Rais kuwa makini na Waziri huyu, atakupeleka pabaya

Sasa kuna hii kombinenga Hatari inasumbua Bunge na kamati zao za Ufundi walizorithishwa na mkuu wa makati ya Ufundi Afrika Yaani January Makamba , hao si wengine bali ni Mwakyembe , kitwanga na Nape Huku January akiratibu kila mtumbuliwa JIPU au wale wanaotarajia kutumbuliwa JIPU mda wowote na kujipatia pesa Kwa style alivyomfanyia Yule Mzungu mtaliano ( kufa kufaana ) Kipindi hiki ni Mavuno Kwa January .
 
Napenda sana watu wanaokwenda moja kwa moja kwenye ukweli bila kutafuna tafuna maneno kama wewe.

Asichokijua mleta uzi ni ukweli kwamba Nape hana ubavu wa kuzuia TBC kuonyesha live mikutano ya bunge. Kwa tunaomjua Nape, tatizo lake kubwa ni kiongozi asiyekuwa makini hasa kwenye kauli zake lakini ni muwazi asiyependa kuficha ficha na kufanyia mambo gizani.

Isipokuwa najua katika hili tutamlaumu na kumbebesha bure Nape mzigo huu na hawezi kusema ametumwa lakini ukweli ni kwamba anatekeleza kile alichoagizwa na bosi wake Magufuli afanye.
Nape katumia kile kile kivuli cha kubana matumizi , Yaani amejua kuwa Magufuli anapenda kubana matumizi sana akajua akienda na wazo la luzuia Live Kwa kisingizio cha kubana matumizi Magufuli ataingia line, lakini Nadhani Magufuli anafika JF akisoma maoni ya wana JF atashituka na kuja na mbinu mpya .
 
Mhe Rais, Tafadhali siku yoyote wakati wowote ikikupendeza, naomba usome ushauri wangu na ikikupendeza zaid ufanyie kazi.
Mimi ni miongoni mwa watanzania uliowaomba wakuombee,lkn kila nikiomba naona giza lmetanda bungeni na giza hlo linaonekana kwa wazir wako.
Kabla sjaendelea zaidi, naomba ninukuu mandiko matakatifu kutoka katika kitabu cha nabii isaya.
"Ondoka, uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja, Na utukufu wa Bwana umekuzukia.
2 Maana, tazama, giza litaifunika dunia, Na giza kuu litazifunika kabila za watu; Bali Bwana atakuzukia wewe, Na utukufu wake utaonekana juu yako.
3 Na mataifa wataijilia nuru yako, Na wafalme kuujia mwanga wa kuzuka kwako.
4 Inua macho yako, utazame pande zote; Wote wanakusanyana; wanakujia wewe; Wana wako watakuja kutoka mbali. Na binti zako watabebwa nyongani.
5 Ndipo utakapoona na kutiwa nuru, Na moyo wako utatetemeka na kukunjuka; Kwa kuwa wingi wa bahari utageuzwa kukujia, Utajiri wa mataifa utakuwasilia."
Mhe. Rais uwepo wa mawazir wako bungeni ni uwepo wa serikali yako. Wewe Rais wa Jamuhur ya Muungano wa Tanzania, umeapa kuwatumikia wananchi. Umeapa kurudisha heshima ya serikal, unahitaji viongozi watakaokusaidia kutimiza dhamira hiyo ya dhati uliyonayo.
Mhe Rais, wewe umetokana na kura za watanzania, wabunge pia wametokana na kura za wananchi,kwa sasa wanashauku ya kukusikia kila wakati unapoongea au kutoa hotuba kwan hotuba zako zmejaa matumaini kwao, wananchi pia wanashauku ya kuona wabunge wao jinsi watakavoibana serikali ,wanataka kuona dhamira yao katika kukusaidia wewe katika kutekeleza dhamira yako njema ikiwa ni kufichua maovu ili wakusaidie katika dhana ya UTUMBUAJI MAJIPU.kukusaidia hakumaanishi kukusifia kila wakati, hakumaanishi kuficha maovu katika serikali na kutangaza mema tu, kunamaanisha kukukosoa pale unapokosea na kukushauri pale ulipoteleza.serikali yetu inautaratibu tuliojiwekea ni vema kila mmja wetu akatumia utaratibu huo, kanun na sheria zilizopo kutekeleza majukumu yake.

Mhe.Rais sijui ni wazir gan huyu aliyetandwa na giza katika serikali yako, sijui ni kwa nn anataka kuwaweka wananchi katika giza, anataka kuwanyima wananchi unaowatumikia kuwasikia na kuwaona wawakilishi wao wakitimiza majukumu yao bungeni.Hawa wawakilishi ndio wasemaji wa wananchi, ndio wanataka kuona serikali yako inawajibika,wanataka kuona, kusikia na kuhisi mabadiliko kupitia kwa wawakilishi wao, lakin wananyimwa Uhuru huo, anayewanyima ni wazir wako, ni serikali yako.
Huyu anayetaka wananchi wawe katika giza amebeba uovu, huyu ni wazir wa kumwangalia kwa makin,huu uovu lazima uutoe mapema ni vema ukaukemea wakati haujakomaa, ukikomaa utaota mizizi.
Huyu huyu naiman ndiye mmoja wapo aliyekuletea mgogoro na mashirika ya misaada ya kimataifa, usipokuwa makini atakuweka katika mgogoro wa kidemokrasia ndan ya nchi na hata na mataifa mengine.
mhe Rais kama shinikizo la kutoonesha bunge live halijatokea kwako na halitokei kwako Tafadhali tafakar ushauri wangu kwa kina na hasa rejea nukuu ya mandiko matakatifu niliyoyaweka.
Hii ngoma unaicheza wewe na wewe ndiye mpiga ngoma.udharimu mwingi dhidi ya wananchi umefanywa na mfumo ulionao na mawazir wako wanatoka katika mfumo huo, tazama sana wasikugombanishe na
wapinzani. Waogope wasaidiz wako wanaofanyia sifa, wanaotaka wafiche maovu na mazur tu yaonekane, hakika nakwambia ukiwaendekeza viongozi wa namna hii, siku akitokea mtu akafunua makabur hayo, uchafu huo,wana wa nchi hii hawatakusamehe.
Mungu akuongoze katika kuwatumikia watanzania kwa moyo wa dhati.Watu wote wanatumain utawatoa katika giza na kuwapeleka katika nuru. Wazir huyu hafai kuwa katika nuru unayoitafuta.

Namaliza kwa nukuu kutoka katika kitabu hcho hcho cha Isaya.
Isaya anasema"Watu wako naona watakuwa wenye haki wote,nao watarithi nchi milele,mdogo atakuwa elfu,na mnyonge atakuwa taifa hodari,mimi bwana nitayahimiza hayo wakati wako."
Mungu ibariki Tanzania na Watu wake.
Acha unafiki unafiki wewe. Kama kweli wataka kumsaidia Rais basi ungemwambia huyo waziri ni yupi na kafanya nini? Kuwa Transparency
 
Acha unafiki unafiki wewe. Kama kweli wataka kumsaidia Rais basi ungemwambia huyo waziri ni yupi na kafanya nini? Kuwa Transparency
Tatizo unatoa maoni bla kusoma na kuelewa vizur, ndo maana ni jukwaa la great thinkers, ungesoma ungejua hyo wazir ni nan na kafanya nn
 
Nishasema mara nyingi tu, madikteta hawataki kukosolewa. Wanachotaka ni kusifiwa tu. Wabunge wa UKAWA hawana tabia ya kuremba wanapoona kuna tatizo, daima wao husema ukweli, na hili ndilo linalosababisha huyu jamaa kuzuia Bunge kuoneshwa live.
 
Nape ndiye wazir wa habari, ndiye aliyepeleka hoja yaya kusitisha matangazo ya bunge live, anasema usitishwaji wa matangazo ilikuwa ni maamuzi ya bunge. Pole pole IPO siku atasema alpokea amri kutoka juu.
 
Mwandishi umeeleweka vyema na ushauri wako ndio ni muhimu sana katika kuendeleza sifa njema za raisi wa sasa. Umezungumza bila hiyana za vyama ndio maana wapo wasiokuelewa, maana wao mawazo yao yanawaza ushabiki wa kisiasa tu na si maendeleo ya taifa.
 
Napenda sana watu wanaokwenda moja kwa moja kwenye ukweli bila kutafuna tafuna maneno kama wewe.

Asichokijua mleta uzi ni ukweli kwamba Nape hana ubavu wa kuzuia TBC kuonyesha live mikutano ya bunge. Kwa tunaomjua Nape, tatizo lake kubwa ni kiongozi asiyekuwa makini hasa kwenye kauli zake lakini ni muwazi asiyependa kuficha ficha na kufanyia mambo gizani.

Isipokuwa najua katika hili tutamlaumu na kumbebesha bure Nape mzigo huu na hawezi kusema ametumwa lakini ukweli ni kwamba anatekeleza kile alichoagizwa na bosi wake Magufuli afanye.
Duuh! Mkuu kama ni kweli basi kuna tatizo kubwa sana.
 
Huyo unayemuomba ambane waziri wake ndio aliyeshika remote, ndio anabidilisha channel. Huyo waziri hana lolote analopanga zaidi ya kuitikia Naam bwana. Naona unajua kabisa anayetaka bunge lisionyeshwe lakini unatumia lugha ya staha tu ili asione kama watu tumejua yeye ndio yuko nyuma ya amri hiyo. Dunia hii ambayo hata mtoto wa darasa awali anajua kutumia vyombo vya mawasiliano wewe unajadili mambo ya nchi kwenye giza. Na wakati huo huo tunajua mikataba mingi ya kihuni imeingiwa kwenye sirisiri hivihivi na waliotungiza kwenye mikataba hiyo ndio hao hao leo wanataka bunge lifanye kwa siri. Tumeshaumwa na nyoka tukiona unyasi ......
Watanzania mbona tunajifanya vipofu na viziwi hivi nchi gani duniani inayoonyesha mijadala ya bunge live muda wote.mbona mnang"ang"ania vitu vya ajabu.unoko tulionao au nini
 
Wewe ndo hjasoma na kuelewa nilichoandika, au kwa vile sikumtaja jina? Sifa za matendo niliyoyataja ndo njia pekee ya Rais kumtambua.
Unajifanya utabiri hakuna wewe ni ukawa sifa mlizozita kupitia tv hazipo sasa mtaipata
 
Umesema awe makini na 'waziri huyu'

halafu unasema 'hujui waziri gani'

so inawezekana hujui hata ni waziri au naibu au katibu wa wizara?
Kwani wewe ni kibogoyo!!? Tafuna na ku"vunja mifupa kungali meno bado iko"(kwa sauti ya samba mapangala)
 
mataputapu mabaya tumia bia mkuu halafu uwe unakula vizuri kabla ya kupost.
 
Hii ni moja ya mada kipumbavu na kinafiki kuwahi kuwa hapa jamiiforum, Ni ujinga kumlaumu Nape juu ya hili, kutoonyeshwa bunge live ni matakwa ya raisi na ili aonekane yeye tu, hajiamini nini sijui
 
Back
Top Bottom