Rais Samia usimtumbue Mkugenzi wa Mamlaka ya viwanja vya ndege; apongezwe kwa kusimamia Reciprocity kwa manufaa mapana ya biashara zetu

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
877
4,106
Kuna wanaharakati wanaanza kushinikiza Mkurugenzi wa Mamlaka ya viwanja vya ndege aondolewe. Kumwondoa nikudhoofisha kujiamini kwa wateule wa Mhe. Rais.

Barua ya kusitishwa kwa safari za ndege za KQ iliyotolewa na Bwana Johari imeeleza mambo makuu mawili ya msingi.

1. Kukiukwa kwa makubaliano
2. Kutokuwepo kwa reciprocity

Nimesoma pia barua ya Kenya, hakuna Sehemu wakenya wamepingana na tuhuma zilizotolewa na Tanzania. Means wao wenyewe walikuwa wanafanya haya makusudi wakiamini hakuna hatua zitachukuliwa na Tanzania.

Hatua zimechukuliwa wameomba poo na sasa wanarudi mezani. Swali, Waziri wa mambo ya Nje wa Kenya alikuwa anasubiri nini siku zote? Rais wa Kenya alikuwa anasubiri nini kuchukua hatua ?

Hizi ni dharau kwa nchi yetu na sasa tunahitaji misuli kama ya Johari ili tuheshimiane. Tunahitaji kuwa na wafanyabishara wenye kiburi pale wanapokuwa ndani ya sheria.

Hongera sana mkurugenzi; hata Wakikutumbua sisi tunaelewa maana na kulinda sovereignity tutakukumbuka. Natambua nyuma yako viko vikao rasmi vilivyofikia haya maamuzi. Wewe ni askari wa mstari wa mbele....pambano. nikukumbushe kuwa " sometimes wanasiasa upenda sana kutoa maamuzi ya kisiasa lakini wewe ni mtumishi wa umma". Una mkataba mrefu sana juu ya nchi yetu

Tunahitaji watoa maamuzi kama hawa ili nchi iendeleee, tuseme no kwenye dharau zakimataifa.
 
well said hapo kidogo heshima itapatikana pia hawatakurupuka katika maamuzi mengine au yajayo.
 
Maamuzi kama yale mkurugenzi hawezi kujiamulia, ni lazima aliwahusisha mabosi wake, na kwa namna moja ama nyingine wako sahihi.​
 
Back
Top Bottom