Red Brigade: Kikundi cha mauaji, watekaji, wamwagia sumu na "nchi kutotawalika"

Status
Not open for further replies.
Mwigulu, Mwigulu…….!



Wenzako kwenye Chama, kila kukicha kazi ni kuzoa matapishi yako. Ukiona tu hali ndani na nje ya Chama imetulia kidogo, unaibuka tena na mambo ajabu na hatari sana kwa ustawi na uhai wa Chama.
Hivi kwanini hautulii? Nini kinakusumbua, kinachokuwasha hadi unacha kufanya kazi ya u-“Naibu Katibu, Bara” (kwa maana ya utawala hapo Lumumba, pale White House na nchini kote ofisi za Chama, mikoa na wilaya? Hapo hapo, kwa pumzi hiyo hiyo, wewe unajifanya kinara au kiranja mkuu wa kuwatuhumu wengine kujitafutia umaarufu.
Mwigulu, elewa fika, wewe utukuwa “mtajwa” wa kwanza kabisa orodha ya waliochangia kadri ya nguvu na uwezo wao wote kukiua Chama!



Mchango wako Red Brigades una dosari kubwa, kubwa mno!


Unawaficha wananchi “fact” muhimu kabisa na ya kihostoria kwamba vikosi vyote ulivyovitaja hapo juu, msingi wao kwa maana ya ideology, ni fikra za kisoshialisti, ujamaa. Je huu kweli ni msingi wa wenzetu wa Chadema? Umefanya utafiti upi hadi kuwataja MSI, watu waliopinda kabisa kufikia hatua ya kuwadanganya, haswa wazee wa Italia, eti MSI kirefu chake ni Madonna Sanctissima Immaculata. We si mkristo? Hivi unahitaji translation yake Madonna Sanctissima Immaculata, au Dr. Slaa, aliyekuwa Padri Katholiki, akueleze?



Umesahau vipi “Baader Meinhoff” ya Ujerumani (Slaa si karejea toka huko hivi majuzi?), kikundi dada na mshiriki mkuu wa Red Brigade kifikra na kimatendo?



Mwigulu, kazi yako ni administration, sio “uenezi”, hata kama ulizoea enzi yako ya u-“NT” kutofanya kazi uliopewa na baadala yake kufanya kazi ya mwingine, bado hii kazi yake si yako ni ya Nape! Kama lazima kufanya kazi ya majukwaani, we concentrate tu kuwaeleza wananchi success story ya Chama. Si ipo? Tena ndefu sana?



Kwanini kila neno la pili toka mdomoni mwako ni Chadema? Hauoni jinsi unavyozidi kuwapaisha kila kukicha? Hata kwa akili tu ya kawaida na si lazima kama ile ya “mchumi daraja 1”, wote tunaona jinsi unvavyowafurahisha hawa wa Chadema. Maumivu haya madogo madogo kama vile kamata kamata na kesi za ajabu ajabu, zote ambazo zazidi kuwajenga, wanavumilia kwa kicheko maana hata wao wenyewe wasingeweza kubuni mikakati kali kama hiyo kujipaisha machoni mwa wananchi. Kujipatia huruma ya wananchi, kwa jinsi watawala “wanavyowaonea” na “kuwatesa”, wanavyotumia vyombo vya dola, n.k. sina haja kuendelea na mifano.



Tatizo lako, unatumia rationale ya mchumi daraja 1 (ingawa hakuna hata moja Benki Kuu anakumbuka kutoa chozi ulipoomba kwenda masomoni; actually ilikuwa sawa na “good riddance” na ombi lako likashughulikiwa haraka haraka, ili mradi tu…) na siyo ile inayohitajika haswa wakatu huu mgumu kwa Chama na Taifa.

Busara na uelewa ndio priority namba 1. Kama mchumi umesoma pia statistics, takwimu na jinsi ya kuzipembua. Laiti ungefanya hivyo, ungeelewa kuwa vijana kuanzia Form III leo ni wapiga kura 2015. Hata wengi tu wa Form II. Je, mpo pamoja, mpo na walimu wao? Threads kama hii ya yako, inakujenga machoni mwao?


