Tairi bovu
JF-Expert Member
- Sep 28, 2017
- 3,063
- 2,983
Elimu ya chuo kikuu ni tertiary education ni elimu ya vitendo yenye kumfanya mtu ayapambanue mazingira yake. Akiongea na wanachuo wa SUA leo ameonekana kutoelewa maana ya elimu ya chuo.
Kwa taarifa tu msomi yeyote asiyekuwa (kasuku). hufungamana na jamii yake, huyaelewa matatizo na kuyatafutia ufumbuzi, kufanya hivyo sio uasi wala uhaini, ni kuelewa na kuitendea haki elimu ya chuo.
Namshangaa Rais anaposema wanachuo wasifanye siasa kivipi? chuo kikuu cha DSM kuna course inaitwa Political science. Hivi wanafunzi wale ukiwaambia wasijihusishe na siasa unamaanisha ile taaluma haina maana ama vipi?.
Rais anawambia wanafunzi katika kipindi chake wasithubutu kugoma na wakigoma atawafukiza na akiwafukuza hajui atawarudisha lini? Hii ni kauli toka kwa mtu asiyeelewa vizuri mazingira na thamani ya elimu ya chuo kikuu. wakati wa mwalimu nyerere wana chuo waligoma intake ya kina samwel sitta waligoma kwa kukataa kwenda jeshini kwa mujibu wa sheria. nyerere hakuwatisha aliwasikiliza. wakati wa mwinyi chuo kikuu kulukuwa na " punch" mwinyi hakusema wanachuo wanatumiwa na mabeberu. kipindi cha kina mkapa na jakaya mdipo walipoibukia hawa kina MWIGULU waliongoza migomo ya kila.aina . ilifikia wakati mwigulu pamoja na kufaulu kwake vizur alikatazwa kusoma shahada ya uzamili chuo kikuu cha mlimani . hakufukuzwa vyuoni wapo wengi ukijumuisha kina.ndaskoi (mmasai).nk
Mfano mwanafunzi wa chuo anaweza akawa anapewa huo mkopo lakini umeme unakatika wakati wa kujiandaa na mitihani yake? Hapo akigoma anakuwa amefanya kosa gani? " someni kwanza hizi siasa mtazikuta tu" anasahau kuwa chama chake kina matawi kwenye vyuo vikuu vyote hapa nchini? mwanafunzi wa chuo anaweza akapewa mkopo lakini kama hana uhakika wa ajira huo mkopo ataulipaje? mwanafunzi wa chuo anaweza kupewa mkopo lakini kama mzazi wake amefukuzwa kazi kimagumashi akigoma atalaumuwa? mwanafunzi wa sanaa ya siasa anayeshughudia kasoro nyingi kwenye chaguzi za marudio akigoma atakuwa amekosea? mwanafunzi anayegoma kuhoji mauaji ya MKIRU atakuwa anakosa la kufukuzwa chuo kweli?
Anatolea mfano enzi zake akiwa chuo kwamba " wakati wanakaribia na mitihani palikiwa panatokea kunji" na kwamba wale vilaza ndiyo waliokuwa wanaongoza migomo kwa kuhofia kukamatwa! uongo ulioje .
Kitila Mkubo ( Katibu Mkuu wizara ya maji) alikuwa rais pakatokea mgomo yeye Kitila alikuwa kilaza, Zitto, Mwigulu, Rugemarila, Alberto Msando wote hawa waliwahi kuwa sehemu ya migomo bila kumsahau Samwel Sitta kweli hawa walikuwa vilaza?
Asichokielewa Rais ni kimoja tu... " mwanafunzi wa chuo kikuu ambaye anasoma miaka 3 au 4 bila kugoma" huyo haelewi anasoma kwa kukariri! ni.msomi " kasuku" ni aliyejingishwa na watawala. kwenye vyuo vikuu vyote kuna matawi ya chama cha mapinduzi hii sio siasa? wakati wa chaguzi zote za serikali za wanafunzi zote chama cha ccm kkinaweka nguvu kwa wagombea wao. hiyo sio siasa?
Mwenye kuelewa huhoji na akihoji anadadisi akidadisi asipojibiwa anagoma. pamoja na kuwa magufuli anajilinganisha na nyerere kama kweli lakini nyerere hakupita vyuoni na kuwatisha wanafunzi wasigome.
Kutisha wanafunzi wasigome ni kutengeneza " wasomi" KASUKU
JItafakati.