Red Brigade: Kikundi cha mauaji, watekaji, wamwagia sumu na "nchi kutotawalika"

Status
Not open for further replies.
944201_478412182248001_1271837198_n.jpg
 
mkuu chadema ni chama cha ajabu sana hawajui kitu kinachoitwa sheria wala utaratibu.

sijawahi kuona chama ambacho kinaongozwa kihuni kama hiki cha chadem wewe ulishaona wapi ukiona mtu anampinga mwenyekiti anauawa huu siyo utaratibu hata kidogo.
Basi serikali yetu, na Msajili wetu wa vyama vya siasa ndiye wa ajabu zaidi kuvumilia uwepo wa chama kama hicho kwa kuwa sheria zetu haziruhusu vyama vya kihuni.

Kama anashindwa kuchukua hatua dhidi ya chadema, basi hii inadhihirisha ama hayo yanayosemwa ni uongo na propaganda, au serikali ni DHAIFU!

Kati ya hayo mawili ni lipi?
 
Kaka tukubali tu kwa kweli CHADEMA inakutesa sana angalia usipate PRESSURE!!!!

Huyu Nchemba hateswi tena na CDM bali damu za watu alioshiriki kuua ndizo zinamtesa, siku mbili hizi ndio kawa kama kichaa fulani vile na nakwambia anavyofanya mambo yake kitoto hatachelewa kunaswa na CDM ndani ya 18 akitekeleza ushenzi wake na hapo ndio mtaona jinsi CCM inavyojua kuwaruka watu wake

CCM SIO MWIGULU NCHEMBA, CCM SIO WAUAJI, WAUAJI HAWAZIDI KUMI NDANI YA CCM, KUUA NI MURDER CASE, KUNA SIKU HAWA WAUAJI WATATAFUTWA KAMA VILE ALEX MASSAWE ALIVYOTAFUTWA NA KUPATIKANA DUBAI
NI LAZIMA SIKU MOJA NCHEMBA ATAJIBU MAHAKAMANI KWANI HISTORIA NDIVYO ILIVYO
 
IFAHAMU RED BRIGADE YA CHADEMA,ILIPOANZIA,ALIYEILETA CHADEMA,MAFUNZO YA VIJANA WA CHADEMA NA KUBADIRIKA KWA BENDERA YA CHADEMA.


Ni dhahiri kumekuwa na mijadala kadha wa kadha kuhusu vyama vya siasa kuwa na vijana wao wa kuwa linda. Nilionesha tofauti baina ya red brigade na greenguard. Wanaojitetea wakakimbilia Dictionary bila kutumia muda kufuatilia historia na chimbuko la kikundi hicho ambacho jina , matendo na malengo yake yako sawasawa na kule kilikoanzia.

Lakini mjadala mkubwa ni kuhusu mpango wa CHADEMA kuanzisha jeshi lao la chama chao, Jeshi ambalo halihitaji msaada wa polisi wala wa Jeshi la wananchi wa Tanzania kwa mjibu wa kauli ya mkt wao mhe Mbowe.

Hivi jamani nyie CCM uongo mutaacha lini? hivi kweli mtu mzima katibu mkuu mzima unawadanga na kupotosha uma wa watanzania, hivi ni kweli mbowe alisema chadema wanataka kuanzisha jeshi? au alisema wanataka wawape mafunzo ya ukakamavu kwa Red brigade? Mbona munazusha vitu ambavyo havipo kabisa au ni ndio munazihirisha jinsi ambavyo musivyo ishiwa na maneno ya uongo na kuzusha?

Nani asiyejua kama CCM wana Green guard? vipi hilo ni jeshi? au kikundi cha ulinzi? watanzania tusaidiane kwa hili mifano tunayo hawa vijana wa green guard ni jeshi? kama siyo jeshi mbona walikuwa makambini wakifanya mafunzo na hata kupatiwa silaha? kwa nini na sisi CHADEMA tusiwape mafunzo Red brigade?

4.-paredi-la-vijana-wa-ccm.jpg 21385_700883443260987_2063181291_n.jpg View attachment 101966

Kwa CCM inakuwa vijana wa ulinzi ila kwa CHADEMA inakuwa jeshi. vipi mbona waoga wa changamoto?