Red Brigrade na hao wengine unaowataja kama nduguze Chadema ni ya miaka ya mid-1970’s (!!!!!), leo hii nadhani ni mwaka 2013. HUU NI USHAHIDI WAKO HATA MBINGUNI? Tofauti ya miaka hii 40 umetoa au kupeleka wapi? Au ndizo hesabu za kichumi? Kama ndivyo hesabu zinapigwa, sishangai kuona umasikini unaendelea miaka 50 baada ya kupata Uhuru.



Eleza “mazuri” ya chama chako, aachana na “mabaya” ya wenzako. Chama chako kimeshike dola, unaogopa nini kama wewe msafi, wenzako wachafu? Aachana na “copy and paste” toka google, wikipedia, n.k. Haikuongezei heshima, hata kidogo!, Inakichafua Chama.
Baati nzuri nimeokoka, ningemtukana vibaya sana.
 
Huyu si ndio yule aliyefukuzwa CDM, umaarufu wote kwisha habari.
Umaarufu ataupatia wapi kutwa nzima anashinda akiosha vyombo,kupika,kulea watoto baba wa kukisia,kutumwa soseji na maandazi Lumumba.
 
Tunashukuru kwa taarifa duu!! Chadema kumbe ni hatari kiasi hiki.

Duh msukule mwingine unaoishi kwa damu za watanzania.Kama kuita jina tu RED BRIGADE imekuwa sawa kimalengo na ilokuwa RED BRIGADE YA ITALIA JE KWA NINI KISIWA CHA MAFIA KISIBADILISHWE JINA ILI KIWE TOFAUTI NA JINA YA LILE KUNDI LA KIGAIDI LA MAFIA ENZI ZILE?Shame on you SISIEMU NA VIBARAKA WENU MANOISHI KWA KUTEGEMEA DAMU.Mwenye hoja amjibu Dr Slaa kenye andiko lake na Bethlehemu sio mnajinyeanyea tu huku mkionesha udhaifu ktk kujadili na kuchangia hoja
 
IFAHAMU RED BRIGADE YA CHADEMA,ILIPOANZIA,ALIYEILETA CHADEMA,MAFUNZO YA VIJANA WA CHADEMA NA KUBADIRIKA KWA BENDERA YA CHADEMA.

300px-Flag_of_the_Brigate_Rosse.svg.png


Watanzania wenzangu,

Ni dhahiri kumekuwa na mijadala kadha wa kadha kuhusu vyama vya siasa kuwa na vijana wao wa kuwa linda. Nilionesha tofauti baina ya red brigade na greenguard. Wanaojitetea wakakimbilia Dictionary bila kutumia muda kufuatilia historia na chimbuko la kikundi hicho ambacho jina , matendo na malengo yake yako sawasawa na kule kilikoanzia.

Lakini mjadala mkubwa ni kuhusu mpango wa CHADEMA kuanzisha jeshi lao la chama chao, Jeshi ambalo halihitaji msaada wa polisi wala wa Jeshi la wananchi wa Tanzania kwa mjibu wa kauli ya mkt wao mhe Mbowe.

Ni kinyume na katiba ya nchi na hata katiba ya chama chao (pitia katiba yao). Wanavunja katiba hiyo sio kwa bahati mbaya bali ni mpango wao unawabana wa kuhakikisha amani ya nchi inatoweka kama ambavyo .,Jeshi wanalotaka kulianzisha si bahati mbaya,ni mpango wa siku nyingi hasa ukifuatilia walikojifunzia ideology ya Red Brigade na aliyeileta CHADEMA.

images


MAANA HALISI YA RED BRIGADE NA WAANZILISHI WA HIYO TAASISI.

Red Brigade ilianzia ITALIA mwaka 1970 kwa kifupi ni BR,Wanzilishi wake anafahamika kwa jina la Renato Curcio na Margherita(mara) Cagol waliokutana kama wakiwa wanafunzi chuo kikuu cha Trento karibu na chuo alichokuwa akisoma Dr Slaa.

