Watanzania panapotokea majanga tujali sana kuokoa nafsi zetu kuliko mali; uhai haitafutwi ila Mali zinatafutwa. Poleni kwa mafuriko

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
879
4,125
Nimeangalia clip mbalimbali zinazosambaa kuhusu hali ya majanga yanayotokana na mvua nchini

Ukiangalia clip na kuangalia maneno yanayotolewa na wahanga yanalenga zaidi kuzifuatilia mali na kusahau uhai wao. Nimeona watu wanasikitika kupoteza nyumba lakini wanaporekodiwa wanakuwa bado wapo kwenye mkondo wa mafuriko.

Wapo watu wameonekana wanakimbilia Kuokoa magari , vyombo na mifugo bila kuchukua tahadhari. Matokeo yake tumeona baadhi ya wananchi wanakufa kwa sababu tu walikuwa busy kukusanya mali kuliko kumshukuru Mungu kwa uhai.

Nimeona mtu mmoja anasema gari yangu nyeupe iko pale, gari yangu nyeusi ipo pale lakini mtu huyu amekaa mazingira yale yale ya mafuriko na maji mengi kiasi kwamba mvua ikiongezeka inamchukua yeye. Haya ni maono hafifu kuhusu majanga

Pamoja na kwamba tunapenda mali zetu tujikite zaidi kulinda nafsi zetu na watoto wetu. Usalama wetu kwanza mali baadaye. Let assume mvua ingekuzoa ungepata muda wakukimbilia magari?

Mwisho niwaombe Watanzania tubadili tabia katika kumiliki ardhi na kujenga. Serikali imeshindwa kutupanga basi tujipange wenyewe.....emergency exit ziwepo kwenye mitaa yetu ili tuokoke tunapopata majanga.

Once again poleni sana
 
We embu tuache, mwaka wetu huu tusiokua na magari na siye tumiliki. Sio kila siku tupande boda. Nishajiokotea vits langu, hapa nasubiri v8 🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom