Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,558
- 41,078
Kwa sasa nchi nyingi za Afrika zisizo na uwezo wa kudhibiti ubora wa bidhaa au nchi ambazo zina mifumo ya hovyo ya kudhibiti ubora wa bidhaa, kama ilivyo Tanzania, wananchi wake wanaingia hasara ya mabilioni ya pesa baada ya kutapeliwa na Wachina kupitia bidhaa fake na zile zenye viwango duni vya ubora.
Inachofanya China, ni wizi na utapeli wa hali ya juu kupitia bidhaa. Wachina wanaiga mwonekano wa nje wa bidhaa zinazotengenezwa Ulaya, America, Japan na hata India, lakini ndani yake ni takataka. Bidhaa hizo duni, nyingi hazifikii hata 10% ya ubora wa bidhaa kama hiyo, zilizotengenezwa Ulaya, America au Japan.
Nchi za Ulaya hupata bidhaa zenye ubora toka China lakini zilizotengenezwa kwenye viwanda vyao walivyovijenga huko China. Vile viwanda vya Wachina wenyewe vinavyotengeneza bidhaa duni kabisa, soko la bidhaa zao ni Afrika. Maana nchi nyingi za Afrika, taasisi za kudhibiti ubora, kama ilivyo TBS, hazina maana yoyote, na wala hazina uwezo wowote wa kudhibiti ubora kutokana na uduni wa ujuzi wa watendaji wake, vifaa na nyenzo duni, rushwa na ufisadi.
Leo hii ni kawaida kabisa ukanunua machine iliyotengenezwa China, leo hii hii ikahitaji matengenezo kabla hujaitumia, na inaweza isifanye kazi moja kwa moja.
Kuna rafiki yangu aliagiza mitambo ya kiwanda toka China, alilipa $800,000, wiki ya kwanza ya majaribio, na Wachina wenyewe wakiwepo, mtambo uliharibika, na ilichukua wiki 5 kupata replacement ya part iliyoharibika. Lakini hata baada ya kupata hiyo replacement, mpaka leo, karibia kila wiki lazima kuwepo matengenezo.
Kuna rafiki yangu mwingine alinunua water pump, kuanza tu kuitumia, haikufanya kazi. Na haikufanya kazi moja kwa moja.
Mimi mwenyewe nilinunua generator ya umeme, ilifanya kazi masaa 2, ikashindwa kuendelea. Ikabidi nimrudishie muuzaji, muuzaji ikabidi anipe nyingine. Hiyo replacement ilifanya kazi siku 3, nayo ikaharibika. Lakini hivi karibuni nilinunua tairi 5 mpya za kutoka China, za gari kubwa, moja ikaanza kuvimba. Ilipofunguliwa, ikaonekana nyaya zake zimekatika, na ilikuwa ndiyo siku ya kwanza tangu zifungwe kwenye gari.
Hali ni hiyo hiyo kwa bidhaa nyingi za China. Huu nauita ni wizi kupitia bidhaa. China inaiua Afrika kiuchumi. Fikiria mtu ananunua kiatu sh 50,000, anavaa siku 3 au wiki 1, kiatu hakifai tena. Huu ni wizi. Nchi za Afrika ziungane kupinga wizi huu wa China kupitia bidhaa.
Fikiria uliyenunua kiatu kwa sh 70,000 toka China, akavaa kwa wiki moja tu. Hii ni wastani wa sh 10,000 kwa siku. Linganisha na mwenzako aliyenunua kiatu kilichotengenezwa Italy kwa sh 150,000 halafu kinadumu kwa miaka 5. Hii ni wastani wa 150,000 gawanya kwa 5×360; ni sawa na sh 83 kwa siku.
Katika mahusiano ya kibiashara kati ya Afrika na China, kwa kiasi kikuvwa China inazinyonya sana nchi za Afrika kwa kuzifanya nchi za Afrika kuwa dampo la bidhaa zake duni. Na mabilioni ya pesa toka Afrika yanaenda China kupitia hizi bidhaa takataka. Waulize wanaonunua malori mapya kabisa toka China, wanaanza matengenezo baada ya miaka mingapi. Utashangaa
OMBI: Pamoja na ughali wa bidhaa zinazotengenezwa na mataifa yenye tekinolojia ya juu kama Japan, Ulaya na America, tunawasihi sana Wafanyabiashara wa Tanzania, kuwepo na wale wanaoagiza bidhaa zenye ubora toka mataifa ya Ulaya, Japan na America. Ili wanunuzi wawe na machaguo. Wanaotaka kuendelea kuibiwa na Wachina, wanunue bidhaa hafifu za China, wanaothamini pesa na jasho lao, wanunue bidhaa zenye ubora zinazoendana na thamani ya pesa yao. Au pia wapatikane wafanyabiashara watakaonunua toka makampuni yaliyopo China yanayomilikiwa na makampuni ya mataifa ya Ulaya, America na Japan, maana Wachina wenyewe, walio wengi hawataki kununua bidhaa zinazotengenezwa na makampuni yaliyopo China yanayomilikiwa na Wachina, kwa sababu ya viwango duni vya ubora.
PIGA VITA WIZI WA WACHINA KUPITIA BIDHAA DUNI.