Tangawizi
JF-Expert Member
- Jun 25, 2009
- 5,266
- 4,097
Daima nimemsifu Bashe kwa msimamo wake wa kutokuzuia wakulima kuuza mazao yao mahali popote, iwe ndani ya nchi au nje ya nchi. Kwenye hilo mpaka sasa namwunga mkono.
Lakini taarifa kwamba Serikali imetumia milioni 16 kwa kila ekari 1 kusafisha shamba/kuandaa shamba, ni upotevu wa pesa wa hali ya juu.
Namwomba Rais ateue kamati ndogo ya watu wachache, au amwombe CAG achunguze ili kujua gharama halisia za kuandaa shamba ekari 1, na kisha kuwapata wahusika wote waliohusika kwenye wizi huu wa pesa ya wananchi.
Pamoja na mambo mengine, nnafanya pia shughuli za kilimo. Nina ekari 657. Nazifahamu gharama halisi kwenye kilimo. Japo kuna utofauti mdogo wa gharama unaotegemea mahali shamba lilipo lakini kiuhalisia hakuna utofauti mkubwa katika gharama.
Uandaaji huu wa shamba unahusisha vitu gani hadi kufikia gharama hiyo?
Kwa ujumla wazo la kuiinua na kuiendeleza sekta ya kilimo, hakika ni wazo zuri sana lakini approach ni completely wrong. Na mpango mzima hautafanikiwa. Pesa hii yote inayopelekwa huko itapotea.
Mpango wa kuinua sekta ya kilimo ulistahili kwa kuwasaidia wale ambao tayari wanafanya shughuli za kilimo huko vijijini. Hao tayari kwanza wanakipenda kilimo, wana mipango, wana elimu ya kilimo iliyotokana na wao kufanya kilimo, na hivyo Serikali ilistahili kuwasaidia kwenye maeneo yale ambayo wao wakulima tayari wanayatambua kama kikwazo kwa wao kufanya kilimo kwa ufanisi. Mafanikio ya wakulima hao, yangewavuta wengine wengi kuingia kwenye kilimo.
Huu mpango wa kuwakokota vijana wa mjini kuwapeleka kwenye kilimo kwa ahadi nyingi za kusaidiwa, wengi watajitokeza, lakini baada ya mwaka mmoja, watabakia si zaidi ya 50% tu kwenye kilimo. Baada ya miaka 3, watakaobakia wakifanya kilimo hawatazidi 25%. Na hao watakaobakia kwenye kilimo, watakaofanikiwa kufanya kilimo chenye faida hawatazidi 10%.
Huu mradi, unaweza kuwa sawa na ule wa 'mabilioni ya Kikwete'; ambao uliishia kwenye upotevu wa mabilioni ya pesa.
Kama ule wa kununua na kugawa simu, wa kupelekea watu majiko ya gesi, na mingine mingi. Ifike mahala sasa, serikali ianze kuwahusisha kwa nguvu zaidi walengwa kwa muundo wa kuwa wafanyabiashara.
Ukianzisha kitu ambacho hakina ownership, uzoefu unaonyesha vinakufa hata havijaanza
Tuanzie kwenye yale mamilioni ya JK. Hivi nani alinufaika na nani anaweza kutoa mahesabu yake?