Crucifix
JF-Expert Member
- Feb 20, 2011
- 1,651
- 588
Nimesikitishwa na kauli za wazanzibari (kupitia kwa wabunge wao) na wengine humu JF wanaolazimisha kuwa rais wa Zanzibar na rais wa Tanzania wawe na mamlaka sawa katika suala la katiba na mustakabali wa nchi yetu.
Urais wa Tanzania sio Jakaya Kikwete. Leo hii JK akifa, ni wazi kuwa Mohamed Gharib Bilal atapishwa kuwa rais wa Tanzania. Kwa hiyo, itawezekanaje Bilal na Shein wakae kuzungumzia mustabali wa Kigoma, Mwanza, Mbeya, Bukoba, Mtwara, Tanga, nk? Kauli za wabunge hawa zinamfanya JK kuonekana kuwa ni rais wa Tanganyika na si rais wa Muungano.
Ni ‘ujuha' kwa rais wa Tanzania kutembelea Zanzibar kama mgeni wa kitaifa wakati yupo katika nchi anayoitawala! Rais huyo huyo anapokwenda Dodoma haendi kama mgeni bali mkuu wan chi yake. RAIS WA TANZANIA SIO RAIS WA TANGANYIKA. Kwa kuongezea tu, sasa ifikie wakati kwa wabunge kukaa kama ‘bunge la Tanganyika' na kuwatoa nje wabunge wa Zanzibar pale yanapojadiliwa mambo yasiyowahusu wa-zenji.
Kama watawaonea aibu wabunge wa Zanzibar pale Dodoma, basi wafufue bunge la Tanganyika pale Karimjee (kwa masaburi) ili Tanganyika iweze kuongea kama Tanganyika bila mwangwi wa visiwa vya Unguja na Pemba. Mungu ibariki Tanganyika