Raisi wangu Kikwete, Lowassa atakupunguzia kura.

Nyauba

JF-Expert Member
Jul 10, 2008
1,098
105
amka2.gif

RAIS wangu, makala iliyopita imewagusa watu wengi mno! Kwakuwa mwangwi wake umekuwa mkubwa, hivi nimeona ni bora niinyumbue ili iwe wazi zaidi. Imeandikwa, “Tazama jinsi ilivyo vyema na kupendeza, ndugu wakae pamoja, kwa umoja.”
Ndugu rais, haya ndiyo yamekuwa matamanio yangu katika siku hizi zangu zilizobakia. Ardhi ya Tanzania ndiyo mama yetu wote. Humo tulitoka na humo tutarudi. Sisi wote tu wasafiri tuko njiani, hatujui lini tutafika. Kujikusanyia mali nyingi ni masumbuko ya dunia. Mungu wetu ni mmoja. Ugomvi kati yetu wa nini?
Ndugu kwa ndugu wanashambuliana hadharani kugombania vyeo. Mungu wetu amekaa kimya na uongozi wetu nao umekaa kimya! Nao kumbe ni sehemu ya tatizo. Uko wapi uongozi wa watu ulio chaguo la Mungu?
Rais wangu, ili kupata mahali muafaka pa kuanzia nazianika meseji chache ili wasomaji wazisome nao waelewe. Lusato aliandika, “Hi Bro! Nafuatilia sana TZ Daima. Inaonyesha una ukweli wote juu ya Lowassa tofauti na tujuavyo. Tuambie ukweli wote ili tuwe nuruni na Lowassa atakasike.”
Mwana mwema aliandika, “Za siku Mzee Mayega, naitwa Kijazi. Nasema kutoka moyoni kwamba, wewe huandiki kwa kumfurahisha mtu. Umeegemea kwenye ukweli. Makala ya leo ni ukweli usio na shaka.”
Mwana mwema mwingine kutoka Chuo Kikuu Dsm akaandika, “Mwalimu Mkuu wa Watu unakatisha tamaa na uandishi wako wa hivi sasa kumpiga vita Spika na kuwatetea watuhumiwa. Ni mimi Sam UDSM.”
Mwingine aliona aibu kujitambulisha, akaandika, “Unaonyesha una akili na busara nyingi sana ila akili na busara za Watanzania zimekuwa zikiathiriwa na rushwa, nahisi umo kwenye payroll ya Lowassa.”
Huyu naye hakujitambulisha aliandika, “Mwalimu kazi yako ni nzuri. Uzuri maandishi hayafi, tutakufa sisi, ndio maana hadi leo tunawasoma akina Plato. Naamini historia itakukumbuka na itakutendea haki wakati ukifika.”
“Bwana akulinde na kukuinulia uso wake Mr. Paschally Mayega. Kazi yako nimeikubali, nakupongeza sana toka ndani ya sakafu ya moyo wangu. Tangu nianze kusoma gazeti na makala mbalimbali hii yako ni mwanzo na mwisho. Tatizo kubwa la wanahabari au si karama yao ni ufitini na unafiki, ila wewe humtumikii mtu, endelea na Mungu atakubariki.”
Mlagala wa Mbezi akaandika, “Huyu rais unamwandikia mambo mazito sana. Nadhani hakuelewi kama mimi na wewe tulivyoshindwa kumwelewa Lowassa alipotoa maneno mazito wakati ule akijiuzulu. Sijui nchi itakuwa katika hali gani atakapokuja kuelewa kuhusu ukweli. Lowassa ni shujaa.”
Mwana mwema Issack kutoka Arusha akaniandikia, “Mwalimu mkuu shikamoo. Rafiki zangu wanaomba makala ijayo usimwandike tajiri yako wala Richmond. Mkumbushie rais wako ahadi zake na maisha yetu bora, au alimaanisha, Bora Shoes?”
Mwalimu Salim Dan akaandika, “Mwalimu wangu mara nyingi nasoma mafundisho yako adhimu na machungu. Sijui imetokeaje, lakini kila nikikusoma nawaombea vifo wanaotutawala.”
Mwalimu kutoka Kawe akaandika, “Mimi ni mmoja wa wale wanaoshangaa vile Mungu alivyokutunuku ujasiri na namna unavyoutekeleza. Sio ati nakusifu, bali hakuna kama wewe. Wengi tumejaliwa vipaji na pengine hatujielewi, licha ya kutovitumia. Amini usiamini unagusa mioyo yetu kiasi ambacho haielezeki. Unachofanya ni kazi ya Mungu na kama kuna mwingine kama wewe ni nadra sana. Mungu akubariki.”
