RASMI: Belouizdad yamfuta kazi kocha wake Sven Vandernbroeck (Kishingo) aliyekuwa kocha wa zamani wa Simba

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,866
Klabu ya CR Belouizdad ya Algeria Imetangaza Kumfuta Kazi Kocha wake Mkuu Sven Vandenbroeck raia wa Ubelgiji Kufuatia Mwenendo Mbaya wa Timu hiyo katika mechi za Ligi kuu ya Algeria (League 1) ambapo Wikiendi hii Timu hiyo ilipoteza mchezo wake wa Ligi wakiwa nyumbani dhidi ya Klabu ya Khenchela FC kwa Kukubali Kichapo Cha Magoli (3-2):

- Sven Kocha wa Zamani wa Simba SC, FAR Rabat na Wydad Casablanca zote za Morocco amehudumu katika Klabu hiyo kwa muda wa Miezi minne tu tangu alipojiunga na Timu hiyo mwezi Julai mwaka huu, Sven ameiacha timu hiyo katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Timu hiyo inashika Nafasi ya (11) katika msimamo wa Ligi kuu ya Algeria.

CR Belouizdad inategemea kukutana na yanga kwenye mechi za makundi CAF Championship.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom