Rais Mwinyi aunda Kikosi kazi cha Kuimarisha Demokrasia Zanzibar akipa Siku 14 kuwasilisha Ripoti, Chadema wamo Kikosini!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,004
142,034
Rais wa Zanzibar Dr Mwinyi ameunda Kikosi kazi chenye Wajumbe 11 kitakachoangalia mwenendo wa Demokrasia nchini humo

Kikosi kazi kimepewa Siku 14 kukamilisha kazi yake na kumkabidhi Ripoti

Miongoni mwa vyama vilivyotoa Wajumbe ni pamoja na CCM Chadema CUF, ACT wazalendo nk

Source ITV habari

====

Daktari Hussein Ali Mwinyi azindua kikosi kazi maalumu cha kukusanya maoni ya wadau kuhusiana na hali ya kisiasa kwa upande wa Zanzibar.​

Jumla ya wajumbe 11 wameteuliwa katika kikosi hicho wakitokea kwenye vyama vya siasa, asasi za kiraia, taasisi za kidini na wasomi

Mwenyekiti wa kikosi hicho ni Dk Ali Uki, Makamo Mwenyekiti ni Balozi Amina Salum Ali, wajumbe ni ACT Wazalendo Ismail Jussa, CCM Vuai Ali Vuai, Chadema Said Issa Mohammed, CUF Rukia Kassim Ahmed, Demokrasia Makini Ameir Hassan Ameir, mashirika yasiyo ya kiserikali Joseph Abdallah Meza, Taasisi za kidini, Sheikh Thabit Nauman Jongo na Padri Stanley Nikolas Nchinga, Mjumbe na Kutoka wasomi Mohammed Professa Mohammed Makame Haji Katibu ni Mohamme Ali Abdallah.

Akitoa neno fupi mbele ya Rais Msajili wa vyama vya kisiasa Jaji Fransic Mutungi ameahidi ofisi yake kufanyia kazi mapendekezo ili nchi ibaki salama.

Jumla ya hadidu rejea sita zimepewa kikosi kazi hicho kwa ajili ya kuzifanyia kazi kabla ya kuwasilisha ripoti hiyo kwa Rais wa Zanzibar kwa muda wa siku 14.

Akisoma hadidu rejea za kikosi kazi hicho mbele ya wajumbe Katibu Mkuu ofisi ya makamo wa pili wa Rais Thabit Idarous Faina aliwaambia wajumbe kuwa hutuba za viongozi wakuu za ufunguaji na ufungaji wa mkutano wa wadau uliofanyika wiki iliyopita zihusishwe katika kazi hiyo.

Kazi kubwa walionayo ni kuchambua maoni yaliotolewa na wadau wa vyama vya siasa, asasi za kiraia pamoja wananchi kuhusiana na hali ya kisiasa nchini.

DW
 
Huyu ni Presidential material.

Huku kwetu, Rais Samia anaweza kuwa 8na dhamira njema kabisa, lakini tatizo liko ndani ya CCM, cha kilichozoea dhuluma, ushirikina, na kila aina ya uchafu.

"WanaCCM hawaachiani vinywaji mezani" - Kikwete. Ina maana wapo tayari kuuana hata wenyewe kwa wenyewe kwa sababu ya madaraka.

"Wahuni wapo ndani ya CCM. Wanaweza hata kukuua" - Poepole.

Watu ambao wapo tayari hata kuuana wenyewe kwa wenyewe kwa sababu ya vyeo, kweli wanaweza kutengeneza mazingira ya demokrasia ya kweli?
 
Huyu ni Presidential material.

Huku kwetu, Rais Samia anaweza kuwq na dhamira njema kabisa, lakini tatizo liko ndani ya CCM, cha kilichozoea dhuluma, ushirikina, na kila aina ya uchafu.

Duh......we jamaa bhana!
 
