Mpap Ndabhit
JF-Expert Member
- Jan 15, 2014
- 237
- 239
Kama siyo wote baadhi ya mawaziri na hata wakuu wa mikoa na WA wilaya utawasikia wanapotekeleza majukumu Yao hujinasibu kwamba mheshimiwa Rais amewapa agizo la kutekeleza jambo Fulani.
Waziri wa ardhi mheshimiwa Silaa alipokuwa mkoani Katavi katika ziara ya katibu mkuu wa CCM Chongolo alisema Rais amemtuma kuumaliza mgogoro wa ardhi kati ya wananchi 400 na chuo Cha kilimo Katavi. Na kwamba hati ya ardhi ya chuo hicho irekebishwe Ili wananchi waendeleze ardhi Yao.
Kauli kama hiyo iliwahi kutolewa na waziri wa ardhi mheshimiwa William Lukuvi kwamba Rais Samia amemtuma kuumaliza mgogoro wa ardhi kati ya wananchi wa Sae mpya (maarufu mtaa wa LUKUVI) na chuo Cha kilimo Cha Uyole. Wananchi Kwa Kasi baada ya kauli wakaanza kujenga Ili kuendeleza eneo lao.
Ajabu akaja mkuu wa wilaya Mbeya na kauli nyingine kwamba Rais amemtuma kuwaondoa wananchi eneo Hilo Kwa matumizi ya serikali na kwamba watalipwa fidia.
Waziri wa kilimo Bashe naye katika Nane Nane anawachongea wananchi Kwa Rais kwamba wananchi wamevamia eneo la chuo Cha kilimo. Ashukuriwe Mungu Samia ana akili sana! Akaagiza viongozi washughulikie mgogoro huo bila kuleta taharuki Kwa Wananchi.
Ndiyo najiuliza hivi hawa mawaziri kweli wanatumwa na Rais au wanatudanganya Ili tuwaamini jambo lisilo la kweli?