Mimi naona CCM hampaswi kuwa waoga kiasi cha kupotosha umma kana kwamba haya mambo chadema ndio wa kwanza kuyafanya hapa Tanzania na huku nyinyi munavijana na makambo tena yenu munayafanya kwa siri kubwa
 
Kwa umri nilionao ccm ilikuwa na viongozi wenyeheshima walipoifikisha chi palikubalika, tatizo huyu nchemba tangu amepewa nafasi hii, hali ya usalama imebadilika. Kama ccm wana akili huyu jini inabidi wamtoe vinginevyo anakoelekea ni kuzimu. na namhakikishia hata akiwa na akina policcm watanzania hamtuwezi. Uongozi sio vitisho kihivo, yawezekana ndo maana unafanya kazi ambayo hukusomea yawekana ulikuwa unawaboa wafanyakazi wenzako ndo ukahamia huku ili hatimaye u-perish shit!
 
mkuu chadema ni chama cha ajabu sana hawajui kitu kinachoitwa sheria wala utaratibu.

sijawahi kuona chama ambacho kinaongozwa kihuni kama hiki cha chadem wewe ulishaona wapi ukiona mtu anampinga mwenyekiti anauawa huu siyo utaratibu hata kidogo.

Kama wewe una ushahidi kama huo kwanini hujaupeleka kwa IGP ili wakamatwe hawa chadema?Wewe nawe una tatizo kwenye ubongo wako.Wewe ni mhalifu namba 2 baada ya Mwigulu.
 
Jamani sisi wananchi wa kanda ya ziwa, tunauliza wapi tunajiunga Red Brgd?. Hata km tunajiunga kwa ada semeni mapema tuanze kudunduliza!.
 
@Dr.W.Slaa

Tumewastukia, siasa zenu za umwagaji damu. Si wapiganaji nyinyi? Red Brigade, Mwigulu kaichambuwa vema sana na hata uipenge vipi, watu siku hizi wanaingia kwenye mtandao wanachota habari, huwezi kuwadanganya.

Babu, hii nchi utaisikia redioni tu, hatukupi ng'oo. Kwanza maadili yako yana mashaka makubwa sana.
 
kwa kweli wewe mwigulu nchemba ; nashindwa kujua uwezo wako wa kufikiri. Jana ulileta uzi wenye maudhui haya haya na picha hizi hizi; tulipoanza kukuuliza maswali ukakimbia kivuli chako. Sasa leo unadhani tushasahau, umeleta uzi kama ule ule ulichoongeza ni idadi ya picha na maelezo ya wikipedia. Maskini mwenzetu hujui hata kuwa wikipendia ni kama jf, ambapo yeyote aweza kuandika chochote.hata hivyo unachofanya ni upotoshaji wa makusudi na kuanzia leo mimi natangaza kutochangia thread zako tena mpaka hapo utakapoamua kuwa muungwana na ukaacha kufanya upotoshaji wa makusudi hali unajua.



  • ndugu zangu watanzania; kama red brigade ni kundi la kihalifu tena linalotumia silaha za moto na ndilo linaloendesha mauaji nchini, na lipo toka dr.w.slaa ,alivyojiunga na na chadema na mauaji na utesejaji ndio kazi yake (kama anavyodai huyu kiongozi mwandamizi wa ccm), ni kwa nini kundi hili limeachwa likaendelea kuwepo nchini mpaka sasa licha ya kuwa limekuwa likifahamika kwa muda wote huo na muasisi wake amekuwa akifahamika fika kuwa ni dr.w.slaa? Kama hili ndilo kundi linalotekeleza mauaji ya kisiasa nchini (kwa mujibu wa kauli ya mwigulu;kiongozi wa chama kinachoongoza serikali) je! Kamanda chagonja na wenzake wako arusha kuwasanifu watanzania?

  • ikitokea mwanafamilia anavamia wanafamilia wenzake, na kuwashambulia; ni nani (chombo gani) anaepaswa kumkamata? .jaalia chadema wamekuwa na tabia ya kujishambulia wenyewe (kama mnavyodai) na kule arusha wamejishambulia wenyewe pia,(mwana familia kaamua kuwashambulia wanafamilia wenzake kwa sababu yeyote ile) ni nani alipaswa kumdhibiti? Je! Aliepaswa kumdhibiti na hakumdhibiti ninyi mnamtafsiri je? Je; mnadhani wanachadema walioshambuliwa (hata kama wameshambuliwa na mwanachedema mwenzao) hawapaswi kuchukua hatua?

