Raisi Samia, kama unaona mbali, legacy kubwa ya kipekee na ya kudumu ni Katiba Mpya. Majengo na vitu vingine vinasahaulika hasa kwa vizazi vijavyo

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,022
144,379
Katika uzinduzi wa Ikulu ya Chamwiono leo hii tarehe 20/05/2023, imejitokeza hali ya kila mmoja kutaka kuonekana ana legacy katika ujenzi wa Ikulu hiyo, lengo ni kila mtu aingie kwenye kumbukumbuku ya waliohusika kufanikisha ujenzi wa Ofisi hizo za Raisi hapa mkoani Dodoma.

Katika hili, namshauri Raisi Samia kuwa kitu pekee kitachompa sifa ya kipekee na itayodumu vizazi na vizazi ni kuwapatia watanzania Katiba Mpya hata kama katiba hiyo inaweza pelekea yeye na chama chake kuondoka madarakani.

Kilio kikubwa cha watanzania sio Ikulu ya Chamwino wala Bwawa la Umeme au Reli ya Kisasa(SGR) na mambo mengine ya aina hiyo, bali hitaji kubwa la watanzania ni Katiba Mpya itayoponguza madaraka ya uraisi, itayotupa Tume Huru ya Uchaguzi, itayoweza kuwajibisha viongozi mafisadi, itayowapa wananchi wananchi fursa ya kuwadhibu viongozi wa kisiasa(wa kuchaguliwa) kama wabunge na madiwani, itayotupa Muundo Sahihi wa Muungano(serikali 3), itayoruhusu matokeo ya uraisi kuhojiwa mahakamani, n.k.

Hivyo, Raisi Samia, tambua hii fursa sasa iko kwako na pengine kuna wenzako wanatamani ufeli katika hili ili usipate hiyo sifa na badala yake wanaomba waje waipate wao. Inawezekana kabisa hata Kikwete leo hii anajilaumu kwa kushindwa kuwapatia watanzania Katiba Mpya kwani alikuwa na hiyo nafasi na bahati mbaya akaipoteza.

Mhe, Raisi, infrasture na vitu vingine vya aina hiyo, vimejengwa na wakoloni na baadhi vimeendeea kujengwa na watangulizi wako, ila impact yake huwa ni ya muda tu na vikishazoeleka, vinaonekana ni vya kawaida tu na watu kutaka vijengwe vingine vya kisasa zaidi au viboreshwe na hivyo kufanya vya awali visionekane vyenye thamani tena(sio dhahabu).

Jiulize nani leo hii anamsifia au anamkumbuka Mkapa kwa kuanzisha Television ya Taifa(TVT enzi hizo), nani anamsifia au anamkumbuka Nyerere kwenye ujenzi wa Reli ya Tazara, nani anamkumbuka au kumsifia Mzee Mwinyi kwa ujenzi wa miundombinu ya barabara wakati wake, nani anamsifia au kumkumbuka Kikwete kwa ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma, n,k. Ukipata majibu, basi utajua hatima ya legacy ya kujenga Ikulu, bwawa la umeme, n.k. japo ni vya muhimu na tunavihitaji.

Kwa upande wa katiba mpya, hali ni tofauti kabisa kwani matunda ya katiba mpya ni ya kudumu na kukumbukwa siku zote. Kwa mfano, kila uchaguzi unapofanyika na watu wakahoji matokeo ya uraisi mahakamani, basi ujue watanzania watakukumbuka sana kwa kuwapa hiyo nafasi tofauti na ilivyo hivi sasa.

Watanzania wakipata katiba itayotibu tatizo la Muundo wa Muungano, utaiingia katika historia kubwa na ya kipekee tofauti na ya kukamilisha ujenzi wa Bwawa la Umeme huko mto Rufiji na miradi mingine mikubwa unayoendelea kuikamilisha.

Watanzania wakipata katiba itayopunguza madaraka ya Raisi na kuimarisha Mamlaka au Nguu ya Bunge na kuipa Mahakama uhuru wa kutosha,basi utambue utaheshimika na kukumbukwa na vizazi vingi vinavyokuja.

Hiyo ni mifano michache miongoni mwa mingi itayopatikana kama matunda ya katiba mpya.

Mhe Raisi, ukitaka kuingia katika kundi moja la watu kama kina Mandela, Martin Luther King, na wengineo ambao hawakujenga miundombinu katika nchi zao bali wanaheshimika dunia nzima kuliko wale walijenga miundombinu katika nchi hizo, basi wapatie watanzania Katiba Mpya na iliyo bora, nakuhakikishia utaingia katika historia ya nchi hii hata kama katiba hiyo itafanya wewe na chama chako mshindwe uchaguzi na kuondoka madarakani.

Raisi Samia jenga picha ya wewe kukabidhi madaraka kwa upinzani na katika hafla hiyo, ukachomekea maneno: "katiba mpya na bora, leo imewezesha wapinzania kuingia madarakani". Mhe, Sentesi hiyo moja tu inaweza kuja kunukuliwa mara nyingi sana huko mbeleni na kufanya ukumbukwe daima kila itapokuwa inanukuliwa na hakika itakupa faraja kubwa sana katika maisha yako hapa duniani hata kama utakuwa umepoteza uchaguzi wewe na chama chako.

Mhe. Raisi, miaka hamsini ijayo, Ikulu ya Chamwino haitakuwa habari tena, ila katiba mpya na bora itaendelea kukuweka kwenye ramani.

Mzee Warioba, kwa kutupatia tu Rasimu ya Katiba Mpya, leo hii tayari ni living example ya hiki ninachokisema.

Madaraka ni ya kupita, ila namna gani umetumia madaraka yako, hii ndio legacy na legacy ni ya kudumu. So, it is upon you to choose between what is temporary and what is permanent.
 
Katiba haitakuja kirahisi kama unavyofikiri,nguvu kubwa na shinikizo ikiambatana na baadhi kuumia

Nchi ngumu sana hii
 
Sina imani thabiti na rais Samia kuhusu katiba mpya lakini akifanya hivyo hakika ataonekana mwanamke shupavu na shujaa kwa kukamilisha jambo ambalo wanaume wameshindwa na yeye mwanamke kaweza.
Kuna wakati utafika watatamani legacy ya kuwaachia watanzania katiba mpya na iliyo bora ingekuwa yao.
 
Katika uzinduzi wa Ikulu ya Chamwiono leo hii tarehe 20/05/2023, imejitokeza hali ya kila mmoja kutaka kuonekana ana legacy katika ujenzi wa Ikulu hiyo, lengo ni kila mtu aingie kwenye kumbukumbuku ya waliohusika kufanikisha ujenzi wa Ofisi hizo za Raisi hapa mkoani Dodoma.

Katika hili, namshauri Raisi Samia kuwa kitu pekee kitachompa sifa ya kipekee na itayodumu vizazi na vizazi ni kuwapatia watanzania Katiba Mpya hata kama katiba hiyo inaweza pelekea yeye na chama chake kuondoka madarakani.

Kilio kikubwa cha watanzania sio Ikulu ya Chamwino wala Bwawa la Umeme au Reli ya Kisasa(SGR) na mambo mengine ya aina hiyo, bali hitaji kubwa la watanzania ni Katiba Mpya itayoponguza madaraka ya uraisi, itayotupa Tume Huru ya Uchaguzi, itayoweza kuwajibisha viongozi mafisadi, itayowapa wananchi wananchi fursa ya kuwadhibu viongozi wa kisiasa(wa kuchaguliwa) kama wabunge na madiwani, itayotupa Muundo Sahihi wa Muungano(serikali 3), itayoruhusu matokeo ya uraisi kuhojiwa mahakamani, n.k.

Hivyo, Raisi Samia, tambua hii fursa sasa iko kwako na pengine kuna wenzako wanatamani ufeli katika hili ili usipate hiyo sifa na badala yake wanaomba waje waipate wao. Inawezekana kabisa hata Kikwete leo hii anajilaumu kwa kushindwa kuwapatia watanzania Katiba Mpya kwani alikuwa na hiyo nafasi na bahati mbaya akaipoteza.

Mhe, Raisi, infrasture na vitu vingine vya aina hiyo, vimejengwa na wakoloni na baadhi vimeendeea kujengwa na watangulizi wako, ila impact yake huwa ni ya muda tu na vikishazoeleka, vinaonekana ni vya kawaida tu na watu kutaka vijengwe vingine vya kisasa zaidi au viboreshwe na hivyo kufanya vya awali visionekane vyenye thamani tena(sio dhahabu).

Jiulize nani leo hii anamsifia au anamkumbuka Mkapa kwa kuanzisha Television ya Taifa(TVT enzi hizo), nani anamsifia au anamkumbuka Nyerere kwenye ujenzi wa Reli ya Tazara, nani anamkumbuka au kumsifia Mzee Mwinyi kwa ujenzi wa miundombinu ya barabara wakati wake, nani anamsifia au kumkumbuka Kikwete kwa ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma, n,k. Ukipata majibu, basi utajua hatima ya legacy ya kujenga Ikulu, bwawa la umeme, n.k. japo ni vya muhimu na tunavihitaji.

Kwa upande wa katiba mpya, hali ni tofauti kabisa kwani matunda ya katiba mpya ni ya kudumu na kukumbukwa siku zote. Kwa mfano, kila uchaguzi unapofanyika na watu wakahoji matokeo ya uraisi mahakamani, basi ujue watanzania watakukumbuka sana kwa kuwapa hiyo nafasi tofauti na ilivyo hivi sasa.

Watanzania wakipata katiba itayotibu tatizo la Muundo wa Muungano, utaiingia katika historia kubwa na ya kipekee tofauti na ya kukamilisha ujenzi wa Bwawa la Umeme huko mto Rufiji na miradi mingine mikubwa unayoendelea kuikamilisha.

Watanzania wakipata katiba itayopunguza madaraka ya Raisi na kuimarisha Mamlaka au Nguu ya Bunge na kuipa Mahakama uhuru wa kutosha,basi utambue utaheshimika na kukumbukwa na vizazi vingi vinavyokuja.

Hiyo ni mifano michache miongoni mwa mingi itayopatikana kama matunda ya katiba mpya.

Mhe Raisi, ukitaka kuingia katika kundi moja la watu kama kina Mandela, Martin Luther King, na wengineo ambao hawakujenga miundombinu katika nchi zao bali wanaheshimika dunia nzima kuliko wale walijenga miundombinu katika nchi hizo, basi wapatie watanzania Katiba Mpya na iliyo bora, nakuhakikishia utaingia katika historia ya nchi hii hata kama katiba hiyo itafanya wewe na chama chako mshindwe uchaguzi na kuondoka madarakani.

Madaraka ni ya kupita, ila namna gani umetumia madaraka yako, hii ndio legacy na legacy ni ya kudumu. So, it is upon you to choose between what is temporary and what is permanent.
Mungu amjaalie akusikie , Amina

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
 
Katika uzinduzi wa Ikulu ya Chamwiono leo hii tarehe 20/05/2023, imejitokeza hali ya kila mmoja kutaka kuonekana ana legacy katika ujenzi wa Ikulu hiyo, lengo ni kila mtu aingie kwenye kumbukumbuku ya waliohusika kufanikisha ujenzi wa Ofisi hizo za Raisi hapa mkoani Dodoma.

Katika hili, namshauri Raisi Samia kuwa kitu pekee kitachompa sifa ya kipekee na itayodumu vizazi na vizazi ni kuwapatia watanzania Katiba Mpya hata kama katiba hiyo inaweza pelekea yeye na chama chake kuondoka madarakani.

Kilio kikubwa cha watanzania sio Ikulu ya Chamwino wala Bwawa la Umeme au Reli ya Kisasa(SGR) na mambo mengine ya aina hiyo, bali hitaji kubwa la watanzania ni Katiba Mpya itayoponguza madaraka ya uraisi, itayotupa Tume Huru ya Uchaguzi, itayoweza kuwajibisha viongozi mafisadi, itayowapa wananchi wananchi fursa ya kuwadhibu viongozi wa kisiasa(wa kuchaguliwa) kama wabunge na madiwani, itayotupa Muundo Sahihi wa Muungano(serikali 3), itayoruhusu matokeo ya uraisi kuhojiwa mahakamani, n.k.

Hivyo, Raisi Samia, tambua hii fursa sasa iko kwako na pengine kuna wenzako wanatamani ufeli katika hili ili usipate hiyo sifa na badala yake wanaomba waje waipate wao. Inawezekana kabisa hata Kikwete leo hii anajilaumu kwa kushindwa kuwapatia watanzania Katiba Mpya kwani alikuwa na hiyo nafasi na bahati mbaya akaipoteza.

Mhe, Raisi, infrasture na vitu vingine vya aina hiyo, vimejengwa na wakoloni na baadhi vimeendeea kujengwa na watangulizi wako, ila impact yake huwa ni ya muda tu na vikishazoeleka, vinaonekana ni vya kawaida tu na watu kutaka vijengwe vingine vya kisasa zaidi au viboreshwe na hivyo kufanya vya awali visionekane vyenye thamani tena(sio dhahabu).

Jiulize nani leo hii anamsifia au anamkumbuka Mkapa kwa kuanzisha Television ya Taifa(TVT enzi hizo), nani anamsifia au anamkumbuka Nyerere kwenye ujenzi wa Reli ya Tazara, nani anamkumbuka au kumsifia Mzee Mwinyi kwa ujenzi wa miundombinu ya barabara wakati wake, nani anamsifia au kumkumbuka Kikwete kwa ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma, n,k. Ukipata majibu, basi utajua hatima ya legacy ya kujenga Ikulu, bwawa la umeme, n.k. japo ni vya muhimu na tunavihitaji.

Kwa upande wa katiba mpya, hali ni tofauti kabisa kwani matunda ya katiba mpya ni ya kudumu na kukumbukwa siku zote. Kwa mfano, kila uchaguzi unapofanyika na watu wakahoji matokeo ya uraisi mahakamani, basi ujue watanzania watakukumbuka sana kwa kuwapa hiyo nafasi tofauti na ilivyo hivi sasa.

Watanzania wakipata katiba itayotibu tatizo la Muundo wa Muungano, utaiingia katika historia kubwa na ya kipekee tofauti na ya kukamilisha ujenzi wa Bwawa la Umeme huko mto Rufiji na miradi mingine mikubwa unayoendelea kuikamilisha.

Watanzania wakipata katiba itayopunguza madaraka ya Raisi na kuimarisha Mamlaka au Nguu ya Bunge na kuipa Mahakama uhuru wa kutosha,basi utambue utaheshimika na kukumbukwa na vizazi vingi vinavyokuja.

Hiyo ni mifano michache miongoni mwa mingi itayopatikana kama matunda ya katiba mpya.

Mhe Raisi, ukitaka kuingia katika kundi moja la watu kama kina Mandela, Martin Luther King, na wengineo ambao hawakujenga miundombinu katika nchi zao bali wanaheshimika dunia nzima kuliko wale walijenga miundombinu katika nchi hizo, basi wapatie watanzania Katiba Mpya na iliyo bora, nakuhakikishia utaingia katika historia ya nchi hii hata kama katiba hiyo itafanya wewe na chama chako mshindwe uchaguzi na kuondoka madarakani.

Raisi Samia jenga picha ya wewe kukabidhi madaraka kwa upinzani na katika hafla hiyo, ukachomekea maneno: "katiba mpya na bora, leo imewezesha wapinzania kuingia madarakani". Mhe, Sentesi hiyo moja tu inaweza kuja kunukuliwa mara nyingi sana huko mbeleni na kufanya ukumbukwe daima kila itapokuwa inanukuliwa na hakika itakupa faraja kubwa sana katika maisha yako hapa duniani hata kama utakuwa umepoteza uchaguzi wewe na chama chako.

Mhe. Raisi, miaka hamsini ijayo, Ikulu ya Chamwino haitakuwa habari tena, ila katiba mpya na bora itaendelea kukuweka kwenye ramani.

Mzee Warioba, kwa kutupatia tu Rasimu ya Katiba Mpya, leo hii tayari ni living example ya hiki ninachokisema.

Madaraka ni ya kupita, ila namna gani umetumia madaraka yako, hii ndio legacy na legacy ni ya kudumu. So, it is upon you to choose between what is temporary and what is permanent.
Katiba mpya imewapa nini wakenya
 
Back
Top Bottom