Red Brigade ni kikundi kilichokuwa kinajishughulisha na kuishambulia(kudhoofisha) serikali kwa kufanya mambo mbalimbali ya Mauaji,Kuteka na Kuua wanasiasa, Kuhujumu kazi za serikali, Kuiba mali za watu, Kupandikiza chuki kati ya wananchi na serikali yao na wananchi na vyombo vya dola na Kufanya nchi isitawalike (Rejea kauli ya Dr.slaa "NCHI HAITATAWALIKA"
Kikundi hiki kilikuwa kinatumia mwamvuli wa kuwa na uchungu na mali za umma lakini badala yake kikatumika , kuteka, kua na kumwagia sumu watu.

NOTE: Nazism ya Ujerumani chini ya Hitler ilijipambanua kama Socialist party(lakini matendo yake yalikuwa ni tofauti kabisa,Ugaidi na kuua ndio sifa yao).

Hiki kikundi kilivuma sana miaka ya 1970 hadi miaka ya 1980 (Hiki kipindi Dr.Slaa alikuwa Italia kwenye masomo na maisha yake yalikuwa huko). Red Brigade wakati huo walikuwa na kazi kubwa ya kuidhoofisha serikali iliyopo madarakani chini ya waziri mkuu Aldo Moro wakati huo.

Mwaka 1978 kilianzishwa kikundi kikubwa zaidi ndani ya RED BRIGADE(Ndio hicho chadema wanataka kukianzisha).Baada ya kuanzishwa kwa kikundi hicho kikiwa na watu 1000,kikundi hiki kilifanikiwa kumteka waziri mkuu Aldo Moro na kumuua Kinyama

Kuanzia mwaka 1974 hadi 1988 kikundi hiki kilifanya matukio ya kuteka, kuua,kumwagia sumu watu kwa matukio zaidi ya 50.Na yote haya yalilenga kufanya serikali ya Italy Isitawalike (DESTABALISE)..


images


KUKUA NA KUVUMA KWA RED BRIDGADE.

Matukio ya kuua na kuteka,kumwagia sumu na kuleta vurugu kila kona ya Itali kiliwafanya Red Brigade kusikika sana nakuleta hofu kwa watu.

Walikuwa wanaua na kuteka kwa USIRI mkubwa tena wakiwa wanatembea chini ya mwavuli wa chama cha kisiasa LOTTA CONTINUA na Potere Operaio.

Pia kilivuma sana kupitia Movement for Change MFC waliyoianzisha na baadaye kuipa jina la MOVIMENTO SOCIALE ITALIANO(MSI) bila shaka ndio M4C ya CHADEMA.

Ilikuwa ni miaka ya 1980 ambapo hiki kikundi kilizimwa kabisa kabisa na serikali.Serikali iliamua kuchukua hatua nzito kwa kuanzisha slogan ya ANTI-BR.

Yapo mengi sana ya kuelezea kuhusunia na kikundi hiki,(Pitia link hapa chini).

images


VIONGOZI WA RED BRIGADE WAKIMBIA ITALI.

Baada ya kusambaratisha Italia,RED BRIGADES wakakimbilia nchi zingine,Mfano Antonio Negri na Cesare baltisti walikimbilia France.

Wengine walikimbilia Palestina.

Takwimu zinaonesha zaidi ya watu 780 waliuawa na kumwagiwa sumu Italia chini ya BR,Lakini pia walifanya matukio zaidi ya 1400 ya uvunjifu wa amani na kuifanya Italia isitawalike.
Tafiti zinaonesha Red Brigade inaendelea kuishi kwenye nchi mbalimbali kupitia vyama vya siasa,Na moja wapo ni India,Tanzania(CHADEMA) Amerika kusini n.k

Pitia Link hii>>https://en.wikipedia.org/wiki/Red_Brigades na hii https://en.wikipedia.org/wiki/Red_Brigades.

ALIYEILETA CHADEMA KIKUNDI CHA RED BRIGADE NA MABADIRIKO YA BENDERA YA CHAMA.

images


Wakati wote haya ya RED BRIGADE yakiendela huko Italia,Kulikuwa na Mtanzania mwenzetu akiishi na kusoma huko (mambo ya kanisa),Ni katibu mkuu wa sasa wa CHADEMA Dr.slaa, Huyu ndiye aliyeleta falsafa ya kuanzishwa kwa kikundi hicho cha kihalifu chini ya mwavuli wa chama.