Mwana mwema Peter kutoka Kariakoo akasema, “Mbona mnampamba sana huyu Lowassa? Tunataka na sehemu waliyoiacha akina Mwakyembe nayo iwekwe hadharani ili tuwahukumu wote.”
Kutoka Mto wa Mbu Arusha, mwana mwema Ramadhani akaandika, “Mwalimu nimekusoma mara nyingi na niliwahi kukwambia unachokusudia unakificha katikati ya maandishi na kugusa kwa tahadhari, lakini leo umeutendea moyo wako haki. Sisi huku jimboni tunamfaidi huyu Lowassa japo alitoswa huko juu, lakini naomba msaada wako. Kwa sababu unamkubali Nyerere, mfumbulie hili fumbo la kumkataa Lowassa kiasi leo wanasema yanayompata ni laana yake, nisaidie tafadhali.”
Ndugu rais, huyu nilimjibu kuwa akumbuke uvumi ulioitikisa Dar es Salaam nzima mwanzoni mwa miaka ya 80. Ilidaiwa mwanaume alitembea na mke wa mtu. Alipoenda kuoga akageuka chatu mwili mzima kasoro kichwa tu.
Karibu jiji zima lilikivamia Kituo cha Polisi Buguruni walikodai amehifadhiwa. Mimi pia nilikuwa mmoja wao, wajinga ndio waliwao, nilisafiri toka Kurasini mpaka Buguruni. Ajabu ni kwamba kila niliyemuuliza kulikoni alinijibu kwa uhakika kabisa kuwa mtu kageuka chatu!
Ajabu nyingine ni kwamba kila niliyemuuliza, umemwona wewe mwenyewe huyo mtu-chatu? Alinijibu kwa uhakika kabisa kuwa, “Mimi sijamwona” lakini aliendelea kueneza uvumi. Nikamwambia na wewe unaendeleza uvumi wa kusikia usio na ukweli wowote!
Uvumi wa kukataliwa Lowassa na Nyerere nimeusikia kwa watu wengine pia. Ajabu ni kwamba kila niliyemuuliza ulikuwapo ukamsikia Nyerere mwenyewe akimkataa? Alinijibu kwa uhakika kabisa, “Sikuwapo na sijawahi kumsikia Nyerere mwenyewe akimkataa Lowassa” lakini aliendelea kueneza uvumi. Jambo gani linaonyesha kuwa Lowassa anaishi kwa shida mpaka awaziwe kuwa ana laana? Kama ni uwaziri mkuu si alijiuzulu mwenyewe, kwani alifukuzwa?
Anzisha uvumi wowote wa kijinga, utatupata tu, wajinga tuko wengi. Na kama ni mwaka 1995 Nyerere hakumkataa mtu zaidi ya yule mzee wa Dodoma! Bali aliwauliza washangiliaji waliokuwa wakishabikia kijinga kuwa, “Nyinyi ni wahuni? Hivi ndivyo tunavyomchagua rais wetu?”
Rais wangu, hizi ni meseji chache kati ya nyingi nilizopokea. Yawezekana kabisa mtu akaona namsemea ndugu Edward Lowassa, lakini mimi ni mwanadamu. Ninachokifanya ninakijua na Mungu wangu anakijua. Nitakisimamia kile ambacho naamini kuwa ni kweli mpaka siku yangu ya mwisho.
Kama kweli kwa moyo wako wote unaamini kuwa namsemea Lowassa, basi elewa kuwa Lowassa amesimama upande ilipo kweli. Kuikataa kweli ni sawa na kujilisha upepo.
Ndugu rais, nimefarijika sana moyoni mwangu kupata habari za karibu kabisa za ndugu Lowassa. Amekaririwa akisema, “Makala ni nzuri, nzito iliyojaa busara na kweli. Lakini kilichonifurahisha zaidi ni kuona mwandishi anaandika ukweli kutokana na uchungu uliomo ndani ya moyo wake, bila kushawishiwa na mtu yeyote.” Akili ni nywele, anayetaka kuelewa ataelewa! Nawashangaa wanaomtetea Lowassa.
Mtu yule amejaliwa upeo mkubwa wa kufikiri na kwa hilo wote hawa wanamwogopa. Akanikumbusha mtu wa Mungu mmoja ambaye ni waziri akiwa Dodoma bungeni mwezi uliopita alinipigia simu na kuniambia, “Nakupongeza sana kwa maandiko yako. Yanasomwa na watu makini wengi sana na wanakukubali. Wewe ni mwandishi ambaye hutumwi na mtu yeyote.” Akajitambulisha kwa kunitajia majina yake yote matatu. Mungu ambariki mtu huyu, yeye na nyumba yake.
Rais wangu, siku zinakuja, siku ambazo Tanzania yenye neema itawezekana. Walikuja manabii wa uongo wakawaahidi Watanzania mbingu ya maisha bora, na sasa wanahaha kwa kupiga ramli za kurudia madarakani. Siku zinakuja siku ambazo Watanzania watakuwa katika jukwaa moja wakiimba nchi yangu kwanza! Hawatajali tofauti zao za kisiasa wala za kidini.
Na juu ya jukwaa hilo hakutakuwa na mahakimu bali wapatanishi. Hakutakuwa na watuhumiwa bali wenye makosa. Wengine wote juu ya jukwaa hilo watakuwa wapendwa, wajamaa wa jamii moja.
Baada ya wewe kulihutubia Bunge kwa hotuba ndefu sana, Samuel Sitta, Spika wa Bunge la Jamhuri alisimama haraka na kutoa hotuba fupi sana. Ilijaa busara, hekima na uwezo wa kufukia mashimo marefu ndani ya mioyo ya wananchi yaliyochimbwa na ile hotuba yako ndefu.
Niliandika kupongeza kitendo hicho chema kilichofanywa na Spika wetu. Wakasema sikufanya sawasawa kwa sababu Spika kwa kufanya vile hakuonyesha nidhamu mbele ya mkuu wa nchi. Niliwaambia kuwa heshima ya mkuu wa nchi haitoki kwa wananchi bali hutokana na matendo ya mkuu wa nchi mwenyewe kwa wananchi wake!
Leo haohao wanasema nampiga vita Sitta. Watuambie basi kilichomfanya Spika wetu aikatae hoja njema ya ufisadi kama ilivyowasilishwa kwake na mwana mwema Dk. Willbrod Slaa wa CHADEMA. Baada ya kunyimwa haki yao ya kuizungumzia hoja yao ndani ya jengo lao la uwakilishi wa wananchi kwa uhuni tu, wanawema hawa hawakukata tamaa.
Walikwenda wakaiwasilisha kwa wananchi wakiwa chini ya mwembe. Majina ya watuhumiwa wa ufisadi yaliorodheshwa yote waziwazi. Vita dhidi ya ufisadi ya Spika Sitta na wenzake iliwafutia tuhuma karibu wote.
Wananchi waliambiwa kuwa waasisi wa kile kilichoitwa mtandao walikuwa watano. Sitta na Lowassa wakiwamo. Waligawana vyeo. Wewe utakuwa rais. Bwana Sitta waziri mkuu. Bwana Chumvi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na wengine wawili vyeo vya juu. Baada ya kuitwaa nchi, bwana Sitta hakuwa waziri mkuu wala bwana Chumvi hakuupata ule uwaziri uliokusudiwa, akaambulia uwaziri kiduchu.
Mtafaruku uliozuka baada ya hapo ulisababisha bwana la Aziz anayetajwa kuwa mmoja wao akalilalamikia taifa kuwa anachukiwa bure kwa kudhaniwa tu kuwa yeye ndiye aliyekuwa anagawa vyeo.
Rais wangu, ndugu Sitta akanushe haya ili wananchi wasidhani kuwa aliweka fundo moyoni mwake dhidi ya bwana Lowassa kwa ‘kum ovateki’ katika uwaziri mkuu wake. Vyombo vya habari vilipoiibua kashfa ya Richmond na Sitta kugundua kuwa Lowassa yumo ndani aliidaka kindakindaki. Akajua kuwa Lowassa kaingia ndani ya kumi na nane zake.
Akamwita kijana wake na vijana wengine akawapa kazi ya kumpiga kipapai Lowassa. Kazi hii sasa ikaitwa vita dhidi ya ufisadi. Vijana wahojaji waliwahoji wote, Lowassa hakuguswa! Bahati mbaya ya kupangwa! Edward Lowassa akafanywa kuwa fisadi kuliko mafisadi wote duniani.
