Rais Samia: Suala la Katiba hakuna anayelikataa. Si muda mrefu nitatangaza hiyo kamati kwa kushauriana na vyama vyote vya siasa

kalacha mateo

Senior Member
Sep 27, 2021
118
237
Katika hotuba ya Rais Samia Suluhu kwenye kongamano la siku ya wanawake duniani ambalo limefanyika Moshi, Kilimanjaro na kuandalia na wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) amesema hakuna ambaye anakataa suala la katiba mpya hata chama chake kiko tayari kwa ajili ya katiba mpya.

"Suala la katiba hakuna anayelikataa, hata chama changu kimesema twende kwenye mabadiliko ya katiba. Hakuna anayelikataa lakini mdogo wangu Aikaeli anataka kasema juzi leo lifanyike. Mambo ni mengi ndani ya nchi hii lakini niwaahidi si muda mrefu nitatangaza hiyo kamati kwa kushauriana na vyama vyote vya siasa ili wakanze kazi."-
Rais Samia Suluhu

FqshewQXgAI4l8v
 
Hili la Katiba mpya mama hata ukikopa Vicoba kakope tu tutalipa.
 
Wananchi wana njaa wanasiasa wanalilia katiba mpya.

Sasa sijui tuanze na lipi??
 
Rais Samia Suluhu anasema mchakato wa katiba mpya unaendelea hiki ni kitu ambacho wapinzani na watanzania wengi walitamani kukisikia kweli Samia amedhamiria kuijenga Tanzania mpya.

Amesema sio CHADEMA tu hata Chama cha mapinduzi pia kinataka katiba mpya.

Nukuu "Swala katiba hakuna anayekataa hata chama changu hakuna anayekataa, na muda si mrefu tutatangaza kamati ambayo itashughulikia jambo hilo"
 
Yaani chadema sjui akili zenu uwa zinafanya kazi muda huo huo alafu zinazima,Kwani kikwete alisemaje kuhusu hiyo katiba na kilitokea nini?,MAGU yeye sababu ya ubishi na ubabe wake alitamka wazi huo muda wa kupoteza na hela za kuchezea hakuna.

Leo mama kasema analifanyia kazi yeye na chama chake na litapita kama lilivyopita kwa watangulizi wake.

Halafu Naomba kukuuliza swali hivi Baba mwenye nyumba anaweza tunga sheria ili mpangaji wake awe na haki kuliko yeye alafu ampindue na achukue nyumba yake na mke wake awe wa kwake,uliona wapi?
 
Yaani chadema sjui akili zenu uwa zinafanya kazi muda huo huo alafu zinazima,Kwani kikwete alisemaje kuhusu hiyo katiba na kilitokea nini...
Unachotakiwa kujua ni kwamba huu ni utawala wa Rais Samia Suluhu na anafanya kila kitu kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu kwaiyo kama katiba mpya itasaidia kuleta maendeleo Tanzania lazima itabadilishwa maana kipaumbele cha mama ni kuijenga Tanzania mpya kwaiyo tuendelee kumuombea Rais Samia Suluhu miaka mingi zaidi ili afanikishe kujenga Tanzania mpya
 
Utawala wa kwake kivipi, yeye yupo kwa mujibu wa katiba ila kuna watu wanamwambia cha kufanya.

Haya nambie unadhani chadema kwann wanalalamikia katiba mpya tena kila wakishashindwa uchaguzi?

Najua hauwezi kuwa na jibu ya ili swali, ni kwamba wao wanataka kibadilishwe kile kipengere tu cha CHA TUME HURU ya uchaguzi wakiamini kuwa kikibadilishwa hicho wanaweza shinda uchaguzi na wakapata dola/wakawa madarakani.

Cha kushangaza wao tangia wametengeneza KATIBA ya chama chao hawajawai badilisha chochote mle, KATIBA ya kwao ipo kama msaafuu hakuna kuguswaaaaaa.
 
mbulula ni mbulula tu ndio maana kina kitila mkumbo wanawambia bodaboda ni kaz nzuri huku watoto wao wakifanya kaz BOT na kwa hizo akili zenu mtazeeka na huo ujinga.
 
Back
Top Bottom