Rais wa Awamu ya Pili, Mzee Ali Hassan Mwinyi alazwa kwa maradhi ya kifua

Makumbele

Member
May 9, 2009
65
390
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mzee Ali Hassan Mwinyi amepelekwa hospitali akiugua maradhi ya kifua. Anaendelea kupata matibabu chini ya uangalizi wa karibu wa madaktari.

Kutokana na ushauri wa madaktari wake, familia imeona ni vyema apate faragha akiwa anapatiwa matibabu. Hivyo Familia inaiomba jamii kumkumbuka kwenye Dua, Sala, na Maombi.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu amjaalie shifaa ya haraka Mzee wetu pamoja na wagonjwa wengine wote wanaokabiliwa na maradhi mbali mbali.

Abdullah Ali Mwinyi
Msemaji wa Familia

Pia soma: Breaking News: - Rais wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi afariki dunia
 
Ndugu zangu Watanzania,

Ndugu Abdullal Alli Mwinyi Msemaji wa familia ya Rais mstaafu wa awamu ya pili mzee Mwinyi ameiomba jamii kumkumbuka mzee wetu na Rais wetu mstaafu kwa sara,dua na maombi.

Ambapo amepelekwa hospitalini kutokana na maradhi ya kifua na kuendelea kupatiwa matibabu chini ya uangalizi wa karibu wa madaktari wake.

Kwa hiyo watanzania wenzangu tumuombee mzee wetu na Rais wetu mstaafu ambaye ndiye muasisi wa mageuzi ya kisiasa hapa nchini.

Ni wakati wake ndio mfumo wa vyama vingi uliingia nchini na demokrasia kuanza kuchukua nafasi yake na kutoa nafasi ya watu kuzungumza kwa uhuru bila shida. Ni wakati wake ambapo mabadiliko makubwa sana ya kiuchumi yalifanyika katika kuwaondoa watanzania katika dimbwi la umaskini uliotopea.

Kwa waliosahau au kutoelewa ni kuwa mzee wetu huyu hapo mwakani panapo majaliwa ya Mwenyezi Mungu atatimiza miaka mia moja yaani karne moja.jambo ambalo kiukweli kufikisha umri huo hapa Duniani ni lazima umshukuru Mungu na kusema imekuwa hivyo kwa neema tu ya Mungu.
 
Jamani Rais ni mali ya wananchi, sasa faragha inatoka wapiii? Km kuna lolote tuambiwe ukweli mapemaa.
Nadhani taarifa waliyotoa inatosha kabisa. Tena wamefanya uungwana sana maana Magufuli alikuwa rais lakini hawakutoa taarifa yoyote. Privacy wanayotaka ni katika kumuuguza, watu wasiwachokonoe kwa kuwazongazonga. Augue pole.
 
Back
Top Bottom