Democrasia kila siku wanafuta usajili wa makanisa, na kuzuia mengine yasijengwe,wawadanganye wapumbavu wenzao
 
CCM kweli nzuri, inagawa asali kwa chadema hadi huko Zanzibar 😂
 
CHADEMA na CUF nawashauri mshishiriki huu unafiki huko visiwani. Waachieni wenyewe na mtoto wao wa zambarau.
 
Huyu ni Presidential material.

Huku kwetu, Rais Samia anaweza kuwq na dhamira njema kabisa, lakini tatizo liko ndani ya CCM, cha kilichozoea dhuluma, ushirikina, na kila aina ya uchafu.

"WanaCCM hawaachiani vinywaji mezani" - Kikwete. Ina maana wapo tayari kuuana hata wenyewe kwa wenyewe kwa sababu ya madaraka.

"Wahuni wapo ndani ya CCM. Wanaweza hata kukuua" - Poepole.

Watu ambao wapo tayari hata kuuana wenyewe kwa wenyewe kwa sababu ya vyeo, kweli wanaweza kutengeneza mazingira ya demokrasia ya kweli?
Hii ndiyo comment yangu Bora ya mwezi huu....
 
Naona Jussa kanaswa hatimaye zile habari zake za kumsimanga Dkt. Mwinyi na YouTube channel yao ya Zanzibar Kamili imeisha iyoo.
 
Rais wa Zanzibar Dr Mwinyi ameunda Kikosi kazi chenye Wajumbe 11 kitakachoangalia mwenendo wa Demokrasia nchini humo

Kikosi kazi kimepewa Siku 14 kukamilisha kazi yake na kumkabidhi Ripoti

Miongoni mwa vyama vilivyotoa Wajumbe ni pamoja na CCM Chadema CUF, ACT wazalendo nk

Source ITV habari

====

Daktari Hussein Ali Mwinyi azindua kikosi kazi maalumu cha kukusanya maoni ya wadau kuhusiana na hali ya kisiasa kwa upande wa Zanzibar.​

Jumla ya wajumbe 11 wameteuliwa katika kikosi hicho wakitokea kwenye vyama vya siasa, asasi za kiraia, taasisi za kidini na wasomi

Mwenyekiti wa kikosi hicho ni Dk Ali Uki, Makamo Mwenyekiti ni Balozi Amina Salum Ali, wajumbe ni ACT Wazalendo Ismail Jussa, CCM Vuai Ali Vuai, Chadema Said Issa Mohammed, CUF Rukia Kassim Ahmed, Demokrasia Makini Ameir Hassan Ameir, mashirika yasiyo ya kiserikali Joseph Abdallah Meza, Taasisi za kidini, Sheikh Thabit Nauman Jongo na Padri Stanley Nikolas Nchinga, Mjumbe na Kutoka wasomi Mohammed Professa Mohammed Makame Haji Katibu ni Mohamme Ali Abdallah.

Akitoa neno fupi mbele ya Rais Msajili wa vyama vya kisiasa Jaji Fransic Mutungi ameahidi ofisi yake kufanyia kazi mapendekezo ili nchi ibaki salama.

Jumla ya hadidu rejea sita zimepewa kikosi kazi hicho kwa ajili ya kuzifanyia kazi kabla ya kuwasilisha ripoti hiyo kwa Rais wa Zanzibar kwa muda wa siku 14.

Akisoma hadidu rejea za kikosi kazi hicho mbele ya wajumbe Katibu Mkuu ofisi ya makamo wa pili wa Rais Thabit Idarous Faina aliwaambia wajumbe kuwa hutuba za viongozi wakuu za ufunguaji na ufungaji wa mkutano wa wadau uliofanyika wiki iliyopita zihusishwe katika kazi hiyo.

Kazi kubwa walionayo ni kuchambua maoni yaliotolewa na wadau wa vyama vya siasa, asasi za kiraia pamoja wananchi kuhusiana na hali ya kisiasa nchini.

DW
Cha Zanzibar ni wiki 2 , ila genge la Mukandala na Pinda ni la milele !
 
Back
Top Bottom