Rais Magufuli: Ole wake atakayeandamana, kama kuna baba zao wanawatuma, watakwenda kuwasimulia vizuri

Rais Magufuli amesema ole wake mtu yeyote atakayeandamana siku hiyo na kama ametumwa na baba yake basi atakuja kusimulia vizuri kilichompata.

Rais amesisitiza kuwa nchi hii ni ya amani na kuna watu hawapendi kuona nchi hii inaendelea kuwa na AMANI.

Nanukuu - ''Wapo watu ambao wameshindwa kufanya siasa za kweli wangependa kila siku tuko mabarabarani tunaandamana. Watu wao wanahamia huku wao wanataka wabaki wanaandamane kule. Nimeshasema ngoja waandamane wataniona. Kama kuna baba zao wanawatuma, watakwenda kuwasimulia vizuri. Niliapa kwa Katiba kwamba nchi hii lazima iwe ya amani.''

Ametoa rai kwa wananchi wote kuendelea kuitunza amani iliyopo kuliko kutaka kuingiza nchi kwenye migogoro kama nchi zingine tunazosikia huku mashariki ya kati na hata nchi jirani.

Rais Magufuli ameyasema hayo kwenye ufunguzi wa tawi la Benki ya CRDB huko wilayani Chato leo hii.



Februari 26, 2018. IGP Simon Sirro alisema Ole wake atakayeandamana bila kufuata sheria

Mnamo Februari 28, 2018. Mkuu wa Majeshi, Venance Mabeyo alisema Kuna viashiria vinavyotishia Usalama wa Nchi, hatua zinachukuliwa kudhibiti hali hiyo.

Leo Machi 9, 2018 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewaonya wale wote wanaotaka kuandamana katika mkoa huo na kuwaambia labda wafanye hivyo yeye asipokuwa mkuu wa mkoa

Leo Machi 9, 2018. Jeshi la Polisi pia kupitia Mkuu wa Operation na mafunzo, CP Nsato Marijani wakati alipokutana na vyombo vya habari amekionya kikundi kinachohamasisha maandamano ya kuiangusha Serikali kupitia mtandao wa Telegram

Hata Gadafi alitamka hivyo tena akiwaita watu "Panya", la kufanya sasa afikirie pa kukimbilia sio kutoa kauli anazofikiri anatisha wananchi
 
HAKIKA TANZANIA IMEPATA RAIS KUTOKA KWA MWENYEZI MUNGU
Kwake siasa za kistaarabu ni kuua, kuteka na kushambulia wengine. 'Eti....."wenzao" wanahamia "huku" wao wamekalia kuandamana'.
Atokae kwa Mwenyezi Mungu haongei lugha za vitisho. Ana staha. Anatoa nafasi kwa anawongoza kusema waliyonayo na hata kumkosoa. Mikutano hataki, basi atapata maandamano kama ilivyokuwa kwa Gadafi na sasa Congo.
 
S


Siasa ni maisha halisi Mzee baba!! Kwa upande mwingine siasa ni kazi kama zilivyo kazi nyingine tu. Alafu kwenye hili jukwaa umefuata nn? Stupid.
Siasa ni kazi kwa wale wanasiasa, siasa zenyewe ni usanii mtupu. Kama Siasa Maisha nambie yamekuletea faida gani? Bidhaa zako unauza kwa siasa? Unakula kwa sababu ya siasa? Sasa sijui nani Idiot atakuwa, yule anaendesha maisha yake bila kuweka siasa ama yule anaendesha maisha yake kwa siasa. :D :D :D

Nimeingia jukwaani kuwafunua vichwa vyenu na mtizame maisha yenu, sio kila mwaka mnapiga kura na kuumizwa.

Weka check point ili next time nikitaka kuchangia kwenye hili jukwaa unizuie.
 
Ninakumbuka siku kadhaa kabla walibya hawajaamua kumng'oa Muammar Gaddafi,kulikuwa na tetesi tu za watu kuandamana,Gaddafi alichimba mkwara mzito sana,ikiwemo kuwaita mende wataondamana,
"Ninatoa tahadhari kwa mende wanaokusudia kuandamana......"
Maweeee mende wakajaa barabarani,vifaru vya kijeshi vikaingizwa mtaani kupambana na mende,mende wakapata usaidizi kutoka Magharibi,mbabe aliyekuwa ikulu akatafuta mlango wa kuchomokea aachie ikulu,akakimbia kunusuru maisha yake,mende wakamzidi nguvu,mwishowe wakamkamata,wakamsokomezea miti njia yake ya haja kubwa,akauwawa kifo cha aibu.Vifaru,silaha za kivita,ndege za kijeshi na risasi lukuki hazikuweza kumnusuru na hasira ya umma!
Sishabikii wala kufurahia mauaji ya mzee Gaddafi,lakini najifunza jambo kubwa kwamba,sio kila jambo linaweza kumalizwa kwa vitisho vya kupiga watu risasi,au minguvu ya majeshi,kuna baadhi ya mambo yanaweza kumalizwa kwa kuzingatia mahitaji ya watu wako na kufanya mazungumzo chanya!
Uhuru Kenyatta kufanya mazungumzo na Raila Odinga na kuafikiana ni silaha kubwa zaidi ya kuinusuru nchi ya Kenya na machafuko ya kisiasa kuliko angewaambia "ole wenu munijaribu,mtaenda kuhadithia waliowatuma"
Baba usijawe na kiburi kwa kutazama ukubwa wa mizinga ya kijeshi,wingi wa risasi na mabomu,uwepo wa ndege za kivita katika makambi yetu ya majeshi,kwani hayo yote ni kwa ulinzi wa mipaka ya nchi yetu,si kwa ajili ya kuwashughulikia RAIA wa nchi yako!
Lakini kubwa zaidi ni kwamba hata waliojaribu kutumia nguvu kama unavyotishia kutumia nguvu,hawakufanikiwa!
Tujitafakari
 
Of course kwa kuwapa vitisho kuna watu hawatoandamana ila ukweli ni kwamba wanataka kuandamana na kma msipoyazuia watajaa sana watu na ndio mtajua nguvu ya umma

Ila kituko mnakejeli kuwa hakuna atakayeandamana ila hapo hapo mnawapiga biti!! Ndio nini sasa???

Nyie ruhusuni alafu ndio muone kma watu hawatokuja sio kejeli hku mnakataza
Umma wote uko kwa ajili ya kuandama? Embu toeni ujinga wenu mitandaoni.
 
Watanzania hatujafikia hatua ya maandamano!!tupo katika hatua ya Kwanza ya HOFU NA UOGA!!!!

Mimi binafsi sitaandamana kwa sababu naogopa nisije nikaandamana peke yangu!!!

Wabongo bwana!Wavumilivu na wasaliti sana!!!!
 
IMG_1520664705.292849.jpg
IMG_1520664716.956220.jpg
 
Ni sababu gani inayomfanya Magufuli kuyaogopa maandamano ya Mange Kimambi. Kiukweli haya maandamano yanayozungumziwa kwenye mitandao ya kijamiina hasa kwenye Instagram ya huyu Mwanadada Mange pamoja na kwenye magroup ya Telegram inaelekea yanamyima usingizi na amani huyu Magufuli na Bashite. Wameshikwa na Homa ya ghafla ya uoga.

Magufuli mwenyewe anasema Watanzania wanaupenda utawala wake na kuunga mkono, kwani hata Madiwani na baadhi ya viongozi wa upinzani wakijiuzulu kwa jinsi wanavyofurahishwa na utawalaa huu wa Magufuli uliojaa upendo na mshikamano katika taifa letu. Katiba iliyo nzuri inayopendwa na Viongozi wetu.
 
Patamu sana tusubiri kuona....

Nahisi itakua ni zaidi ya enzi za CUF ile ya ngangari na ngunguri

Sema na nyie waandamanaji safari hii mfanye kweli isije kua mnapiga tu JAMBA JAMBA halafu hamuandamani ikifika iyo tarehe....

Kiukweli msipoandamana iyo tarehe 26/4 mtatuangusha sana Watanzania tunaotaka mabadiliko mana tunawategemea nyinyi waandamanaji muikomboe nchi yetu.

Inshallah!
we utakuwa wap?
 
Back
Top Bottom