Richmond ikafanywa kuwa ni ufisadi mkubwa uliotendwa katika nchi hii kuliko ufisadi mwingine wowote ulioko nchini. Hata wa IPTL ambao kama ungekuwa ni mlima, Richmond ni kichuguu. IPTL ni Mlima Kilimanjaro haukuguswa. Vita njema ikageuzwa na kuanza kupiganwa kifisadi. Nchi njema haiwezi kuendeshwa kihuni namna hii!
Ugomvi wa Sitta na Lowassa sisi Watanzania wengine ungetuhusu vipi? Lakini Spika Sitta kuufunga mjadala wa Richmond kwa sababu za hovyohovyo kama zile ndiko kunakoleta majonzi na majuto kuona kuwa huyu mtu amelitumia Bunge kuisimamisha nchi isifanye lolote kwa miaka miwili kwa chuki binafsi tu.
Yatolewe maelezo ya kina na Spika mwenyewe vinginevyo sioni kosa kwa wote wanaotaka Spika na genge lake walaaniwe! Kitu ambacho hawakukijua ni kwamba uongo hausimami peke yake kwa muda mrefu. Kikao cha Bunge kilichopita kimewavua nguo. Na kwakweli wamejivua nguo wenyewe. Madhara walioisababishia nchi kwa vita ya mtu mmoja ni makubwa mno. Hayawezi kupita bila watu hawa kuadhibiwa.
Ndugu rais, tusaidie, hawa wanaosema hakuna kiongozi wa juu bali kuna ombwe la uongozi na kwamba mwenyekiti ni dhaifu mno kiuongozi, sisi tunaokuunga mkono tukitaka kuwajibu tuwape sababu zipi kuwaonyesha kuwa si kweli?
Makapi ya maprofesa wanaotuletea sifa za mvuto katika swala zito kama hili la kumtafuta kiongozi mkuu wa nchi, badala ya kumpelekea ndugu Lundenga mwenye mashindano yake, tuwabanebane vipi? Profesa kuwa kihiyo siyo ‘contradiction in terms’ bali ni ‘paradox’ kwa hiyo inawezekana kama tunavyoshuhudia leo kwa profesa huyu.
Rais wangu, tutaungana na mwanamwema, mwanamke jasiri wa ukweli Ananilea Nkya na wanaharakati wenzake kuizunguka nchi yetu kuwaambia Watanzania juu ya uhuni huu. Tutafika Nyamongo, tutafika Loliondo, TICTS na TRL na popote penye dhuluma mpaka kwa wazazi wetu na vijana wetu walioko Urambo kuwaeleza jinsi mtu huyu, Spika Sitta alivyoliongoza Bunge kuwasaliti Watanzania kwa kuizima hoja ya ufisadi.
Ndugu Ngallawa mmoja kati ya wazee wanaoheshimika sana katika jamii yetu, alikuwa na yake kuhusu wapambanaji feki wa ufisadi.
Nasisitiza tena, mimi simchukii mtu. Tatizo ni pale ninapogeuka na kumwangalia binti yangu. Remmy Ongala aliimba, “Tajiri na mali yake, maskini na mtoto wake.” Mwenyezi Mungu peke yake ndiye atamhukumu!
Rais wangu, nimalizie mada ya leo kwa kusema bado naamini kuwa uwingi au uchache wa kura zetu za urais au hata kuupata au kuukosa urais wenyewe katika uchaguzi mkuu ujao utategemea sana msimamo wa ndugu Edward Ngoyayi Lowassa.
Labda ikanushwe sasa, lakini kama kweli aliwaongoza wanamtandao mpaka wakaifunika CCM na kuitwaa nchi 2005, ni kipi kitamzuia leo? Kisiki kingekuwa Bunge lakini sasa nalo limenywea kukiri nguvu kubwa aliyonayo. Mambo mengi ya hila yalifanyika kufanikisha kuingia kwetu Ikulu, akisema ayaweke hadharani ni nani kati yenu atabaki salama? Muda wote huu kakaa kimya, anawaza na kupanga nini? Tukibakia na ushabiki wetu wa kijinga kuwa huyu anapendeza, Lowassa atatuchagulia rais ajaye! Ni nadra sana katika maisha yetu ya kawaida kumkuta mtu mwenye uwezo wa kujenga, asiye na uwezo wa kubomoa! Tumwombe Edward, amtangulize Mungu mbele aisaidie nchi hii mwezi wa kumi ipate uongozi ili taifa lipone!

