Rais Magufuli ashiriki ibada katika kanisa la Antoni Lusekelo, atoa ahadi ya barabara

Jumapili hii Rais Magufuli amehudhuria ibada katika Kanisa la Mchungaji Lusekelo maarufu kama "Transfoma" au "Mzee wa Upako" eneo la Ubungo-Kibangu

Hii ni kama "desturi" aliyoanza kujiwekea kwa kusali katika makanisa ambayo siyo dhehebu lake,mara ya mwisho Rais alijumuika na waumini wa kanisa la KKKT usharika wa Azania Front

Tunasubiri kupata ujumbe wa Jumapili na neno la heri kwa Watanzania kupitia "homilia" ya Rais kwa waumini wa Mzee wa Transfoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amelitembelea Kanisa la Maombezi linaloongozwa na Mchungaji Antony Lusekelo (Mzee wa Upako) lililopo Ubungo Kibangu Jijini Dar es salaam na kuwaahidi waumini wa kanisa hilo kuwa Serikali yake itatengeneza barabara ya kutoka Ubungo Kibangu hadi River Side ambako itaungana na barabara ya Mandela.

Rais Magufuli ambaye amezungumza katika ibada ya asubuhi ya Kanisa hilo iliyofanyika leo tarehe 05 Juni, 2016 amesema amepita katika barabara hiyo ambayo imekuwa ikitumiwa na waumini wa kanisa hilo na wananchi wengine wa eneo la Ubungo Kibangu kwa lengo la kujionea hali halisi.

Aidha, Rais Magufuli amempongeza Kiongozi wa Kanisa hilo Mchungaji Antony Lusekelo maarufu kwa jina la Mzee wa Upako kwa huduma ya maombezi anayoitoa kwa waumini wake na watazamaji wanaofuatilia vipindi vyake vya Mahubiri kupitia Luninga.

“Mimi ni mfuatiliaji mzuri sana wa mahubiri yako, kwa hiyo mahubiri unapoyatoa yanasambaa, kwa kweli mimi na familia yangu huwa yanatubariki sana, kwa hiyo nataka kukuthibitishia ninakupenda sana.

“Ndio maana kuna siku moja, ulizungumza kuhusu shida ya barabara yako ikabidi nitafute mbinu za namna gani tunaweza kuishughulikia kwa utaratibu ulio wazi, nikamtuma meneja wa barabara wa Mkoa wa Dar es salaam, akaja, akaipitia na akafahamu changamoto zilizopo, akafanya upembuzi yakinifu na usanifu, nataka kukuthibitishia kuwa fedha za kutengenezea barabara hii zipo” Amesema Dkt. Magufuli huku akishangiliwa na waumini.

Kwa upande wake Kiongozi wa Kanisa la Maombezi Mchungaji Antony Lusekelo (Mzee wa Upako) amemshukuru Rais Magufuli kwa kulitembelea kanisa hilo, na amemuombea heri katika uongozi wake ili aweze kufanikisha azma ya kuliletea taifa maendeleo ikiwemo mpango wa kuanzisha viwanda.

Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Jambo jema kwa kiongozi was nchi kujumuika na waumini ..Hakika Tanzania INA Rais Makini.
 
Waislamu wanaanza mfungo mtukufu wa ramadhani kama anawapenda ashiriki nao pomoja,kwa kufanya hivyo atapata thawabu kwa mungu.
 
Mbona kazungumzia issue ya barabara??? Hiyo nayo Ni kusali??? Angeongea mambo yanayohusiana na imani/dini,,eg.watu waache kutenda dhambi nk. Sasa yeye kuanzisha mambo ya barabara,, Kama si kujitafutia umaarufu Ni nini???? Anapenda mno camera aisee!!!mno mno mno...
CHA ajabu ni nini? Anajumuika kusali popote kama mahali hapo hapana kanuni za kuzuia mtu kusali kama si muumini wa hapo.Ni utaratibu mzuri Rais kujumuika kumuomba Mungu na raia wake.
 
Hahaaa siasa zinawatoa watu ufahamu sana, kuna watu humu wana kazi ya kupinga kila kitu afanyacho Magu kisa siasa au wametumbuliwa. Hadi miaka yake 10 iishe mtakufa kwa pressure, halafu anaingia Majaliwa mwendo unabaki ule ule for another 10 yrs, aahaaa kazi mnayo.

Ila kwa ushauri tu mngebadilika tu hakuna namna, ya kale mnayoyataka hayawezekani tena TZ hii. Kuishi kwa dili dili acheni hakuna namna tena, mtaendelea kulia lia bure wakati hakusaidii kitu
Miaka kumi? hiyo mitano yenyewe kuimaliza kwa mwendo huu ni hatihati!
 
Hapo Mzee wa Upako ataandaa special program ya kumsifia na kumtetea MAGUFULI kwenye kila jambo, liwe zuri au baya!
 
Jumapili hii Rais Magufuli amehudhuria ibada katika Kanisa la Mchungaji Lusekelo maarufu kama "Transfoma" au "Mzee wa Upako" eneo la Ubungo-Kibangu
1465132528859.jpg

Hii ni kama "desturi" aliyoanza kujiwekea kwa kusali katika makanisa ambayo siyo dhehebu lake,mara ya mwisho Rais alijumuika na waumini wa kanisa la KKKT usharika wa Azania Front

Tunasubiri kupata ujumbe wa Jumapili na neno la heri kwa Watanzania kupitia "homilia" ya Rais kwa waumini wa Mzee wa Transfoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amelitembelea Kanisa la Maombezi linaloongozwa na Mchungaji Antony Lusekelo (Mzee wa Upako) lililopo Ubungo Kibangu Jijini Dar es salaam na kuwaahidi waumini wa kanisa hilo kuwa Serikali yake itatengeneza barabara ya kutoka Ubungo Kibangu hadi River Side ambako itaungana na barabara ya Mandela.

Rais Magufuli ambaye amezungumza katika ibada ya asubuhi ya Kanisa hilo iliyofanyika leo tarehe 05 Juni, 2016 amesema amepita katika barabara hiyo ambayo imekuwa ikitumiwa na waumini wa kanisa hilo na wananchi wengine wa eneo la Ubungo Kibangu kwa lengo la kujionea hali halisi.

Aidha, Rais Magufuli amempongeza Kiongozi wa Kanisa hilo Mchungaji Antony Lusekelo maarufu kwa jina la Mzee wa Upako kwa huduma ya maombezi anayoitoa kwa waumini wake na watazamaji wanaofuatilia vipindi vyake vya Mahubiri kupitia Luninga.

“Mimi ni mfuatiliaji mzuri sana wa mahubiri yako, kwa hiyo mahubiri unapoyatoa yanasambaa, kwa kweli mimi na familia yangu huwa yanatubariki sana, kwa hiyo nataka kukuthibitishia ninakupenda sana.

“Ndio maana kuna siku moja, ulizungumza kuhusu shida ya barabara yako ikabidi nitafute mbinu za namna gani tunaweza kuishughulikia kwa utaratibu ulio wazi, nikamtuma meneja wa barabara wa Mkoa wa Dar es salaam, akaja, akaipitia na akafahamu changamoto zilizopo, akafanya upembuzi yakinifu na usanifu, nataka kukuthibitishia kuwa fedha za kutengenezea barabara hii zipo” Amesema Dkt. Magufuli huku akishangiliwa na waumini.

Kwa upande wake Kiongozi wa Kanisa la Maombezi Mchungaji Antony Lusekelo (Mzee wa Upako) amemshukuru Rais Magufuli kwa kulitembelea kanisa hilo, na amemuombea heri katika uongozi wake ili aweze kufanikisha azma ya kuliletea taifa maendeleo ikiwemo mpango wa kuanzisha viwanda.

Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
 
Sijaona mantiki ya msigwa kutumia headed paper ya ikulu kwa kutoa habar. Hio kuwa kama ya kitaifa wakati ni personal event za raisi.
 
hivi itakuwa Mzee Wa upako aligusiwa kidogo ujio wake? au amestukia tu!!
 
Back
Top Bottom