Mpap Ndabhit
JF-Expert Member
- Jan 15, 2014
- 237
- 239
Wananchi wa Sae mpya jijini Mbeya wanataka kubomolewa nyumba zao kwa maonevu makubwa. Awali waziri Lukuvi ALIKUJA Kwa Wananchi na kusema umemtuma kurejesha eneo lao ambalo TARI Kwa miaka zaidi ya miaka 40 walilitwaa bila kulipa fidia.
Clip hiyo IPO wakati waziri anakabidhi mbele ya mkuu wa mkoa, mheshimiwa Tulia, spika wa bunge mwenyekiti wa CCM wote, kamishina wa ardhi alikuwepo. Kwa kauli ya waziri Wananchi wakaanza kujenga,na tayari wameanza kuishi katika makazi hayo.
Wakati huu waziri Silaa naye ana maelekezo mapya ya Rais kwamba Hilo eneo ni la kilimo wananchi wabomoe nyumba zao, bila hata kuwasikiliza, wananchi wanaambiwa ni wavamizi kwenye eneo la kilimo.
Mheshimiwa Rais imebaki kauli yako wewe tu. Ikikupendeza Wananchi wanaomba kuachiwa maeneo hayo ambavyo TARi iliyachukulia hati bila kutoa fidia na Wala hawajawahi kuyatumia.