Historia inatuambia
Mwaka 1977 Dr Slaa alifanikiwa kupata upadirisho, Aliamua kujiendeleza kimasomo kwa kujiunga katika chuo kikuu cha Ponfical Urban Cha Roma cha huko Italia karibu na chuo walipokuwa wakisoma waanzilishi wa Red Brigade kipindi hicho Italy .

Alipokuwa Italia masomoni ndipo alipojifunza mbinu hizi za RED BRIGADE na hatimaye kuzileta CHADEMA.

Baada ya Dr.slaa kujiunga CHADEMA akaongoza ubadilishaji wa bendera ya chama (Bendera ya CHADEMA imebadilishwa na kuwekwa rangi nyekundu kama mwagaji damu Italy na aliyeasisi mabadiriko haya ni Dr.slaa akichukua sehemu ya bendera ya Red Bridgade wa Italy)na uundwaji wa katiba mpya ya chama yenye Red Bridgade(jina hili alilitoa Dr.slaa kwa kuiga lile la kikundi cha Italy) ndani.

Dr. Slaa alipojiunga CHADEMA amekuwa mstari ma mbele kutengeneza mahusiano na Italia ya kisiasa.

Kwa mara ya kwanza CHADEMA walipeleka vijana zaidi ya 50 kwenda masomoni Italia kujifunza mambo ya Red Bridgade kwa mwavuli wa mafunzo ya siasa na utawala.

lwakatare-case-april16-2013(1).jpg



RED BRIDGADE YA ITALIA(CHADEMA) NA KINACHOTOKEA NDANI YA NCHI YETU.

hqdefault.jpg


Ni wazi kabisa kabisa,Nchi yetu imekuwa ikikumbwa na mikasa ya uvunjifu wa Amani, kutekwa kwa watanzania wenzetu,Kuuawa kwa wananchi, Kutekwa na kuuawa kwa wanasiasa wenzetu kama ndago na mipango ya kuteka wandishi. Kubwa zaidi tumeshuhudiwa Kiongozi mkubwa wa chadema akisimama jukwaani na kujinasibu "NCHI HAITATAWALIKA"(DESTABALISE). Na kuwambia maaskofu wasiombee Amani

images


Ni ushuhuda ambao kila mtanzania anaweza kuusema, Mikutano inayoua ni ya chadema, Wanaoteka na kumwagia tindikali (sumu) ni vijana wa CHADEMA,Wanaojiita RED BRIDGADE ni CHADEMA,wanaoteka watu hao hao wanahusishwa ni CHADEMA, Chama maarufu kwa maandamano Afrika Mashariki na kati ni CHADEMA,Uvunjifu wa amani na matukio ya kigaidi yanatokea kwneye mkitano ya CHADEMA

Na hayo yote ni yale yale waliyokuwa wanayafanya RED BRIGADE wa Italia kuhakikisha serikali na chi haitawaliki.

images


Slogan ya MOVEMENT for Change na Peoples Power ni mwavuli tu ambao ulichukuliwa toka Magharibi kuwa ni wanademokrasia,Ili hali ni wanademogasia

313701_250604634977789_100000847625338_687930_911968435_n-560x373.jpg


Kwahiyo niseme wazi,mpango huu wanaotaka kuufanya chadema wa kuunda RB kubwa zaidi tena isiyohitaji msaada wa jeshi la polisi na Jeshi la Wa Tanzania, ni uhaini, ni ugaidi,ni maandalizi ya kupindua nchi au kuvuruga kabisa kabisa amani tuliyonayo. Kama wanavuruga amani na hii Redbrigade ndogo,itakuwaje wakiwa na jeshi.

lema_mjeshi1.jpg


Naunga mkono kauli ya Rais Mh.Jakaya kikwete hakuna kuundwa kwa jeshi hilo,na serikali itachukua hatua stahiki kuhakikisha nchi inafuata misingi ya katiba yake.

Hivyo basi,nawaomba watanzania tuamke, tusome nyakati kuhusiana na upinzani huu wa CHADEMA wenye mwavuli wa kisiasa kumbe ni kundi la RedBrigade wa Italy ni hatari kwa nchi yetu.

