Rais Samia safisha wabunge wa CCM 2025

Kanyunyu

JF-Expert Member
May 2, 2012
335
495
Mheshimiwa Rais Samia Suluhu tunakuomba usafishe genge la wabunge wa mwendazake aliowajaza Bungeni mwaka 2020 kwa ajili ya kazi ya kubadili katiba Ili aweze kutawala milele.

Magufuli aliingiza Bungeni mamluki wengi sana wa idara ya usalama wa taifa kwenda kudhibiti wabunge kuhusu mkakati wa kubadili katiba kuondoa ukomo wa miaka kumi Ili Magufuli aendelee kuongoza anavyotaka.

Katika mkakati huo wa kubadili katiba ulipangwa ifikapo mwaka 2023 ungeandaliwa muswada wa mabadiliko ya katiba kuondoa ukomo wa miaka kumi, na tayari spika Job Ndugai aliandaliwa kusimamia ajenda hiyo kikakamilifu na ingepitishwa kwa kishindo, bahati mbaya sana Mungu nae ana mipango yake kikatokea Kifo Cha mwendazake mwaka 2021.

Wabunge wengi waliopo Bungeni sasa ni zao la dhuluma na mipango ovu dhidi ya nchi yetu, wengi hawakushinda kwenye Sanduku la kura kuanzia ndani ya CCM na kwenye uchaguzi Mkuu.

Magufuli alilazimisha wabunge aliowataka na hakutaka wabunge wa upinzani kwenda kupinga mpango wake wa kubadili katiba ya nchi Ili aongoze anavyotaka.

Mfano ndani ya CCM waliachwa washindi wa kura za maoni na kuchukuliwa watu waliopata kura chache kabisa na kuteuliwa kuwa wagombea wa CCM, mfano majimbo ya Kibaha Vijijini, Muheza , Tunduma , Shinyanga mjini n.k.

Wabunge wa upinzani walioshinda hawakutangazwa kwasababu Magufuli alitoa amri ya moto kwamba hakuna kutangaza Mbunge wa upinzani.

Mama safisha uharo wa Magufuli wapatikane wabunge wa zao la haki Ili tufunge kabisa kurasa za mwendazake.
 
Aanze na mafisadi Kama Makamba Juzi tu katia 120M mfukoni kiujanja sana Alafu kule Norway zaidi ya Bilion imetumika kiujanja kanajiweka kimkakati kifedha Kwa mwaka 2030

Mtu asitolewe kisa ni team fulan bali Kwa uadilifu Au utovu wa nidhamu!!


Britanicca
 
Kesi ya 'ngedere' kwenda kwa........................................ 🤣
Ila kiukweli karibu 80% ya wabunge wote ni zao la udhulumati wa yule kichaa!
 
Mheshimiwa Rais Samia Suluhu tunakuomba usafishe genge la wabunge wa mwendazake aliowajaza Bungeni mwaka 2020 kwa ajili ya kazi ya kubadili katiba Ili aweze kutawala milele. Magufuli aliingiza Bungeni mamluki wengi sana wa idara ya usalama wa taifa kwenda kudhibiti wabunge kuhusu mkakati wa kubadili katiba kuondoa ukomo wa miaka kumi Ili Magufuli aendelee kuongoza anavyotaka .

Katika mkakati huo wa kubadili katiba ulipangwa ifikapo mwaka 2023 ungeandaliwa muswada wa mabadiliko ya katiba kuondoa ukomo wa miaka kumi, na tayari spika Job Ndugai aliandaliwa kusimamia ajenda hiyo kikakamilifu na ingepitishwa kwa kishindo, bahati mbaya sana Mungu nae ana mipango yake kikatokea Kifo Cha mwendazake mwaka 2021 .

Wabunge wengi waliopo Bungeni sasa ni zao la dhuluma na mipango ovu dhidi ya nchi yetu, wengi hawakushinda kwenye Sanduku la kura kuanzia ndani ya CCM na kwenye uchaguzi Mkuu . Magufuli alilazimisha wabunge aliowataka na hakutaka wabunge wa upinzani kwenda kupinga mpango wake wa kubadili katiba ya nchi Ili aongoze anavyotaka .

Mfano ndani ya CCM waliachwa washindi wa kura za maoni na kuchukuliwa watu waliopata kura chache kabisa na kuteuliwa kuwa wagombea wa CCM , mfano majimbo ya Kibaha Vijijini, Muheza , Tunduma , Shinyanga mjini n.k .

Wabunge wa upinzani walioshinda hawakutangazwa kwasababu Magufuli alitoa amri ya moto kwamba hakuna kutangaza Mbunge wa upinzani.

Mama safisha uharo wa Magufuli wapatikane wabunge wa zao la haki Ili tufunge kabisa kurasa za mwendazake.
Waondolewe wote kabisa akiwemo aliyekuwa Makamo wake.
 
Back
Top Bottom