kama ni ninyi kwa mfano; kuna mtu anawavamieni ndani kwenu, anawashambulia na kuwaibia; na chombo kinachotakiwa kumdhibiti hakifanyi hivyo (kwa sababu zozote zile), mkikiuliza kinasema anayewavamia huwa ni mwanafamilia mwenzenu, ninyi mngechukua hatua gani? Mfano kama mkisema mtakuwa mnajificha nyuma ya mlango halafu mvamizi akifungua mlango tu mnamkamata; halafu ikatokea chombo ambacho ndicho kilitakiwa kiwe kinamkamata (japo hakifanyi hivyo) kinaibuka na kusema "ole wenu muwe mnamvizia muhalifu nyuma ya mlango", (huku kikisisitiza kuwa kitahakikisha kinawadhibiti kama mtachukua hatua ya kudhibiti uhalifu mnaofanyiwa), nyinyi mtakitafsiri vipi chombo hiki ? Je; mnadhani wanaofanyiwa hivyo sasa nao wakijiwa na fikra/tafsiri inayokuja kichwani kwako sasa; watatakiwa kulaumiwa?
wenzetu wa ccm mnajisikia je?

1. Mnajisikiaje ikiwa mnashambuliwa (bila kujali mshambuliaji ni nani) kisha mshambuliaji hakamatwi halafu ukitaka kujilinda, alietakiwa kumkamata mhalifu (aliyeshambulia) anakukabili kwa nguvu zote?

2. Unajisikiaje siku umevamiwa ndani ya familia yako, ukashambuliwa, (mtoto wako mdogo akafariki kwa kupigwa) halafu ukaripoti kwa vyombo husika vikakuambia utakuwa umejishambulia mwenyewe ili upate misaada na huruma?utajisikia je?

3.utajisikia je siku ukiwa unaumwa pengine na malaria (si unajua wanadamu tumeumbwa kwa nyama) halafu umelazwa muhimbili, ghafla unasikia sauti ikikupa pole na kisha unafungua macho; mbele yako unamuona mtu asiye na meno ya mbele,anatembea anachehemea huku ana makovu mengi usoni.mkononi kabeba sabuni na chupa ya uji. Kwa mbali unakumbuka ni miongoni mwa watu ambao wewe uliwatuma askari wampige na kumsababishia hali hiyo (eti tu kwa kuwa alikuwa na mawazo tofauti na yako) unajisikia je? Hivi unajisikiaje?


4. Unajisikiaje unapotembea njiani, halafu ukakutana na watu; watu wanaojua kwamba kuna uhalifu unatokea hata kusababisha mauaji na wewe wakati wote hoja zako ambazo umekuwa ukizitoa zinakuwa za kuukadhamiza upande wa wahanga na kuwatetea upande wa wahalifu; hivi unajisikia je? Unadhani wanaokuona na kukutizama nao wanajisikia je?

5. Unaonaje ukijikuta katia mazingira ambayo kuna watu watatu. Mmoja anahisi anaweza kudhuriwa (kwa kuwa alishawahi kudhuriwa mara kadhaa) na hivyo anafikiri kujilinda (defensive) na wa pili anataka kudhuru (offensive) hivyo hataki wa kwanza ajilinde (ili asije akapata upinzani), na huyu wa tatu yeye anapingana na wa kwanza na hivyo kuungana na huyu wa pili. Wewe utajisikia je? Na utachukua upande gani hata kimoyo moyo tu?


Mambo haya kimsingi yanahitaji diplomasia kubwa sasa ya kisiasa kwa sasa (vinginevyo ni hatari sana) na hilo linawezekana tu, ikiwa kutakuwa na nia njema hasa kutoka kwa upande unaowatenda wenzao.hata hivyo kwa haya wanayoendelea kuyazusha viongozi wa ccm, kwenye vyombo vya habari badala ya kushughulikia tatizo la msingi, sioni kama wana nia njema katika hili.ndugu zangu; tunajenga vizazi vyenye mafundo ya chuki, hasira na roho za visasi; hivi nani anajua vizuri saikolojia ya mtu anaedhani anadhulumiwa, anaonewa anakandamizwa na akijaribu kujitetea anazimwa kwa nguvu?

