Rais Magufuli atengua uteuzi wa Balozi Alphayo Kidata, amwondolea hadhi ya Ubalozi!

Who knows kama kamuita ili aje ampe ubunge na uwaziri hapo hapo wa fedha na amvue Waziri na ubunge mtu ambae kawa mkweli kuhusu hali ya sasa serikalini. Time will tell
Kulikua na haja gani ya kumuondolea hadhi ya Ubalozi?Kwani hauwezi kuwa hadhi ya ubalozi na Ubunge?BTW nafasi za kuteua Wabunge zilishaisha.Huyu amerudishwa kwa misconduct
 
Mzuqa

Kwanza una advantage una "perfect genes" ya kabila pendwa na asili yako vilevile ni kutoka hukohuko kanda pendwa.

Kuna nafasi imeachwa waz Toronto. Endeleza kusifu ikiwezekana kwa siku posti thread humu si chini ya 10 zikimsifu malaika mkuu na toto lake pendwa

Isitoshe piga juju kwa sana tuu kwa kutembelea masangoma namajungu juu.

Kila la kheri
Kwanini Manenepa a. k. a makond boy asipelekwe?
 
Rais John Magufuli ametengua uteuzi na kumrejesha nchini aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada, Alphayo Kidata pia ameondolewa hadhi ya Ubalozi

View attachment 926728


MY TAKE:

Ndugu Kidata ni mzaliwa wa wilaya ya Bunda, mkoani Mara, A-Level kasoma HGE Songea Boys High School pamoja na Mheshimiwa Kangi Lugola, akaajiriwa Idara ya Mahakama mkoani Tabora, baadaye akajiunga na UDSM kuchukua BA ya Economics, mwalimu wake akiwa ni Prof. Lipumba, Prof. Benno Ndulu pamoja na Dr. P. Mpango.

Baada ya Kumaliza UDSM alijiunga na wizara ya Ardhi idara ya Uchumi na Mipango(Mtumishi wa Umma-WIZARA YA ARDHI, Nyumba na Maendeleo ya Makazi-IDARA YA MIPANGO-AFISA BAJETI WA WIZARA) ambako alijiendeleza kimasomo ya uchumi huko Japan akahitimu Masters Degree, hatimaye akarudi nchini na kushika nyadhifa mbalimbali serikali.

Awali alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, akateuliwa kama Kamishina Mkuu wa TRA ambapo hakudumu sana akapelekwa kuwa Katibu Mkuu Ikulu ambapo ndani ya miezi kadhaa akateuliwa kuwa Balozi 10 Jan 2018 hatimaye tarehe 05 Nov 2018 Katumbuliwa na kushushwa chini mavumbini.

Sitashangaa akipandishwa Kizimbani Kisutu kwa kesi isiyo na dhamana ya Uhujumu Uchumi na kutakatisha fedha.

Novemba hii ilikuwa tupokee Ndege 3 kubwa, Mbili aina ya Bombardier CS300 kutoka Canada na Moja Boeing 787-8 Dreamliner kutoka Marekani. Sijajua kwanini ndege haijaja badala yake kaja Kidata.


Habari zaidi, soma=>Ikulu, Dar: Rais Magufuli awaapisha Alphayo Kidata na Msalika Makungu - JamiiForums
Magu hanaga mzaa jamani. kuweni makini
 
Those myopic many others
Funny,hivi ni nani myopic,mimi au wewe?Magufuli anayofanya ndiyo wengi tuliyokuwa tunayataka,tunamuombea akaze uzi.The problem is, wengi hatukujua he would go this far.Tulidhani hatafukua makaburi na kuzuia aina zote za uovu na ulaji,tumeliwa.Magufuli go,go,go mpika upinzani warudi kijijini wakalime.Wanapewa ruzuku halafu wanatafutia vimada na kufanyia starehe,aibu sana.
 
Nimekuja kugundua asilimia kubwa ya watu umu jamii forums awaelewi uandishi wa pascal, kwa kifupi yule jamaa sio mtu wa kujikomba sema kama sio great thinker uwezi muelewa milele.
 
Funny,hivi ni nani myopic,mimi au wewe?Magufuli anayofanya ndiyo wengi tuliyokuwa tunayataka,tunamuombea akaze uzi.The problem is wengi hatukujua he would go this far.Tulidhani hatafukua makaburi na kuzuia aina zote za uovu na ulaji,tumeliwa.Magufuli go,go,go upika upinzani warudi kijijini wakalime.Wanapewa ruzuku wanatafutia vimada na kufanyia starehe,aibu sana.
Uovu upi unaozungumzia? Ikiwa 1.5 trillion haipo na biashara ya uchaguz na manunuzi inashamiri unapata wapi ujasir wa kuandika hizi takataka kaa kimya kama hujui mambo.
 
Funny,hivi ni nani myopic,mimi au wewe?Magufuli anayofanya ndiyo wengi tuliyokuwa tunayataka,tunamuombea akaze uzi.The problem is wengi hatukujua he would go this far.Tulidhani hatafukua makaburi na kuzuia aina zote za uovu na ulaji,tumeliwa.Magufuli go,go,go upika upinzani warudi kijijini wakalime.Wanapewa ruzuku wanatafutia vimada na kufanyia starehe,aibu sana.
Rubbish, wengi na nani? Avoid sweeping statements
 
Kidata ni mwizi mla rushwa, alijengewa nyumba na mafisadi, alikuwa na kiburi akijiaminisha uaminifu aliopewa, nadhani sasa atafilisiwa abaki kama alivyozaliwa au awe kama Wage yule DT wa Bwagamoyo aliyefilisiwa mpaka kakimbiwa na mkewe

Roho mbaya itakuua ndugu
 
Mimi naomba hiyo nafasi ya Toronto apewe lemutuz a.k.a libaharia jamani khaaaa! Degree 3 kabsa anafaa Sana!
 
Back
Top Bottom