pamoja na uraia yake. Wanayo mamlaka haya?

Tunajua wasioridhishwa wanatakiwa wakate rufaa direct to NEC. Lakini hii pia bado haijakaa sawasawa kwani baada ya uchaguzi matokeo mengi hutangazwa kwa wakati mmoja, hivyo jee NEC wanaweza kumudu influx za rufaa in a short time?

Maana inavyoeleweka, returning officer akisha tangaza mshindi, huwa ndiyo basi tena, labda mshindwa afungue kesi mahakamani.

Napenda kuwasilisha hoja.
 
Umezungumza Mkuu ZM: Umafia wanaofanya hawa pamoja na ule wa ma-DC ndiyo tegemeo kubwa la ushindi wa CCM. Ondoa hao, na CCM itatokomea kunakostahili. Nasikia katika katiba mpya ya Kenya mambo kama hayo ambayo yalikuwapo sana tu katika chaguzi zao yamerekebishwa.

Ukiacha kutolea maamuzi mazito kuhusu uraia wa mgombea, hawa ma-returning officer pia wamekuwa wanaamua wao wenyewe kwamba saini za wadhamini ni feki! wana utaalamu gani wa kuamua hivyo? Kweli ni makada wa CCM hawa......!!!!!
 
Kwa kweli hapa ndipo upinzani unaponyanyaswa. Ndiyo maana tunasikia matokeo yanabadilishwa katika vituo ambavyo wapinzani wana nguvu na kusemekana kuwa walishinda. Lakini yote ni kwa sababu ya njaa ya mawakala wetu pia. Au wasaliti kama huyo aliyejiengua kugombea ubunge Singida baada ya kupewa ama kuahidiwa 60 Mio.

Lakini inafaa mwaka huu kujaribu kila mbinu ya kulinda haki yetu isipokonywe kwa hila.
 
Back
Top Bottom