Rais Samia, tafadhali pitia huku uokoe maisha ya mwananchi wako anaepambana kuokoa uhai wake

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Sep 9, 2020
6,968
12,435
Screenshot 2023-03-22 043021.png


Rais wetu, kwa heshima na taadhima napenda kutanguliza salam zangu za dhati kwako na kwa Watanzania wote, waliopo humu na wale wasiokuwepo humu nawasalimu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Rais Samia leo katika kuperuzi peruzi kwenye mitandao yetu ya kijamii ili kupata habari mbali mbali za ndani na nje ya nchi yetu, nilikumbana na habari moja ambayo ki ukweli imenisononesha na kuniumiza sana.

Habari hiyo inamhusu dada fulani wa Kitanzania ambae hapo zamani inasemekana aliwahi kuwa msanii (sijui ni wa bongo movie au mziki) kwa jina anaitwa Hawa Hussein Ibrahim na jina lake la usanii ni "Karine".

Dada huyu alikuwa anahojiwa na sister fulani ambae ana chanel yake inayoitwa "Nitetee" huko YouTube. Bahati mbaya jina la huyo sister limenitoka. Ila ki ukweli huyu dada anaonekana anateseka sana kutokana na utumbo wake kutoboka, hivyo uchafu unaotakiwa kutoka nje kupitia njia yake ya asili hutokea katika tundu hilo na kusambaa katika maeneo mengine ya tumbo, hivyo kumsababishia maumivu makali na matesa makubwa katika maisha yake.

Anasema kwamba ugonjwa huu umemsumbua kwa muda mrefu sana, na ameshafanya oparation zaidi ya 15, lakini tatizo bado liko pale pale.

Kwahiyo alikuwa akipewa michango na watu mbali mbali ili kumsaidia kuokoa uhai wake, lakini kwa vile hali yake au oparation zake hazionekani kumpa afueni basi hata wachangiaji nao wameonekana kukata tamaa, na hivyo kumuweka katika wakati mgumu binti huyo na familia yake.

Familia yake imeshapoteza pesa nyingi kumpambania bila mafanikio. Kwahiyo nakuomba Mh. Rais kama ikikupendeza uamuru serikali yako iangalie namna ya kumsaidia binti yule ili kuokoa uhai wake yeye na hata wengine wenye maradhi ya aina mbali mbali ambao hawana uwezo wa kujitibia ili kuokoa uhai wao.

Tunatambua huruma yako, upendo wako na mchango wako kwa wananchi wako ni mkubwa mno, na ndio maana umekuwa mstari wa mbele kuwashika mkono na kuwafariji wale wote wanaohitaji faraja. Tafadhali tupia jicho na huku kwengine ili kumuepusha mwananchi wako na umauti wa mateso.

Natambua kufa kupo na kila mmoja wetu atakufa, lakini pale inapopatikana njia ya kujiepusha na vifo vya maradhi basi tuitumie kuokoa maisha na pia kuwaondolea watu maumivu yasiokwisha kutokana na maradhi mbali mbali.

Kama Rais hajafanikiwa kuuona ujumbe huu, basi kwa wale walio karibu nae wamfikishie ujumbe huu ili kuokoa uhai wa dada yetu, na ndugu zetu wengine.

Umoja ni Nguvu 💪 Utengano ni Udhaifu 🙏.
 
Back
Top Bottom