Hivi ninyi wenzetu wa ccm, kwa nini mnawafanyia wenzenu na mnapenda wenzenu wafanyiwe vile msivyovipenda kufanyiwa ninyi? Kwa nini mnapenda kuwa na vitu ambavyo hampendi wenzenu wawe navyo? Kwa nini mnapenda wenzenu wafanye vitu ambavyo ninyi hamfanyi na msingependa kufanya? Wakati fulani mnawasababisha watu wapate jazba na mimi naona jazba ishaanza kunivizia.ngoja ni ache.....

Wenzetu wa ccm, kwa nini mnazusha mambo ambayo mnajua wazi kuwa ni uongo, uzushi na uchochezi na kuacha kushughulikia tatizo la msingi, huku wenzenu wamewapoteza wapendwa wao? Hakika huku ni kupoteza ubinadamu kwa ulafi wa madaraka.

Kilichobaki kwenu ni mungu kuwatamkia kauli moja tuu...

"mene mene tekeri na perese!" maana yake; utawala wenu umepimwa na umeonakana na mapumgufu makubwa! Na kisha ukachunguzwa ukakutwa umepungua na tena umegawanjika!. Na sasa watapewa watu wengine na mtaishia kudhalilika! .


nimesoma nashangaa ila nikumbushe tena mara hii nitatoa mfano utasaidia kuelewa kwamba kama ilivyo dunia angani na mungu hakuwahi kuiachia pamoja na uzito wake binadamu tukiwa humo.mungu ndiye anayeitunza amani na kulinda watu wake maana unyama unaofanyika unaamusha hasira ya mungu
 
Last edited by a moderator:
watanzania tunajitambua mwigulu tuondolee upuuzi wako hapa unafiriki tutakuamini wewe mnafiki mkubwa
 
wanaJF,
Jitihada za Mwigulu kuhusianisha Red Brigade ya CHADEMA na Brigate Rosse ( neno la ki Italiano. Lenye maana ya Red Bigades) ni propaganda ya Kipuuzi. Red Brigade ( inaitwa brigedi Nyenyekundu) ya CHADEMA, ambayo ipo kwa mujibu wa Katiba ya Chadema na Kanuni zetu. Fasili na Ufafanuzi wa Brigedi Nyekundu ni "..Chombo cha ulinzi na usalama wa mali na maslahi ya Chama na viongozi"( Rejea Kanuni za Uendeshaji Kazi za Chama... kif. B " Fasili na Ufafanuzi". Wajibu wa kujilinda ni wa kila mtu na chama nacho kina wajibu wa kulinda Mali zake, wanachama wake na viongozi wake.

Aidha Mwigulu anazungumzia "Brigate Rosse". Ni dhahiri Mwigulu anafanya siasa ya maji Taka. Kwanza ni vema Mwigulu wajulishe wasomaji Kama neno hilo Lina maana ile ile ya "Red Brigade", na je Red Brigade ya CHADEMA in a fasili na Tafsiri ile ile ya CHADEMA? Kama ndivyo atuwekee Katiba ya Brigate Rosse hadharani ili wanaJF na GT wote wafanye uchambuzi wa kina na kuona Kama anachosema Mwigulu ni sahihi au ni Propaganda tu!

Ni kweli Dr. Slaa nimesoma Roma Italia toka 1979 hadi 1981. Hivyo siyo tu ninajua na kuzungumza Kiitalia, lakini pia ninafahamu Brigate Rosse ya Italia kwa kuwa miaka hiyo ndio kipindi kulikuwa na umafia na uhalifu mkubwa na kulikuwa na kesi denying dhidi ya Mafia. Katika Masomo yangu ya Sheria,kesi hizo Mara nyingi zimekuwa rejea ya Maprofesa. Hivyo ninaijua si kwa kuwa nimeishi katika utamaduni wa Italia wa wakati huo.

Hata hivyo, Ndio maana sikuzote, Sina sababu ya kujibu upuuzi wa Mwigulu. serikali iliyoko madarakani ni ya CCM. Kama ni kweli anayosema Mwigulu na anayaamini, Anashangaza sana. Dr. slas nimemaliza masomo yangu mwaka 1981. Tangu wakati huo sijarudi Roma isipokuwa kipindi nilipokuwa Katibu Mkuu wa TEC. Sasa Mwigulu anataka kusema TEC nayo ilikuwa inanzisha Brigate Rosse kwa kuwa Kama Katibu wajibu wangu ulikuwa kuunganisha Baraza letu na Nchi zingine duniani.kauli ya Mwigulu,unaweza kutolewa tu na mtoto wa darasa la pili.

