Rais Magufuli awasomesha namba wakazi wa Ubungo, Kimara na Mbezi kwa mwendokasi

Suala la mwendo kasi lilianza kabla ya JPM hajawa raisi. Hayo mabasi ya daladala yalikuwemo kwenye mpango wa kuyafreeze. JPM hahusiki hapa!!!!
Do you mean hana mamlaka ya kubadili kuwa mazuri?? Mbona kapangua 'mizigo' ya toka serikali iliyopita???
 
Kutokana na wakazi wa Ubungo, Kimara na Mbezi kuipiga chini CCM katika uchaguzi uliopita, sasa inaonekana Mhe. Rais ametoa maelekezo kwa Sumatra kuondoa magari yote kwenye route ya Mawasiliano - Posta, Kimara - Posta na Mbezi - Posta ili wanachi wa maeneo hayo waisome namba.

Katika utafiti wetu mdogo tulioufanya kwa baadhi ya wakazi wa maeneo hayo wanasema Rais Magufuli ndio ametoa maelekezo kuyaondoa mabasi hayo ya abiria kwenye maeneo hayo. Wakazi hao wanasema hata Sumatra wenyewe wanadai wamepewa maelekezo kutoka ofisi kubwa ili kuyaondoa mabasi haya kabla ya muda wake.

Hali ya usafiri katika maeneo haya ni mbaya sana, kwasababu kwanza nauli ni kubwa sana halafu watu wa mbezi wanalipa nauli mara mbili kwenye mabasi ya mwendokasi.

Nauli za mwendo kasi kwa sasa ni Tshs. 650 kituo hadi kituo lakini abiria wanalipa Tshs. 700 kwa kisingizio kwamba wahudumu wa Mwendokasi hawana chenji ya Tshs.50, kwahiyo kiuhalisia nauli ya mwendokasi ni Tshs. 700 kituo hadi kituo na Tshs. 200 kwa wanafunzi.

Lakini kwa wakazi wa Mbezi nauli ni mara mbili ya hii na usumbufu juu.

SUMATRA hata kama mmepewa maelekezo ya Ofisi ya juu kwahiyo mnafurahia wananchi ya maeneo hayo wanavyopata shida sio?

Poa tu Mungu yupo atawatendea wananchi wa Ubungo, Kimara na Mbezi kulingana na mapenzi yake.
Wakaombe usafiri huko walikopeleka kura zao period!!
 
Back
Top Bottom