Rais Samia asema itungwe Sheria itakayotoa muongozo kuwashughulia viongozi wanaofanya majukumu ambayo sio yao

Nimefarijika na kufurahia sana wasilisho la leo la Tume ya Haki Jinai lilifanywa na Jaji Mkuu mstaafu Mh.Othman Chande.

Juu ya yote nimependezwa na mapendekezo yaliyotolewa na approach aliyotumia Mh.Rais kuyatafutia ufumbuzi.

Tendo zima na dhamira ya Mh.Rais ni ya kiutu na kibinadamu,maana walioko jela ni binadamu kama sisi,wanahitaji kuwajali,kuwapenda na kuwaheshimu pia...japo miaka mingi tumewasahau mno.

Wahusika tumeaswa,tubadili mitazamo/mindset,tabia na tamaduni zetu za kuenenda kama tume ilivyoshauri.

Wazo lililotolewa la kutumia tume ndogo kuandaa mpango wa utelekelezaji/Action Plan,kwa mapendekezo yote na kuanisha wahusika ni nani,time frame, budgetary requirements nk ni zuri zaidi.

Lakini nishauri pia hiyo hoja ya kuandika Concept Note ipewe kipaumbele zaidi,yaweza kusaidia kifedha na tukiinadi kwa wabia wetu wa haki za binadamu, demokrasia na utawala bora,ikiandikwa kwa weledi na viwango Bora na vya ushawishi murua,tunaweza kupata support kubwa zaidi toka kwa wenzetu maana kwao haya ni maeneo ya kimkakati na kiungwana kutuwezesha na huwa wanaguswa vyepesi na maeneo kama haya.
Tutangaze kandarasi kama wafanyavyo UNDP nk tupate wataalam wazuri watuandalie andiko zuri ili tulitembeze panapohusika.

I wish I would be given an opportunity to draft such a concept note...I would do it to my best talent to achieve the desired targets!
c28cd668779b4ce2857692396b8fe522.jpg
 
Hiki kiburi ni another level
Itungwe sheria ya wananchi kuwakamata watawala wabovu tuwaweke magereza mpaka further notice
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akipokea Taarifa rasmi ya Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuboresha Taasisi za Haki Jinai hapa Nchini, kutoka kwa Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman, Mwenyekiti wa Tume hiyo leo tarehe 15 Julai, 2023 katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete - Ikulu Dares Salaam.

Tume hiyo iliundwa Jan 2023 na kuanza kazi rasmi Feb 1 2023 lengo likiwa ni kutoa tathmini ya kina ya mfumo wa haki jinai nchini ili ije kufanyiwa maboresho kwenye taasisi za Jeshi la Polisi, Mahakama za Mashtaka, TAKUKURU, Jeshi la Magereza, Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya na Mahakama ya Tanzania, tume hiyo iliundwa watu 11 ikiongozwa na Jaji Mstaafu Mohamed Chande, kwa ujumla tume imegusa taasisi 18.




View attachment 2688953
Mwenyekiti Tume ya Haki Jinai - Jaji Mstaafu Mohamed Chande Othmani


Tume imebaini uwepo wa udhaifu mkubwa kwenye mnyororo wa mzima wa Haki Jinai kwenye; kubaini na kuzuia uhalifu, kukamata na kupeleka watuhumiwa vituo vya polisi, uchunguzi wa upelelezi wa makosa ya jinai, undikishaji mashtaka, usikilizaji wa mashauri ya jinai hamakamani, waliotiwa hatiani kutumikia kifungo gerezani au kupewa adhabu mbadala, na maisha ya wafungwa anapomaliza vifungo vyao na kurejea uraiani.

Maeneo Makuu 13 yanayohusu Mnyororo wa Haki Jinai na Mapendekezo yake, kichobainika na mapendekezo ya tume

1/ Kubaini na Kuzuia Uhalifu


Tume imebaini Taifa halina mkakati mahususi wa kuzuia na kubaini uhalifu, jambo linalochangia vyombo vya utekelezaji sheria kujikita zaidi kwenye kwenye ukamataji kutokea, baada ya kutokea kuliko kubaini na kuzuia uhalifu.

Mapendekezo
~ Mamlaka na Wadau wengine wa Haki Jinai waandae na kusimamamia utekelezaji wa Mkakati mahusushi wa kubaini na kuzuia uhalifu Crime Detection and Prevention Policy ikiwemo uhalifu wa Majini na wa Mitandaoni.

