Rais Samia atengua uteuzi wa Albert Chalamila RC Mwanza, Dkt. Batilda ateuliwa kuwa RC Tabora

Yaani Mkuu wa Mkoa anakuwa yeye ndiyo hakimu wa kuamua nani aishi na nani auwawe??

Utasema hakuna Mahakama?? Inashangaza hata huo uRC alipewa kwa vigezo vipi🙆🙆

Hata huyo PM atasingiziwa tu, lakini kwa kifupi Vetting yake itakuwa iligoma
Jamaa Kachongewa Na Pm Jana Kwenye Kikao Huko Mwanza
 
mambo ya kijinga huwa yanapenda kushikilia vichwa zaidi kuliko yenye tija.

Tugusie bajeti,
mie najikita katika faini za waendesha pikipiki na bajaji, kiufupi naona hizo faini ka hazijasaidia kitu na pili waendesha bodaboda wanajua sheria za barabarani na vyombo vya moto kiujumla ila wengi wanakiuka makusudi, mfano kuambiwa wasipakize mishikaki na wao wanapakiza, yani hilo la mishkaki hata mtoto wa miaka 12 anajua kuwa haitakiwi
Pili swala la kofia ngumu, kila dereva wa pikipiki anajua kuwa inampasa yeye na abiria wake kuvaa hiyo kufia ngumu ila hawavai kwasababu mbalimbali ila zaidi ya 90% ya hizo sababu zao hazina mashiko.

Swala la usalama kwa mtu mmoja mmoja na jamii nzima halihitaji mbwembwe ama siasa flani maana yale ni maisha ya mtu, kitendo cha kushusha hizo adhabu mie sioni kama itawasaidia ila itawafanya waone adhabu hiyo ni ndogo ambako kutawafanya wawe wazembe zaidi ambako kutakuwa na madhara zaidi.

Kitendo cha dereva wa pikipiki kuona adhabu ka ni ndogo na anaimudu kunaweza fanya wale wenye uelewa mdogo kuona ka ndo muda wa kufanya vile waonavyo inafaa kwao
 
Duuh, huyu siyo kiongozi...

Kiongozi kazi yake ni ku - PREVENT na ku - CONTROL uhalifu na wanaokamatwa ni kuacha sheria ivhukue mkondo wake...

RC unapohamasisha watu wajichukulie sheria mkononi kuua kila wanayedhani ni mhalifu, ni KOSA KUBWA, umeshindwa kazi ya uongozi wewe..!
Tena anakiri hadharani baada ya Kuua akajipongeza kwa kunywa Bia mbili,

Ingekuwa Nchi inayofata sheria huyo jamaa saivi alitakiwa awe mikononi mwa vyombo vya Uchunguzi. Usikute baada ya kuua akaamua kuitupa maiti huko maporini kupoteza ushahidi.
 
Safi sana mama wanapaswa watambue wewe huangalii kelele zisizo na tija kwa wananchi Bali unaangalia weledi na hekma kwa viongozi.
 
Mkuu angalia hata ule uzi wa bajeti haukuwa na wachangiaji hata kabla ya hii taarifa. Kwa ujumla taarifa za bunge ni kama watu wamezipuuza.
Siyo kwamba wamezipuuza ila watz wengi ni wajinga na wapumbavu!

Hivi unapuuzaje taarifa zitakazoathiri maisha yako kwa miaka zaidi ya 2 ijayo huku ukikomalia taarifa ya mtu mmoja ambae hana impact yeyote kwenye maisha yako? Kama si upumbavu ni nini hiki?
 
watanzania tunakamatwaga padogo sana, kodi ya simu na nyumba, mafuta zimeongezwa tutakuja kustuka tushakuwa na nundu
 
Ulevi wa Madaraka unazidi kuchika hatamu hapa nchini. Mkuu wa mkoa mzima anahimiza chuki na uwasi dhidi ya Raisi. Mkuu wa mkoa kweli anachochea Raisi wetu mpendwa azabwe kofi hadharani ? Kama yaliomkuta ule raisi wa Ufaransa kuzabwa kofi hadharani na mwananchi wakati akiwa ziarani? Huyu Challamila anatakiwa viombo vya usalama zikampumzishe kule Mirembe...
 
Mmemchulia huyu bwana mpaka kafurushwa....ila namuona ni Mtu mmoja poa tu.
 
Chalamila ni msema hovyo naturally.
Angalia mdomo ulivyomponza.
Kashindwa kumsoma boss wake.
Arudi darasani akapige chaki.
 
Back
Top Bottom