Pumzika kwa amani mzee Mwinyi. Katika utawala wako ulitufanyia mengi katika taifa ikiwemo swala la kuifungua nchi, kutuepusha kuvaa midabwada, chakacha, kula ugali wa dona na mbilimbi, kuogea majani ya mpapai nk.

Mazishi yatafanyika kijijini kwao Mkuranga au Zanzibar?
 
Rais wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi afariki dunia.

Taarifa hii imetolewa usiku huu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

View attachment 2920484
Pole sana kwa familia na watanzania kwa ujumla kwa kumpoteza mpendwa wetu. Huyu ni rais ambaye wakati wa uongozi wake hakuwahi kuwa na kikundi cha watu wasiojulikana wanaopoteza roho za watu. Pumzika kwa amani mzee ruksa, umepigana vita vizuri mwnedo umeumaliza. Mwanga wa milele eeh Bwana umuangazie.
 
Tunamsubiri kwa hamu kubwa sana kumsikia mama yetu mpendwa kipenzi cha watanzania mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita, nyota ya matumaini, nuru ya wanyonge na jemedari wetu mpambanaji ambaye wakati wote yupo vitani katika kuwapigania Watanzania wanyonge kuhakikisha kuwa wanainuka kiuchumi na kupata tabasamu katika mioyo yetu.

Watanzania tuna imani kubwa sana na Rais samia,tunampenda,kumuamini na tuna matarajio makubwa sana na uongozi wake.kakata kiu yetu iliyokuwa katika mioyo yetu.katupatia kila kitu tulichohitaji,kagusa maisha yetu na kuleta matumaini katika kutimiza ndoto zetu watanzania.
Ila tupo msibani sasa. Hayo mengine yanaweza kusubiri.
 
Duh! Kazi kwelikweli
 
Back
Top Bottom