voicer
JF-Expert Member
- Jul 13, 2020
- 5,553
- 11,885
Haiwezi kuwa serikali awamu ya Sita wakati inatumia ilani ya uchaguzi iliyotumiwa na Awamu ya Tano kushinda uchaguzi na kuingia Madarakani.
Haiwezi kuwa serikali awamu ya sita kwa sababu haijapigiwa kura na wananchi wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hii ni serikali muendelezo wa awamu ya Tano, iliyoingia madarakani kwa mujibu wa Vifungu vya katiba.....
"Kwa mujibu wa kifungu cha 37 (5) cha Katiba ya JMT.iliyotungwa mwaka 1977, nafasi ya urais inapokuwa wazi kwa sababu yoyote ikiwemo kifo, viongozi watatu wameorodheshwa na ni Makamu wa Rais, na endapo hatakuwepo atachukua Spika wa Bunge na kama hayupo atachukua Jaji Mkuu."
Sasa Samia anapotaka tumtambuwe kama Rais wa awamu ya sita anatumia kifungu gani cha katiba?
Na nini faida kwa watanzania kuiita awamu ya sita badala ya awamu ya tano?
Samia anaposema tufuate Sheria, alipaswa yeye kuwa mfano hai.
Asituaminishe awamu ya sita ambayo imejaa viraka na makovu lukuki.
Awamu ya Sita itaanza ifikapo 2030 na kama tu CCM itaweza kupenya kwenye tundu la sindano ifikapo 2025.
R.I.P mashujaa wetu.
Amen .