~ Mfumo wa nyumba 10 uhuishwe kisheria na kutambulika rasmi katika mfumo wa serikali za mitaa ili kurahisisha wananchi kutambuana kwa lengo la kuwezesha mikakati ya kuzuia uhalifu kuwa endelevu.

~ Mfumo wa huduma za kijamii na kibiashara zifungamanishane na mfumo wa utambuzi w usajili za makazi, RITA na NIDA ili kila mwnanchi awe na namba moja ya utambuzi kwa maisha yake yote.

2/ Ukamataji wa Watuhumiwa
Vyombo vyenye mamlaka ya ukamataji mara kadhaa hutumia nguvu kupita kiasi na kusababisha mateso kwa watuhuimiwa.

Uwepo wa taasisi nyingi zenye mamlaka ya kukamata, ziznazoidhinishiwa kuwa na mahabusu na hivyo kusababisha ugumu kwa wananchi kutambua taasisi ipi inakamata watu, na mahabusu nyingine hazijulikani zilipo.

Mapendekezo
~ Taasisi zenye mamlaka ya ya kukamata watuhumiwa zitekeleze hayo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi na maabusu za jeshi la polisi pekee ndio zitumike kuhifadhi watuhumiwa wa makosa yote ya jinai waliokamatwa.

3/ Watuhumiwa kutofikishwa mahakami ndani ya muda

Kuna malalamiko mengi ya muda mrefu kutoka kwa wananchi na wadau kuhusu watuhumiwa kushikiliwa kwa muda mrefu vituo vya polisi na kutofikishwa mahakamani nje ya muda na kinyume cha sheria.

Polisi kuendelea kukamata watuhumiwa kabla ya kukamilisha upepelezi.

Masharti magumu ya dhamana ya polisi.

Mashtaka kuchelewa kuandikwa ofisi ya mashtaka kutokana na uchache wa rasilimali watu na fedha.

Mapendekezo
~ Jeshi la polisi na vyombo vingine vya ukamataji kuwafikisha watuhumiwa mahakamani kwa wakati na kwa mujibu wa sheria na watuhumiwa wasikamatwe kabla ya upepelezi kukamilika isipokuwa kwa makosa makubwa.

4/ Upelelezi kuchukua muda mrefu
Wanachi walalamikia upelelezi kuchukua muda mrefu.

Mapendekezo
~ Sheria ya mwenendo ya Mashauri ya jinai irekebishwe, iweke kikomo wa muda wa upelelezi kwa mashauri yanayosubiri kusikilizwa Mahakama kuu.

5/ Matumizi Mabaya ya Madaraka
Wakuu wa Mikoa na Wakuuwa Wilaya wanalalamikiwa kutumia vibaya yao ya kutoa amri ya kuwakamata na kuwaweka wananchi mahabusu. Tume imependekeza mamlaka haya yafutwe.

Wakuu wa wilaya na mikoa kuongozana na wajumbe wa kamati za usalama hata katika ziara ambazo hazistahili uwepo wa kamati hizo.

wakuu wa mikoa na wilaya kujitambulisha kama Wenyeviti wa Kamati za Ulinzi na Usalama kinyume na sheria.

Mapendekezo
~ Wakuu wa mikoa na wilaya wakiwa anatekeleza mamlaka ya ukamataji ni muhimu kufata kifungu cha 7 na 15.

~ Kiongozi yoyote atakayekiuka maagizo awajibishwe.

~ Wakuu wa mikoa na wilaya wasijitambulishe kama wenyekiti wa kamati za ulinzi na usalama badala yake wajitambulishe kama Wenyeviti wa Kamati za usalama wakiwa wanaongoza vikao vya baraza la usalama.

~ Mamlaka ya kumkamata na kumuweka mtuhumiwa kizuizini waliyonayo wakurugenzi wa halmashauri na maafisa watendaji wa kata yaondolewe na yaache mikononi mwa jeshi la polisi, na mahakimu ambao ni walinzi wa amani waondolewe pia mamlaka hayo.

~ Baadhi ya viongozi wa juu wa kisisasa wamekuwa wakitoa matamko na amri kwa vyombo vya dola kukamata na kuweka ndani wananchi wakati mamlaka hayo hawana; Viongozi hao walekezwe kuzingatia sheria.

6/ Upelelzi na Uchunguzi
Kutotenganishwa kwa idara ya upelelezi wa jeshi la polisi na shughuli zingine za jeshi hilo limesababisha ucheleweshaji wa upelelezi, ukosefu wa ubobezi, ufanisi mdogo katika upelelezi, na upelelezi wa jeshi la polisi wakati mwingine kupangiwa shunguli nyingine ambazo hazihusiani na upelelezi.

