Ray C amtembelea Rais Kikwete Ikulu jijini Dar, amshukuru kwa msaada wa matibabu!

Steve Dii

JF-Expert Member
Jun 25, 2007
6,402
1,254
Mwimbaji mashuhuri hapa Tanzania, Ray C, ametangaza kupona na matatizo ya yaliyokuwa yakimsumbua. Ametangaza hayo akiwa Ikulu baada ya kupata msaada mkubwa kutoka kwa Mh. Rais Kikwete.

attachment.php

RAY C AKIMSHUKURU RAIS KIKWETE

attachment.php


RAY C, MAMA YAKE NA DADA YAKE WAKIMSHUKURU RAIS KIKWETE
 

Attachments

  • RAY C akimishukur Rais Kikwete.jpg
    RAY C akimishukur Rais Kikwete.jpg
    67.2 KB · Views: 5,794
  • RAY na Mamama na Dada yake ikulu.jpg
    RAY na Mamama na Dada yake ikulu.jpg
    61.7 KB · Views: 5,720
...naaam! Ray C kapona. Hata hivyo anaendelea na matibabu mengine madogomadogo ili kurudisha afya kwa 100% na kuweza kurudi kwenye stage mapema iwezekanavyo!!

Safi sana, inatia moyo kwa kweli.... Nina imani atakuwa amejifunza mengi sana....Na mtakia kila la Kheri!
 
Jamani huyu ni Ray C kweli??machoni ni kama yeye lakini sura kama vile sio yeye as if ni kibibi flan toka korea kaskazini. Kweli unga noumer.
 
Hatimaye baada ya Ray C kuteseka kwa muda mrefu bila kupata mtu wa kumfadhali hela ya matibabu hatimaye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ajitosa kumfadhali. Akiongea katika viwanja vya Ikulu Ray C amemshukuru Rais Kikwete kwa moyo aliouonyesha wa kumsaidia matibabu na sasa hivi anaendelea vizuri.

SWALI:
1.Rais Kikwete ametambua sasa madhara ya madawa ya kulevya, Je, atawachukulia hatua sasa wote wanauzia madawa ya kulevya maana kuna tetesi kuwa anayo majina ya DRUG DEALERS?
2. Je, ni Ray C tu mwenye aliyekumbwa na tatizo la kuwa TEJA? Watanzania wengine tena nguvu kazi kubwa ambayo imeshadhirika na madawa ya kulevya ana mpango upi wa kuwasaidia? Ama wao hawastahili msaada?

AIDHA; Nampongeza Rais Kikwete kwa moyo wake wa kumuokoa Mtanzania huyu " RAY C" maana angepotea na talent yake ya uimbaji.
 
ni kweli huyo ni Ray C nimemuona kwenye taarifa ya habari ya Channel 10 akiwa anacheka na kukenua na Rais Kikwete.

Dah masikini Hawa Ngulume umeugua peke yako mpaka umauti umekukuta.

Umeona eeh, nchi hii bana haina dira wala mwelekeo. Ni rahisi kwa Mateja kupata msaada kutoka magogoni, kuliko kwa viongozi wastaafu. That's why kila aliyeko madarakani anachukua chake mapema, ukizubaa zubaa kama ngulume utakufa unajiona. Anyway RIP ngulume and get well soon Ray C
 
Nami mwanzo nilidhan si Ray c, kumbe ni yeye
Kweli kabadilika, haya kila la heri kwake.
 
Back
Top Bottom