Rais Magufuli sasa huna jinsi, Toka nje ya nchi

Habari Comrades..

Kwasababu sasa Mh Rais umeshaona na kukubali wewe mwenyewe kwamba misaada kwa Nchi hii ni LAZIMA..haikwepeki. Na kwamba ulifanya kosa sana pale ulipokebehi misaada ya kutoka nje kwa hii nchi..sasa huna jinsi Mh Rais toka nje ya Nchi

Kwa sasa hali ilipofikia, Rais kafanye ziara nje ya Tanzania kwenye Nchi zile ambazo tumekuwa na udugu na urafiki wa siku nyingi kwa mfano Mataifa ya Scandinavia (Sweeden, Norway, Finland na Denmark) na mataifa mengine ya Ulaya na America huko aende akakutane na wawekezaji na kuongea nao physically kuwaeleza hali ya Nchi, vivutio vya uwekezaji n.k. Tengeneza Mahusiano mazuri na watu wa huko nje. Acha kujifungia tu ndani.

Hii kukaa hapa ndani muda wote na kukutana na akina Mengi na Wafanyabiashara wa ndani peke yake haitoshi. Nenda nje kawaeleze hao watu huko mambo ya Tax Holiday etc etc na vivutio vingine vya kuwekeza hapa Tanzania.

Hivi sasa unakaa tu kupokea marais wa nje na kuomba msaada kwa kila kiongozi anaekuja kutembelea hapa Tanzania, hii sio sawa kabisa, hadi Ethiopia tunawaomba hivi sasa!!

Nenda nje mwenyewe.Kama unamtumia sana Waziri wako wa Foreign, huyu sio competent kabisa. Hamfikii hata nusu Membe kwa Diplpmasia ya Nje.

Nenda nje tafadhali.
Unaogopa nini..!!
na kweli hana ujanja la sivyo nchi itamshinda kama ilivomshinda baba wa taifa. JK alikuwa vizuri katika hili na misaada wakati wa JK ilimiminika, mikopo ya masharti nafuu ilimiminika, tatizo lilikuwa usimamizi haukuwa mzuri.
 
Alituambia Tanzania ni tajiri hatuhitaji misaada,cha kuchangaza kila Rais anaekuja Tanzania anamuomba msaada,watanzania tuamke.Kusema ukweli mimi naanza kupunguza imani yangu kwa Rais,bora tu akatembeze bakuli kwa nchi tajiri,maana imeshadhihirika kuwa Tanzania siyo nchi tajiri na inahitaji misaada.
 
"Rais wa nchi maskini aliyeamua kujifungia ndani ya nchi yake ili afuatwe na marais wengine wa nchi maskini na kuwaomba msaada"
 
Rais wa kupiga mizinga?
Hii sasa ni aibu kubwa sana, maana kila akitembelewa tu hapo hapo anaomba msaada!!
Yaani mpaka Ethiopia tuliwaomba msaada!
 
JK mlipinga mno ziara zake mkasema ni hasara kwa serikali. Mkamuita Vasco Da Gama! Sasa Magufuli amekuja na system mpya ya kulipa hilo jukumu wizara ya mambo ya nje kupitia mabalozi. Hili nalo mnaona ni kosa kubwa!

Najuta kuzaliwa taifa moja na watu wa aina hii!
 
Mtamkumbuka sana ,JK naye alisema wakati anaaga mtanikumbuka mnasema mie mlegevu, too much smiling sasa linaingia tinga tinga JEMBE.
Oh!!! mwanagu Magu weka muziki achana na maneno yao, kula kulala hao wanyooshe mpaka wapige push up
Ulipo kuwa waonyesha mfano wa push up na trotting ktk kampeni zako walikukejeli sana kwa sababu ya ufinyu wa fikra zao na elimu zao hawakujuwa kama unawakilisha ulimi kwa vitendo na hiyo ndio lugha ya tija.lakini hatambui hilo ila mwenye mwanga kichwani.
PIGA KAZI MAGU KAZA TWENDE PUNDE WATAELEWA KWANINI PAKA HULALA JIKONI
JPM OYEEEEeeeeeeeeee by 100%
 
Wasiwasi wangu huyu jamaa ipo siku atajisahau amuombe shein msaada. Itakuwa hivi, shein ameshuka kwa ndege anapokelewa kwenda ikulu, jamaa anampokea na kumwambia mzee naomba unisaidie vijana wangu wapate ajira.... Shein anacheka kwa dharaaaaaaaaau,..... Mzee vipi tena mm si balozi wako visiwa vya karafuu

Oooo niridhani ni mfarume wa Oman bwana. Ok PIGA KAZI
 
Sio nyie mliokuwa mkipiga kelele JK anapenda safari na kumkashifu anapoteza hela za nchi, kama kweli mlikuwa ni wenye akili utokaji nje wa Jk umefunguwa au kutengeneza miradi mingapi humu nchini? kama hamtokuwa na jicho mchungwa nyie, miradi takriban yote anayosimamia Magufuli hivi sasa ni mazao ya Jk kwa safari zake za nje wakati wake kutafuta wafadhili,
Leo Magufuli Katulia tuli kama sultani kipingo kwenye Kizimba chake, kawa mbaya mwapita mkibweka midomo juuuuu, toka !!! toka !!!! haaa !!! lipi zuri kwa bata maji ?
Unafki hautokubadilisheni rangi
sultan kipingo kakosa udevu na lemba kubwa. Kizimba cha moto sana hadi anataka kukopa kwa wazulu.
 
Habari Comrades..

Kwasababu sasa Mh Rais umeshaona na kukubali wewe mwenyewe kwamba misaada kwa Nchi hii ni LAZIMA..haikwepeki. Na kwamba ulifanya kosa sana pale ulipokebehi misaada ya kutoka nje kwa hii nchi..sasa huna jinsi Mh Rais toka nje ya Nchi

Kwa sasa hali ilipofikia, Rais kafanye ziara nje ya Tanzania kwenye Nchi zile ambazo tumekuwa na udugu na urafiki wa siku nyingi kwa mfano Mataifa ya Scandinavia (Sweeden, Norway, Finland na Denmark) na mataifa mengine ya Ulaya na America huko aende akakutane na wawekezaji na kuongea nao physically kuwaeleza hali ya Nchi, vivutio vya uwekezaji n.k. Tengeneza Mahusiano mazuri na watu wa huko nje. Acha kujifungia tu ndani.

Hii kukaa hapa ndani muda wote na kukutana na akina Mengi na Wafanyabiashara wa ndani peke yake haitoshi. Nenda nje kawaeleze hao watu huko mambo ya Tax Holiday etc etc na vivutio vingine vya kuwekeza hapa Tanzania.

Hivi sasa unakaa tu kupokea marais wa nje na kuomba msaada kwa kila kiongozi anaekuja kutembelea hapa Tanzania, hii sio sawa kabisa, hadi Ethiopia tunawaomba hivi sasa!!

Nenda nje mwenyewe.Kama unamtumia sana Waziri wako wa Foreign, huyu sio competent kabisa. Hamfikii hata nusu Membe kwa Diplpmasia ya Nje.

Nenda nje tafadhali.
Unaogopa nini..!!
Mhh!
 
WEWE SI NDIYE ULUKUWA MPINGAJI MKUU WA SAFARI ZA RAIS KIKWETE?!
Kakumbukia maisha ya nyumba ndogo tatu za sinza, temeke na kinondoni. Kakumbukia maisha ya kuwambiwa na side chick kwamba laki sio pesa.

Maisha yakienda kwa haki bin sawia hapa bongo ni wachache sana wenye kuweza kuwa na jeuri ya kutukana na kunyanyasa walio wengi.
 
Back
Top Bottom