Idara ya upelelezi ya jeshi la polisi inategemea bajeti ya jeshi la polisi na hivyo kuwa na bajeti ambayo haikidhi mahitaji.

TAKUKURU inakabiriwa na ukosefu wa wachubguzi wabobezi na wenye weledi wa kutosha kuhusu masuala ya rushwa, ufinyu wa bajeti, ukosefu wa vitendea kazi na kukosa ushirikiano kutoka taasisi nyingine.

Mamlaka ya Kudhibiti na kupambana na Dawa za Kuvya inakabiliwa na changamato kadhaa ikiwemo mamlaka hii kutokuwa chombo cha muungano na kuwa katika maeneo machache nchini.

Changamoto ya uhalifu kuungamana mfano uhalifu wa kusafirisha dawa za kulevya kuhusiha utakatishati wa fedha na rushwa.

Mapendekezo
~ Serikali iunganishe nguvu ya upelelezi na uchunguzi iliyopo sasa ya vyombo vyote hivi kwa kuanzisha mamlaka upya huru ya upelelezi itakayojulikana na itakayijitegemea kama ofisi ya taifa ya upelelezi - National Bureau of Investigation itakayokuwa na jukumu la kupepeleza makosa yote makubwa ya jinai yakiwemo Rushwa na Dawa za Kulevya.

7/ Makubaliano ya kukiri kosa
Mapendekezo

~ Elimu zaidi itolewe kuhusu makubaliano ya kukiri kosa.

~ Malalamiko ya washtakiwa kulazimishwa kukiri kosa ambao wanasema hawakukiri kosa kwa hiari washaghulikie kwa kufata utaratibu mfano njiaya mahakama kutengua uamuzi huo.

~ Iundwe timu maalumu ya kuchunguza utata katika baadhi ya mali zilizotaifishwa katika utaratibu wa kukiri kosa na utendaji wa kikosi kazi ili kuishauri serikali.

8/ Uhuru wa kufuta mashauri mahakamani aliyonayo Mkurugenzi wa Mashtaka bila kutoa sababu na mahakama kutoweza kuingilia uamuzi huo
Uwepo wa malalamiko ya matumizi mabaya ya fursa hii - sheria ilirekebishwa (kifungu cha 31 (3)).

Mapendekezo
~ Mamlaka ya DPP kufuta kesi kwa uhuru wake ilendelee lakini kama kutaendelea kuwa na changamoto ya matumizi mabaya ya uhuru huu marekebisho ya sheria yanaweza kufanyika kama ilivyo kwa nchi nyingine ili uhuru huo utolewe kwa ridhaa ya mahakama.

~ Maafisa wa mahakama na waendesha mashtaka watakaoshindwa kuzingatia matakwa ya sheria wanatakiwa kuwajibika.

9/ Dhamana
Wadau mbalimbali wamekuwa na mtazamo tofauti kuhusu sheria zinazoruhusu dhamana kwa baadhi ya makosa, kwa sasa mamkosa ambayo yanakosa dhamana ni takribani 50.

Mapendekezo
~ Bila kuathiri mikataba ya kimataifa ya makosa ya udhibiti uchumi na mengine tafsiri ya makosa tangulizi ya utakatishaji fedha haramu irekebishwa ili kupunguza washtakiwa wengi kukosa dhamana kutokana na tafsiri hiyo pana.

~ Jedwali la 1 linaloainisha makosa ya uhujumu uchumi katika sheria ya kudhibiti makosa ya uhujumu uchumi na uhalifu wa kupangwa lipitiwe upya ili kuona iwapo kama kuna umuhimu wa makosa yote yaliyobainishwa kwenye sheria hii kuendelea kuwa ya uhujumu uchumi.

~ Makosa kwenye sheria ya kudhibiti uchumi irekebishwe kjuipa maamuzi ya dhamana mahakama ya Tanzania.

~ Sheria ya mwenendo ya mashauri ya jinai irekebishwe ili masharti ya makosa yasiyo na dhmana yaanze kusikilizwa ndani ya muda maalum na ikiwa mashauri hayo hayajasikilizwa ndani ya kipindi maalum basi mtuhumiwa anaweza kupewa dhamana.

~ Itungwe sheria moja ambayo itabeba kila kitu kuhusu dhamana.