my take:Hivi huyu mwandishi anaongozwa na hisia zake au naye ni sehemu ya ufisadi!!!

Na Paschally Mayega Tz Daima.

Uandishi wa huyu Mayega umebadilika ghafla kama alivyobadilika Mrema vile , pengine bwana Mayega nae kuna kitu anawauzia mafisadi!! Ukweli Mayega ni kwamba ,Lowassa bila Rostam si lolote ; mtu anayeweza kumuangusha Kikwete ni huyo burushi kwani ndio mwenye mkoba wa siri zote!! Lowassa hafukuti asipobebwa na huyo burushi!!
 
Aisee Nyauba, asante kwa ulichokiandika ingawa sijasoma kwa sababu inaumiza macho.

Unapokuwa na habari ndefu kama hii, inabidi uwe unaacha nafasi kati ya paragraph na paragraph. Hapo macho hayatachoka
 
Kambi za 2010. Mayega amepewa nafasi kubwa kwenye gazeti lile anaitumia anavyoona inafaa. Yeye anampenda na kumthamini Lowasa kuliko JK?
 
Labda ikanushwe sasa, lakini kama kweli aliwaongoza wanamtandao mpaka wakaifunika CCM na kuitwaa nchi 2005, ni kipi kitamzuia leo? Kisiki kingekuwa Bunge lakini sasa nalo limenywea kukiri nguvu kubwa aliyonayo. Mambo mengi ya hila yalifanyika kufanikisha kuingia kwetu Ikulu, akisema ayaweke hadharani ni nani kati yenu atabaki salama? Muda wote huu kakaa kimya, anawaza na kupanga nini? Tukibakia na ushabiki wetu wa kijinga kuwa huyu anapendeza, Lowassa atatuchagulia rais ajaye! Ni nadra sana katika maisha yetu ya kawaida kumkuta mtu mwenye uwezo wa kujenga, asiye na uwezo wa kubomoa! Tumwombe Edward, amtangulize Mungu mbele aisaidie nchi hii mwezi wa kumi ipate uongozi ili taifa lipone

My take: Huyu mwandishi anaongozwa na hisia kweli??
 
imekaa njema

ila inaumiza macho
hukuipanga vizuri

kazi za kupaste bana!!!
 
Think twice!
 
Uandishi wa huyu Mayega umebadilika ghafla kama alivyobadilika Mrema vile , pengine bwana Mayega nae kuna kitu anawauzia mafisadi!!

Bulesi, Nakubaliana na maneno yako haya.
Kwa maoni yangu, Mayega ni mwandishi 'mzuri' anayajua vyema matatizo ya nchi yetu, anaweza kuyaelezea kwa ufasaha na kama walivyo waandishi makini yaelekea huwa anayafanyia utafiti yale anayotaka kuandika. Hata hivyo, wakati mwingine nilikuwa naona kama alikuwa anamsakama JK kupita inavyohitajika.

Pamoja na hayo, ana muda sasa ameonyesha kugeuka/kubadilika katika uandishi wake. Ukisoma makala zake siku hizi lazima atatafuta mahali alipachike jina la Lowassa kwa namna ya kusifia utendaji kazi wa Lowassa. Mie nadhani kuna namna imepita. Anayeandika sasa si yule Mayega tuliyemjua ambaye aliandika kitabu cha hadithi ya nchi moja yenye matatizo yaliyofanana na ya Tanzania na hatma ya nchi ya aina hiyo. Kitabu hicho kimejaa uamsho ili watu wazinduke na hatimaye kufanya maasi dhidi ya Serikali yao!

Wakati mwingine sisi binadamu katika unyonge wetu, matatizo yanaweza kutufanya tutende yale ambayo huko nyuma hatukudhamiria wala kudhani kwamba tunaweza kufanya.

Kama inavyodhihirika hapa, uandishi wa Mayega unaanza kutiliwa mashaka na wasomaji waliokuwa wanamuona ni mkweli. What a shame, kwa mwandishi aliyekuwa akionyesha umakini na uzalendo katika makala zake!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom