Rais wa Tanzania sio rais wa Tanganyika (Wazanzibar hamjui hili?)

Pasco siafikiani na wewe. Ninaangazia 'angles' zote mkuu. Ni kwa kujiamini huko ndio maana tumejiachia bila tahadhari kwa kudhani kuwa siku zote rais wa muungano hatatoka znz kupitia uchaguzi na eti bara tutatawala siku zote kwa uwingi wetu. Vipi rais akifa akiwa madarakani na katiba inatamka makamu ndiye anachua urais? Bado utasema tena kuwa chance ya mwisho ilikuwa kwa Dr Salim? Au kuna mkakati wa rais na makamu wote kutoka Tanganyika?
Crucifix,
Rais akifa katiba inaitisha makamu rais ashike madaraka nadhani kwa siku tisini. Baada ya hapo uchaguzi unafanyika. Na uwezekano unaweza kuwa mkubwa kwamba makamu rais (Mzanzibari) hatapata kura za Busegwe.
 
Hakuna kitu kwamba rais wa muunganano atoke Zenj. Ni bara tu tutaendelea kujiwekea madude yetu....zenj ni midebwedo sana.
 
Ndugu kasome tena katiba. Moi aliukwaa urais baada ya Kenyatta kufa. Goodluck Jonathan wa Nigeria aliukwaa urais baada ya rais kufa. Baada ya Keneddy wa US kuuliwa, Lyndon B. Johnson aliukwaa urais. Hivyo usije ukastaajabu kumwita mh Bilal rais wako
 
Mzenji akiwa prezdaa wa muungano taifa litakuwa la vilaza sana kwa kuwa atatilia mkazo watoto wakasome quran kuliko elim dunia, baada ya hapo watalazisha tuwe wanachama wa oic, mzenji yeyote hafai hata kidogo kuwa rais wa muungano
 
Kwani kuna Serikali ya Tanganyika.?

Nani rais wake?
serikali ya Tanganyika ilikuwepo ila kwa sasa haipo lakini ipo serilkali ya jamhuri ya muungano ya Tanzania ambapo inatawala Taifa la watanzania lakini ni vizuri uelewe kuwa hakuna taifa la zanzibar wala tanganyika ila kuna dola ya zanzibar kwa ajili ya wazanzibari tu, ni sawa kuwa na uchifu wa kabila fulani ndani ya nchi fulani wakawa na utaratibu wao wa kujitawala,kutatua matatizo na majukumu yao mbalimbali lakini kamwe hawaundi taifa na bado wanabaki kuwa chini ya serikali ya nchi husika i.e afrika kusini kuna uchifu wa wazulu lakini wanabaki kuwa ni raia wa afrika kusini na wanatawaliwa na serikali ya afrika kusini huku wakiendelea kutekeleza taratibu zao kimila,HAKUNA TAIFA LA ZANZIBAR KAMA AMBAVYO HAKUNA TAIFA LA TANGANYIKA BALI KUNA TAIFA LA TANZANIA LILITOKANA NA MUUNGANO WA HAYO MATAIFA MAWILI NA KWA MAANA HIYO WAZANZIBARI WASIJIDANGANYE KUWA KUNA TAIFA LA ZANZIBAR hata passport wanazopata haziandikwi uraia au utaifa wa zanzibar bali Tanzania.
 
Mzenji akiwa prezdaa wa muungano taifa litakuwa la vilaza sana kwa kuwa atatilia mkazo watoto wakasome quran kuliko elim dunia, baada ya hapo watalazisha tuwe wanachama wa oic, mzenji yeyote hafai hata kidogo kuwa rais wa muungano

Sipingi mzanzibari kuwa rais wa muungano......lakini kama akiwa, nani atasimamia mambo ya Tanganyika? Maana sasa kuna mtanzania bara JK, rais wa Tanzania na hatujui maslahi ya Tanganyika ndani ya muungano yanashughulikiwa na nani. Na huyu Pinda ni waziri mkuu wa Tanzania au Tanzania bara? simsikii akikohoa kule zenji ati!
 
Tatizo la watu wa bara wengi wao hawaijui historia ya Zanzibar na Tanganyika ndio maana munapata shida na zanzibar iwe isiwe rudini katika historia ya kweli usibishe kwa sababu tu munabisha ila bisheni kwa hoja na semeni ukweli munalazimisha muungano ambao wazanzibar hawautaki hilo ndio la kweli kwa nini munaingangania zanzibar wakati wenyewe hawataki au kuna agenda gani ? au mumetumwana wakoloni wenu kwamba musiiachie zanzibar?
 
hayo matusi yenu ndio yanayowafanya wazanzibari wauchukie muungano maana hakuna munaloliandika zaidi ya matusi mbona wao wanaongea bila ya kutukana
 
Hakuna kitu kwamba rais wa muunganano atoke Zenj. Ni bara tu tutaendelea kujiwekea madude yetu....zenj ni midebwedo sana.

Angalia unachoongea huna hata hekma wala busara ni matusi na kejeli kwa wazanzibar kisa unajuwa kutumia computer andika vitu vya maana ili kila mtu aweze kuchanganyua sio kutukana kama huna la kuongea kaa kimya usome wenzio wameandika nini na ujifunze usitujazie humu pages kwa kuandika kejeli hunahekma wala busara halafu angalia pia na umri wako na ulichoandika
 
asante mkuu! watu wengine sijui wanafikiria na nini....?
 
Serikali tatu hapana! Kama tumeungana lazima kiwe kitu kimoja,kama mke na mume wanakuwa kitu kimoja kwanin isiwe Tanganyika na Zanzibar? Kama ni muungano iwe Tanzania moja Zanzibar iwe kanda kama ilivyo kanda ya ziwa na mikoa yake.!
Hizi hoja nyingine hazina mashiko kabisa.

Wewe nani alikwambia muungano wa nchi ni sawa na ndoa? Hata kwenye ndoa nani alikudanganya kuwa watu wawili wanakuwa kitu kimoja wakioana? Sasa kama hiyo ndiyo mantiki huu ushirikiano wa afrika mashariki utaufananisha na ndoa ya mitala?

Aliyeuloga huu muungano ni Nyerere pale alipoamua kuunganisha vyeo viwili akachukua yeye. Yaani uraisi wa Tanganyika na urais wa Tanzania. Hakutaka kuachia urais wa Tanganyika kwa sababu ulimpa nguvu ya dola.
 
Pasco siafikiani na wewe. Ninaangazia 'angles' zote mkuu. Ni kwa kujiamini huko ndio maana tumejiachia bila tahadhari kwa kudhani kuwa siku zote rais wa muungano hatatoka znz kupitia uchaguzi na eti bara tutatawala siku zote kwa uwingi wetu. Vipi rais akifa akiwa madarakani na katiba inatamka makamu ndiye anachua urais? Bado utasema tena kuwa chance ya mwisho ilikuwa kwa Dr Salim? Au kuna mkakati wa rais na makamu wote kutoka Tanganyika?
nilikuwa sijaliona hili. Ila ataongoza kwa mpito tu kama ilivyokuwa kwa jonathan wa nigeria.
 
Pasco siafikiani na wewe. Ninaangazia 'angles' zote mkuu. Ni kwa kujiamini huko ndio maana tumejiachia bila tahadhari kwa kudhani kuwa siku zote rais wa muungano hatatoka znz kupitia uchaguzi na eti bara tutatawala siku zote kwa uwingi wetu. Vipi rais akifa akiwa madarakani na katiba inatamka makamu ndiye anachua urais? Bado utasema tena kuwa chance ya mwisho ilikuwa kwa Dr Salim? Au kuna mkakati wa rais na makamu wote kutoka Tanganyika?
Crucifix, kwa hili nakubaliana na wewe asilimia 100%, mimi nilimaanisha chance ya wabara kumchagua Mzanzibari kwenye sanduku la kura.

Ila hoja yako ni ya msingi, muungano wetu una matatizo ya msingi toka kwenye structure, kinachofanyika sio kutatua tatizo, bali kuahirisha au kufunika viraka.

Kama ni kweli Tanganyika na Zanzibar zimeungana zikaunda Tanzania, then rais wa JMT ndiye rais wa nchi, lakini ni ajabu akiingia Zanzibar, he is nothing, kama ilivyo kwa rais wa Zanzibar ndani ya structure ya muungano, he is nothing!.

Ni Nyerere pekee aliweza kumnadi Mwinyi kumpokea urais na Watanzania wakamchagua, baada ya Dr. Salim kupigwa zengwe na mtandao wa JK, that is the end kwa Mzanzibari kuchaguliwa rais wa Tanzania. Wataishia kulalamika tuu mke kulia wivu kwenye ndoa za mitala!. Kama JK ambaye ni mbara kachaguliwa na 42% ya waliojindikisha kupiga kura, huyo Mzanzibari, atachagulikaje?.
 
WaDanganyika acheni kulala mnapaswa kudai Utaifa wenu na Rais wenu kama Zanzibar.

Laini naona ipo namna kwanini waTanganika hawaitaki Serikali na nchi yao ya Tanganyika kama ilivyo Zanzibar? WaZnz wanawabembeleza sana waanzisha serikali ya Tanganyika ndani a muungano lakini hawataki ndipo tunapojiuliza kuna nini hapo? Je kuna manufaa gani kwa TNG?
 
Na ndio maana imefika wakati eti wanadai rais wa Tanzania awe na hadhi sawa na yule wa Zanzibar, kwa maana hiyo akichaguliwa rais mzanzibari kuongoza Tanzania ndio kusema watanganyika tutakuwa 'koloni' la Zanzibar. RAIS WA TANZANIA SIO RAIS WA TANGANYIKA
kwahiyo hivi sasa Zanzibar ni koloni la Tanganyika?
 
Hakuna kitu kwamba rais wa muunganano atoke Zenj. Ni bara tu tutaendelea kujiwekea madude yetu....zenj ni midebwedo sana.
Mnajidanganya sana tu. Kwa minyukano inayoendelea huku bara uwezekano wa kuwa na Rais wa JMT kutoka Zanzibar 2015 ni mkubwa tu. Vinginevyo niambieni sasa nani huku bara anaonekana atamrithi JK?
 
Wasichokijua Wazanzibari kwa sasa ni kuwa wana serikali ambayo haitambuliwi na KATIBA ya JMT. Kama ni halali au sio hilo nawaachia akina Lissu.
 
wewe koma kabisa kufananisha muungano wa nnchi hizi kama vile ndoa hii sio ndoa na wala haiwezi kuwa ndoa milele kwa huwezi kusema ni nani kaolewa sasa hapo au nani ni mume wa mwenzake
Zanzibar atakuwa mke alafu Taganyika ni mume. AHHAAAAaaaaaaaahahahahahahahaha mawazo mengine bwana.
 
buddy you really sound like a great thinker! ni vizuri zaidi kama wazanzibar wakaangalia hata japo eneo lao kwa kilometa za mraba kabla ya kuicrash hoja yako.
 
Back
Top Bottom