10/ Utitiri wa vyombo wenye taswira ya kijeshi
Uwepo wa vyombo vya haki jinai vinavyotekeleza majukumu yake kwa taswira ya kijeshi jeshi la zima moto na uokoaji, jeshi la uhamiaji, jeshi usu la uhifadhi hali inayosababisha matumizi ya nguvu kupita kiasi kwa watuhumiwa katika ukamataji, upekuzi na mahojiano.

Uvaaji wa vyeo vinavyoshahabiana na jeshi la ulinzi na usalama la Tanzania.

Baadhi ya Taasisi hizo kujilinganisha hadhi na Jeshi la Ulinzi na Usalama.

Taasisi za haki jinai kukosa ushirikiano.

Malalamiko ya wananchi ya kunyanyaswa na kuteswa na taasisi zenye taswira ya kijeshi.

Kuwepo kwa uwezekanao wa kusambaa silaha zikiwemo za kivita suala ambalo linaweza kutishia amani ya nchi

Mapendekezo
~ Taasisi zinazotekelza majukumu ya Haki Jinai au zinazotoa huduma kwa wanachi zenye taswira ya kijeshi zirejee na kujikita zaidi kwenye majukumu yake ya awali ya utoaji huduma kwa wananchi.

~ Huduma za zima moto na uokoaji zirejeshwe na kutekelezwa kwenye ngazi ya halmashauri hasa ikizingatiwa shughuli za kuzima moto zina uingiliano mkubwa na shughuli nyingina za halmashauri katika mipango miji.

~ Mafunzo ya askiri misitu, uhifadhi na nyamapori yatolewe yatolewe na polisi kwa kuzingatia misingi ya haki jinai, binadamu na utawala sheria.

~ Waziri wa Maliasili na Utalii warejeshee watumishi wote raia katika vyombo vyao vya ajira ya awali na kuwaondolea mavazi ya vyeo ya kijeshi isipokuwa tu mavazi yavaliwe na watumishi walioko kwenye idara inayohisana na majukumu yakupambana na ujangili.

11/ upelelezi binafsi
Mapendekezo

~ Tume itunge sheria mahususi itakayoruhusu na kusimamia upelelezi binafsi ambapo itaainisha mamlaka itakayosimamia na kuratibu upelelezi binafsi, masharti ya usaili, aina ya upelelezi, mipaka ya upelelezi binafsi, maadili na nidhamu, wajibu wao wa jeshi la polisi na vyombo vingine vya uchunguzi.

12/ Adhabu ya kifungo cha maisha
Maoni na malalamiko ya kifungo cha maisha hakiwapi wafungwa nafasi ya kujirekebisha na kuendelea kulitumikia taifa na kwamba wakati umefika kifungu hiki kiwe na ukomo ili kuhakikisha wafungwa wanaotumikia kifungo cha maisha kuwa na matumaini.

Mapendekezo
~ Tume inapendekeza kwa sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 irekebishwe ili kuweka tafsiri ya kifungo cha maisha kwa kuonesha muda maalum wa kifungo.

13/ Adhabu ya kifo
Kuna maoni mbalimbali juu ya adhabu ya kifo, baadhi wanasema adhabu ya kifo isiondolewe kwakuwa ni stahiki kwa makosa yaliyotendwa na muhusika na ni funzo kwa jamii kutotenda makosa ambayo adhabu yao ni kifo. Wengine wanapendekeza adhabu ya kifo iondolewe kwakuwa ni ya kikatili isiyozingatia haki ya kuishi na haki za binadamu.

Adhabu hiyo imekuwa haitekelezwi kwa miaka mingi na kusababisha waliopewa adhabu hiyo kuishi maisha ya hofu huku wakisubiri utekelezaji wa adhabu hiyo, takwimu zinaonesha hadi Mei 2023 kuna watuhumiwa 691 wanasubiria kutekelezwa kwa adhabu hii, Tanzania haijatekeleza adhabu hii kwa miaka zaidi ya 28.

Mapendekezo
~ Sheria ya kanuni za adhabu, sura ya i6 ifanyiwe marekebisho ili adhabu ya kifo isiwe adhabu pekee ya kosa la mauaji.

~ Adhabu ya kifo isiporidhiwa na Rais kwa mamlaka aliyonayo kikatiba kwa kipindi cha miaka mitatu adhabu hiyo itengulike kuwa kifungo cha maisha.