Aidha, Kama Anachosema Mwigulu ni kweli anapaswa kukamatwa,kwani Kama Raia Mwema, toka mwaka 1981 Mwigulu alikuwa na Taarifa ya mtu aliyejifunza mbinu za Brigate Rosse, ambazo ni makundi ya uhalifu na Umafia na Mwigulu amekaa na Taarifa hizo za kihalifu na kwa kuwa kwa mujibu wa sheria za nchi yetu, mwenye kukaa na Taarifu za uhalifu na yeye ni mhalifu. Anapaswa akamatwe kwa ushiriki wake kwenye uhalifu huo. Katika Hali ya kawaida sina hakika Kama Mwigulu aliwahi kujifunza kitu kinachoitwa logic katika maisha yake. Kuelewa kuwa Kaulinzako zinajikanyaga huhitaji sana kwenda shule kubwa kubwa, unless mnatuambia Chuo Kikuu kilichompa Degree ni hovyo kiasi hicho. Kwa maana nyingine, Kama kweli Mwigulu ni Naibu Katibu Mkuu, Serikali aliyoko ni hiyo hiyo ya CCM toka miaka 1977, maana yake ni kuwa Serikali hiyo ambayo inamjua mhalifu muda wote tcoka 1981, inaibuka Leo na kauli tata hivi, wakati Katiba ya CHADEMA ipo kwa Msajili toka mwaka 2006 basi wakubali Serikali ya CCM imeshindwa kuongoza na ilipaswa kujiuzulu siku nyingi sana.

Nadhani nimejieleza ya kutosha. Nawaomba wasomaji wapuuze upuuzi huu wa Mwigulu nchemba.

Mkuu Invisible, Fang, Silencer, nk tunaomba mu-tagg hii comment ya Dr.W.Slaa hapo juu kwenye post ya Mwigulu Nchemba.

TUMBIRI (PhD - HULL).
 
Last edited by a moderator:
Natangaza kuanzia leo nikiona uzi umeanzishwa na Mwigulu sifungui kwani huyu jamaa uelewa wake ni mdogo sana.
 
Kama ingetokea muujiza nikapewa uenyekiti wa CCM mtu wa kwanza ambaye ningemweka kando ni Mwigulu kwa kuwa anakitia chama hasara kuliko faida. Mwigulu anatakiwa kufahamu gutter politics hazina nafasi katika kipindi hiki cha dot.com
 
Kumbe hata mauaji ya chacha wangwe yalifanywa na hiki kikundi cha waasi cha red brigade pia kimefanya matukio kama haya sehemu nyingi sana hata tanzania likiwemo la kumteka mama yake zito.
Dr.mmoja ambae yupo kwenye jopo la madaktari bingwa pale muhimbili anadai ugonjwa uliomua Baba wa Taifa Mwl.Nyerere ni sumu iliyotengenezwa na ccm kutokana kuwa kikwanzo kwenye mambo yao,nikamkumbuka pia Colimba kweli ccm hatari...
 
Niliawhi kusema kwamba Mwigulu Mchemba is an IDIOT sasa naona wote mnanielewa.
Hiyo kofia ya MAO unayovaa haikufai hata kidogo kwani itikadi za wachina na zenu magamba ni tofauti sana.
Ben Saanane aliweka bandiko hapa ambalo wengi wamelipa hadhi ya writer-up ya PhD kwa jinsi alivyopangilia maelezo ya tatizo na suluhisho zake, sasa naona na Mwigulu Nchemba kaamua kuiga conposition ile ndio kaishia kuleta haya madudu! Sijui kama kweli Mungu atamsamehe huyu bwana, ni wa kumuombea sana
 
mkuu chadema ni chama cha ajabu sana hawajui kitu kinachoitwa sheria wala utaratibu.

sijawahi kuona chama ambacho kinaongozwa kihuni kama hiki cha chadem wewe ulishaona wapi ukiona mtu anampinga mwenyekiti anauawa huu siyo utaratibu hata kidogo.

MMMMMM!!!
Join 4/7/2013
Post 248! Chadema imewashika pabaya, hii ina maana kazi yako ni kujibu na kuandika -----!, hiki ni kipimo mmekwisha, haya ni maandalizi ya kutoka kwenye uongozi, kila linalojaribiwa ni feki fanyeni wema wananchi ndipo watawakubali, haya majungu hakuna anayoyaamini. Pole!!!!!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom