Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 8,171
- 11,572
Tendo la ndoa baina ya wanandoa na wachumba ni chachu na kiungo kimojawapo muhimu sana cha kuimarisha upendo, uaminifu, furaha na muunganiko wa wanandoa au wachumba.
Ni tendo muhimu sana linaloweza kuimarisha na kuchochea zaidi uimara wa ndoa au uchumba likitumiwa vizuri, kwa hiyari, ubunifu, ustadi, maarifa, umahihiri, unyenyekevu, utayari na kwa utoshelevu.
Lakini pia likitumiwa vibaya kana kwamba ni adhabu, karaha, usumbufu, uchafu au uonevu basi, upendo ndani ya ndoa au uchumba huo unaweza kuchomoka na kutafuta makazi mahala pengine kwa faraja ya muda ya kificho.
Kupanga ratiba ya kufanya tendo la ndoa kwa wana ndoa au wachumba ni mwanya au uchepushaji wa upendo wa ndani ya ndoa kwenda nje ya ndoa. Tendo la ndoa lifanyike wakati wowote bila ratiba, wanandoa au wachumba wanapopata joto la kuhisi kufanya tendo, iwe sebuleni nyakati za usiku mkalai, jikoni watoto wakiwa shule, chumbani na mahali popote tulivu pa faragha panapo weza kuwapa uhuru na kuwasitiri haja stahiki.
Kila la kheri sana...