Rais wa Rwanda Paul Kagame awasili Nchini na kufanya Mazungumzo na Rais Samia, leo Aprili 27, 2023

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
Fuatilia yanayojiri kwenye Mapokezi ya Rais wa Rwanda Paul Kagame akiwasili nchini Tanzania leo Aprili 27, 2023.



Rais wa Rwanda Paul Kagame amewasili nchini leo na kupokelewa na Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dr. Stergomena Lawrence Tax kwenye uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu JK. Nyerere.

Msafara huo umeelekea Ikulu ambapo Rais huyo anatarajia kufanya mazungumzo na Mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Samia Suluhu Hassan.

UPDATES;

RAIS SAMIA KUZUNGUMZA NA RAIS KAGAME IKULU YA DAR ES SALAAM

4f63538b-6370-4164-89f0-c6dae8679bbf.jpg
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Rwanda, Paul Kagame mara baada ya kuwasili katika Ukumbi wa Kikwete, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 27 Aprili, 2023.

ec28d238-3b39-4da5-bcf3-c232c5a5a6da.jpg

659baf19-394d-4eb1-b1df-f5fa6460b469.jpg
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mgeni wake Rais wa Rwanda, Paul Kagame mara baada ya kuwasili katika Ukumbi wa Kikwete, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 27 Aprili, 2023.

ec55e762-6935-4727-8a8f-a53de3f75da3.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Mgeni wake Rais wa Rwanda, Paul Kagame mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 27 Aprili, 2023.

MAZUNGUMZO
Rais wa Rwanda, Paul Kagame ambaye yupo katika ziara ya siku mbili Nchini Tanzania amewasili Ikulu ya Magogoni, Dar es Salaam na baada ya mapokezi amekutana na mwenyeji wake Rais Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya mazungumzo ya faragha kabla ya kuzungumza na vyombo vya habari.



Rais Samia amesema miongoni mwa Mambo waliyojadili ni kuimarisha Biashara hasa kwa Kuboresha Bandari, Kuzindua mradi wa Rusumo pamoja na Kuendeleza ushirikiano wa vyombo vya Ulinzi na Usalama.

Naye Rais Kagame amemshukuru Rais Samia kwa mapokezi mazuri aliyopata yeye pamoja na ujumbe aliokuja nao, amesisitiza kuendeleza ushirikiano baina ya nchi ya Rwanda na ndio maana kafika Tanzania kwa kazi hiyo.

Amemshukuru pia Rais Samia kwa kujitoa kwake kwenye kushughulikia migogoro ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, amesema amani na utulivu ni hitaji muhimu sana kwa ajili ya maendeleo na umoja wa Afrika.
 
Kama unafuatilia kupitia Rwanda TV ishu kubwa ni ishi ya mashirikiano kati ya air Tanzania na shirika la Rwanda air, reli , bandari na walimu wa kufundisha kiswahili.

Nimemuona Gabriel Zakaria kumbe amerudi TBC1 baada ya kupigwa chini u- DC anakijua kinywaranda kiasi kama mimi vile .


USSR
 
Kama unafuatilia kupitia Rwanda TV ishu kubwa ni ishi ya mashirikiano kati ya air Tanzania na shirika la Rwanda air, reli , bandari na walimu wa kufundisha kiswahili.

Nimemuona Gabriel Zakaria kumbe amerudi TBC1 baada ya kupigwa chini u- DC anakijua kinywaranda kiasi kama mimi vile .


USSR
Labda kajifunza cha kuombea maji ila nafahamu alikuwa Uganda na Malawi kama mtangazaji.
 
Kagame ngoma ngumu

Lazima ashangae utitiri wa makanisa na manabii wa mchongo bongo

Ova
 
RAIS SAMIA KUMPOKEA RAIS KAGAME IKULU JIJINI DAR ES SALAAM MCHANA HUU.

Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Alhamisi Aprili 27, 2023 atampokea Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame Ikulu ya Dar es Salaam kuanzia saa 9 alasiri. Rais Kagame yuko nchini kwa ziara ya siku mbili leo Alhamisi na kesho Ijumaa.

Fuatilia matangazo ya moja kwa moja kupitia Akaunti zetu za Instagram: ikulu_mawasiliano, Facebook: Ikulu Tanzania
Facebook fanpage: Ikulu Mawasiliano
Twitter: ikulu_Tanzania
Youtube Channel: Ikulu Tanzania
Tovuti: ikulu.go.tz
 

Attachments

  • 20230427_140518.jpg
    20230427_140518.jpg
    100.2 KB · Views: 7
Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan atampokea Ikulu Jijini Dar es Salaam, Rais wa Rwanda Paul Kagame leo ambapo tukio hilio lintarajiwa kuwa mbashara kuanzia saa 9:00 Alasiri.

Je tutegemee nini kutokana na ziara hii kutokana na historia kati ya nchi za Tanzania na Rwanda lakini pia ikizingatiwa Rais Kagame anakuja nchini akitokea kwenye mkutano wa kimkakati wa mageuzi barani Afrika uliofanyika nchini Zimbabwe huku Rais Kagame akiongoza kikao cha bodi ya Smart Africa (Smart Africa Board Meeting) kilichojumuisha wajumbe kutoka mataifa 36 kikilenga kujadili maendeleo ya Kidijitali barani Afrika.

Tutegemee yapi katika mkutano wa viongozi hawa?
 
Rais wa Rwanda, Paul Kagame yupo katika ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Tanzania.

Baada ya kupokewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Stergomena Tax katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, Rais Kagame atakutana na mwenyeji wake Rais Samia Suluhu Hassan, Ikulu ya Magogoni, Dar es Salaam.

Tanzania na Rwanda zimekuwa na uhusiano wa muda mrefu na zimekuwa zikishirikiana kwenye mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na biashara, uwekezaji, nishati, uchukuzi, elimu na utamaduni.



 
Kwani HABARI ikulu haijasema PK anakuja kuongea na mama Issues zipi..🤔
Mkuu ebu tusichoshane, haya mambo ya kupasua kichwa kujadili mambo ambayo bado yapo kwenye fikra za watu wengine, sio poa aiseeeee.....🤨
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom