Rais kuapisha wateule wake wa katiba kesho tar 13/04/2012 dar

dosama

JF-Expert Member
Dec 25, 2010
912
957
Source Kutoka Bungeni

Ndo mkuu wa kaya kesho anawapa meno wateule wake michango yetu hapa jamvini imesaidiaje? Na kwa ujumla wake tumepigwa changa la macho kwasababu tuliambiwa ataapisha mwisho wa mwezi ili kutoa nafasi ya watu kuichambua wataule wake imeukuwaje sasa
 
Hawa wasaidizi wa Mkulu wanakosa kumbukumbu au ni wasahaulifu sasa. Siku chache zilizopita walidai shughuli hiyo imesogezwa mbele hadi mwisho wa mwezi kwa madai kuwa baadhi ya wateule walikuwa safarini nje ya nchi na kwamba maandalizi makubwa yalihitajika ili Wajumbe wakishaapishwa kusiwe na muda mrefu wa kusubiri kuanza kazi.

Inawezekana hapakuwepo mawasiliano
sahihi kati ya "Mkulu" na "wasaidizi wake" au pengine waliokuwa safari wamerejea na maandalizi mengine yamekamilika.

Haya, kila la heri wajumbe wateule, tunasubiri mwongozo wenu wakati wa safari yetu ya kutoa maoni na hatimaye kuandika Katiba mpya!
 
Back
Top Bottom