RC Dar apiga marufuku watendaji walio chini yake kusafiri nje ya jiji bila kibali chake

Hii sheria ipo kwa kila mwajiriwa nchini, hakuna kipya alichokisema hapo! Mwajiriwa yeyote nchini hapaswi kwenda nje ya mkoa wake pasipo ruhusa ya mwajiri wake!

Sikuwa na jua, kumbe mkuu wa mkoa ndio muajiri? Nachojua kila mtumishi kabla ya kuondoka lazima aombe ruhusa kwa mkuu wake wa kazi either DED, DAS, RAS lakini sio kwa mkuu wa mkoa.
Anyways, huenda siko sahihi.
 
angalizo na kwa mikoa mingine ,maana jamaaa aikipitisha jambo dar linaweza pia kupitishwa na mikoa mingine ,na wasiwasi huo.mfano wapiga debe
 
Uyu jamaa anadharau sana anajiona PM juzi majaliwa kasafiri kamtuma mkuu wa wilaya kumsndikiza yeye hadhi yake ni President
 
Kazi kweli kweli .Mfano mtu anatoka mbezi anaenda kibaha MILE MOJA kwa ndugu yake au anaenda kumuona ndugu yake Hospital ya tumbi na kurudi siku hiyo hiyo achukue kibali kwake au mtu anatoka dar na kwenda kumuona mwanawe ST mathew ya Mbagala maana ipo mkoa wa pwani achukue kibali kwake......
ndo maana yake
 
Safari za kikazi

Hawachelewi kupima mkojo kuangalia kama umeenda Mlandizi Jumamosi hawa.

Hizo anaweza kusema anazuia safari holela kubana matumizi.

Najaribu kuwa fair. Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni.

Ila maagizo yatolewe kwa lugha nyepesi, ya upendo na hekima. Ama sivyo wafanyakazi wataona kama wanasimangwa na hilo litashusha morale ya kazi.

Nyota za kiserikali kama Mkuu wa Mkoa anazo.

Makonda ni mtu bogus, lakini kwenye kazi yake kufanya kama kazi yake inavyomruhusu sitaki kumuingilia.

Kama mtu ana safari ya muhimu naamini atampatia kibali.

Mimi mzee wangu alikuwa haishi kusafiri dunia nzima, na safari zake zote anasema alikuwa anapata vibali vya Ikulu. Ni hapa katikati tu katika utawala wa Kikwete watu wameacha kufuata utaratibu wa kupata vibali vya safari. Naona Magufuli kaurudisha. Unasaidia kupunguza safari zisizo za lazima na kupunguza matumizi, ila wasibane sana mpaka safari muhimu ziminywe.

Naandika hayo kama mtu ambaye simfagilii Makonda, Magufuli, Lowassa wala Kikwete.
 
Ningekua mimi nisingekua naitamedia naongea ongea maana kama unajiabisha pia wamwandikie cha kuongea aibu sana kuongea visivyotekelezeka
 
Ha ha ha ha.. Hao aliowapiga marufuku waliomba ajira kutokana na taaluma zao, wakafanyiwa interviews na mwisho kuajiriwa kwa kufuata sheria za kazi..

Yeye amejipendekeza na kufika hapo alipofika bila ya kufanyiwa interview wala vetting.. Aliteuliwa tuu na mtu aliefanana nae akili.. Asijilinganishe na walio kazini kisheria..
Eeeeeh hapo sawa kabisa
 
Kwahiyo nikipata kamchepuko kibaha hapo nikataka nichomoke jumamosi moja nikalegeze chaga lazima niombe ruhusa....maana ni mkoa mwingine ule!
 
RC yuko sawa,kasema wale walioko chini yake.kama hujawahi kuwa chini yake hupaswi kuogopa tamko hilo.
 
Hii sheria ipo kwa kila mwajiriwa nchini, hakuna kipya alichokisema hapo! Mwajiriwa yeyote nchini hapaswi kwenda nje ya mkoa wake pasipo ruhusa ya mwajiri wake!
Unaelewa muajiri ni Nani katika Serikali kuu na Ni Nani katika serikali za mitaa?
 
Kibali anasaini Accounting Afficer ambaye ni CEO/RAS,DED/DAS au Afisa Utumishi kwa niaba ya Accounting Officer, yeye atasaini kama nani? kweli ukipata ziro lazima na akili zitakuwa ni ziro.
Kwa hiyo wale wanaoishi Kibaha na kufanya kazi Dar wataomba ruhusa kwake kila siku?
 
Back
Top Bottom