"KWA HABARI ZAIDI INGIA GOOGLE SEARCH RED BRIGADE"

====Majibu ya Dr. Slaa====




Yaani napata tumaini kuwa UPINZANI Tanzania una nguvu isiyokuwa ya kawaida!!! Mpaka naibu katibu mkuu wa chama kikongwe Africa (lakini kilichochoka) anavua dignity na respect na kuanza kulalamika kwenye mitandao kwa chama cha upinzani!!

Hongera CHADEMA, you have completely changed the political sphere of Tanzania. Sasa tunaichukua nchi yetu kiulaini!!! Wameanza kujifunza kuwa wapinzani. Thank you God, now we are going to possess our land, hatukudhani wala kuwaza kuwa itafika siku CCM watalalamika na kutoa machozi mtandaoni.
 
... Mwigulu Nchemba ingetokea umekuwa kiongozi wangu ningejiuzuru,na kama ningekuwa kiongozi wako ningekufukuza hata kwa zengwe, nisinge weza kuvumilia fedhea kama hizi kwa mtu kama wewe...
 
Last edited by a moderator:
Join Date : 6th May 2006
Location : Online
Posts : 2,019
Rep Power : 1078
Likes Received183
Likes Given
0


Kwenye red: Wewe jamaa ndio Idd Amini, miaka yote hiyo JF hata kutoa LIKE kwa wenzako hutaki?

POOR COMMENT.kuna formula ya kutoa likes kama hajaona cha kutoa au unataka aje na propaganda za nyie wanywa damu ZA NDIYOOO ASILIMIA 100 lakini unatoa hoja na maswali kwa ulichokubali na kukipitisha????Ndo akili zenu maga,mba
 
Wadau mlioko kwenye Huu uzi; Hebu nisaidieni. Yuko wapi mleta mada?Wakuu wasiwasi wangu ni mmoja.Nilisema sijadiliani tene na mwigulu lakini nimepata wazo ambalo nimeona nibora nikawastua.Nahisi lengo la jamaa kuleta huu uzi hapa ni ili tuendelee kujadili, halafu wakati huo yeye anaenda kupaki mzigo wa mali iliyobakia (kutoka china)kisha anaelekea Arusha! Uchaguzi si Jpili wakuu? Hebu ngoja!
 
Sisi watanzania tutaendelea kulala hivi hadi lini jamani??!! tuamke sasa. Tuna jeshi la polisi, jeshi la wananchi (JWTZ) Usalama wa Taifa, Serikali tulioipa madaraka kupitiliza, na vyombo vingine vyote vya usalama ambao watu wote hawa tunawalipa kwa kodi zetu tena zinazokamuliwa toka kwa watanzania masikini!!!!!!

Sasa vyombo vyote hivi vimeshindwa kufanya kazi zake huyu mpuuzi alienda shule bila kuelimika (Mwigulu Nchemba) kuja kutuandikia upuuzi wake hapa na kutupotezea muda wetu wa kufanya kazi na kulikomboa taifa letu lililogubikwa na umasikini wa kutupwa uliasisiwa na kuendelea kulindwa na Mwigulu na CCM yake tangu miaka na miaka???!!!

Kama serikali inajua mambo yote haya ilikuwa inasubiri nini kuchukua hatua muafaka wa kukiwajibisha kikundi hiki anachodai huyu mwehu??!!!

Au Mwigulu na CCM yake wanajua kwamba watanzania wa leo ni wapuuzi kama wao na kutumia mbinu zao chafu za vitisho na mauwaji wanayoendelea kuyaratibu kote nchini dhidi ya upinzani especially CHADEMA ili CCM iendelee kuinyonya Tanzania na wananchi wake kama walivyozoea

Mwigulu nakushauri tafuta namna nyingine ya kutudanganya watanzania kwani hii unayoitumia imepitwa na wakati na watu tumeshaigundua kwamba ilitumika mwaka 1995 ikafanikiwa ila this time tayari imeshaonyesha kushindwa maana watanzania wa leo sio wa miaka hiyo unavyofikiria
 
Mwigulu ni mtu wa kupuunzwa....siasa zake maji taka zilizo jaa chuki zita lifikisha taaifa pabaya
 
Sidhani kama chadema walikua wanajua maana ya hili jina vizuri..Hongera Mwigulu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom