Rais Magufuli amteua Humphrey Polepole kuwa Mkuu wa Wilaya ya Musoma

Kama wanaojiita wazalendo wanaishia kupewa chochote, tunawafundisha nini vijana wetu kuhusu UZALENDO!!!
 
hapo ndo utajua kuwa ccm ni ileile




ila jpm afanye kumkumbuka kijana mwenzetu humu jamvini mtela mwampamba maana kasahaulika sana kafulia hata bando la jf na fb anakosa
 
Tulishaeleza tangu awali kuwa Pole pole anatembea na ahadi kichwani.
Namsubiri aanze kuikana Rasimu ya Katiba aliyoshiriki kuiandika na kuitetea kwa nguvu zote na kukubaliana na Katiba Pendekezi ambayo alikuwa anaipinga hadharani.

Waswahili walinena "Uzao wa kenge hauwezi kuwa Mamba asilani"
 
Ukimtazama kwa jicho la kisiasa Polepole hutoweza kuona kilicho ndani yake. Kilichombeba Polepole ni kuonesha anasimamia anachokiamini pasipo kujali atatukanywa kiasi gani.
 
Musoma wamekutana wajuaji watupu! Ajiandae kupambana na Mulongo! Hatakubali kufunikwa! Tusubiri!!

Acha kupotosha kwani kila mtu ana job description yake hivyo hakuna kufunikana na hata hivyo hata iweje kiitifaki Hamphrey Polepole 100% anawajibika kwa Mkuu wake wa Mkoa Magesa Mulongo ila kama Mkuu huyo wa Mkoa atapata udhuru wowote basi Majukumu ya Mkuu wa Mkoa atakuwa nayo Poleple.
 
Naona wachangiaji wengi wanaongozwa na hisia bila kuangalia uwezo wa nafasi aliyopewa kama anaimudu. Wengine hatuna mlengo wa kisiasa kwa hiyo mnatuchanganya na kutuletea uccm na uchadema... Tunahitaji kujua nafasi aliyopewa na nature ya eneo je ana fit
 
Back
Top Bottom