View attachment 2688955
Samia Suluhu Hassan - Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

~ Mageuzi makubwa yaliyopendekezwa na Tume ya Haki Jinai yanaanza kwanza kwa kubadilisha mtazamo wetu sisi wenyewe kabla ya kwenda kwenye maboresho ya kiutawala na kiufundi.

~ Itungwe sheria kwa vingozi wanaoingia kwenye maeneo ambayo sio yao washughulikiwe.

~ Vyombo vya Haki Jinai visomane ili kupunguza watu kutotendewa haki.

~ Jeshi la Polisi litizamwe na kurebishwa, lisimame vizuri pamoja na stahiki zao kufanyiwa kazi ili lifanye kazi zao vizuri.

~ Nguvu za kupiga vita madwa ya kulevya na rushwa itiliwe mkazo kwa pande zote mbili Bara na Zanzibar.

~ Liandikwe concept paper ya marekebisho ya demokrasia, utawala bora na haki za binadamu Tanzania na kuwashirikisha wadau wengine wanaotaka kusaidia kwenye maeneo hayo.

~ TBC iite wataalam kuchambua Ripoti ya Tume ya Haki Jinai ili watu wasikie na waone mwelekeo wa serikali inapoelekea.

Bonge la article
 
SOMA HAPA MUHTASARI WA RIPOTI YA TUME YA KUANGALIA JINSI YA KUBORESHA TAASISI ZA HAKI JINAI NCHINI
 

Attachments

  • MUHTASARI HAKI JINAI.pdf
    503.4 KB · Views: 3
Nimekuwa mvivu wa kusoma ripoti kubwakubwa nategemea uchambuzi wa wadau wa forum hii ya jamii lakini kinyume na matarajio naona ukimya umetawala au DPW bado imeshika hatamu.?
 
Mama anazunguka mbuyu huyu,Itungwe sheria ya kuwaadhibu viongozi wanaofanya makosa period.Yaaan blah blah nyingiii.This county bwana,Aaaah
 
Kuna uzi nilitoa swala la jeshi la polisi swala la ukachero na upelelezi kuwa idara tofauti ila niliishia kushambuliwa na watu ambao itakuwa wapo idara hiyo.

Tumeona tume haki jinai imeeleza kila kitu kuhusu ili jambo na mapungufu yake.

Mda mwengine mtusikilize wananchi kasoro tunazoziona tena undani kabisa
IMG_0028.jpg
 
Kwa hili, Kongole sana Mh Rais, ila isiwe maneno matupu fuatilia uone utekelezaji wake.
 
Kuna uzi nilitoa swala la jeshi la polisi swala la ukachero na upelelezi kuwa idara tofauti ila niliishia kushambuliwa na watu ambao itakuwa wapo idara hiyo.

Tumeona tume haki jinai imeeleza kila kitu kuhusu ili jambo na mapungufu yake.

Mda mwengine mtusikilize wananchi kasoro tunazoziona tena undani kabisa View attachment 2689627
Mrejesho wa kamati unadhihirisha namna kulivyo na pengo kubwa la haki kwenye mtirirko wa utoaji na usimamizi wa haki nchini.

Jeshi la polisi livunjwe au sheria ya uundwaji wake iboreshwe mpaka jina lake
 
Tume na ripoti za kupotezeana muda maana hakuna utekelezaji wowote. Iwapo ccm itaendelea kukaa madarakani kwa shuruti, tusitegemee utekelezaji wowote wa hayo mapendekezo hayo, maana zaidi ya 80% ya hayo malalamiko na mapendekezo ni athari za uwepo wao madarakani.
Nina uhakika hujasikiliza kilichosemwa
 
Mtaje kwanza na bei iliyouziwa
Kama ambavyo Loliondo iliuzwa hatukuambiwa tulishangaa watu wanahamishwa anakabidhiwa mnunuzi ndivyo bandari ilivyouzwa sirini tukashangaa kuona kataba la kimangungo. Siku ukiona unafukuzwa kwenye shamba lako na unaambiwa ni mali ya mtu mwingine jua limeshapigwa bei bila wewe kujua hata ukiuliza bei hutaambiwa sasa usishangae bandari imeuzwa kwa mabadilishano na kioo cha kujitazama.
 
hakuna Raia ana haki yoyote Polisi

sana sana Polisi akikukamata ni kama kakamata paka tu.

Jeshi la polisi lichunguzwe sana Raia tunapitia madhira mengi kupitia Polisi.

Polisi akija kukukamataka kitu atakachochukua uhesabu maumivu maana hutakipata tena …
 
Back
Top Bottom