Rais Kikwete, Watanzania wana imani na wewe achana na hoja dhaifu za Chadema

na huyu ndio Rais anayeongoza barani africa kwa kusafiri nchi za nje kuliko marais wengine
 
.....Watanzania bado wana imani kubwa na Rais Jakaya Kikwete, kuna baadhi ya watu ambao wanaishambulia serikali ya JK kuwa kuna ufajaji wa fedha za umma, ufajaji wa fedha za umma kwa vigogo wa serikali hayakuanza leo bali tangu serikali zilizopita.

Umesahau rekodi ya kuwapa UDC mahawara zake!!

Kororoka usiku kwenda mahotelini kulala na mahawara zake!!

Kuchekacheka misibani!!

Mfumuko wa bei!!

DHAIFU!!

Huyu ni Great Thinkers wa Chadema-Kata.
 
Kama una ushahidi wa huo wizi, unangoja nini kuwashtaki? unangoja aje Rais kuwashtaki? Vituo vya Polisi hujui vilipo? amma kweli.

Polisi gani? Policcm? Polisi wanahongwa na wenye pesa kukandamiza wasio na kitu? Hasiye na kitu, hana chake polisi!

Hakuna pa kukimbilia zaidi ya kuitoa CCM na kusuka upya mfumo wa utawala na uwajibikaji katika utumishi wa umma.
 
Kama huyawezi hayo, mtume Rais kivuli akakusaidie.
 
Kama huyawezi hayo, mtume Rais kivuli akakusaidie.

Ushasema rais kivuli - hasiye na madaraka kamili kama rais mwenyewe.
Sasa huyo kivuli atafanya nini kama rais mwenyewe mwenye makali na madaraka yote kunyoosha watumishi wa umma anashindwa?!

Chifu rais ni mchemsho - amechemsha na anazidi kuchemsha kila kukicha. Ashukuru watanzania wengi bado wapo kwenye giza, la sivyo...
 
ubora wa kiongozi haupimwi kwa ujenzi wa barabara, zahanati,shule nk haya ni majukumu ya msingi ya serikali yeyote ile duniani. ubora wa kiongozi upimwa kwa uwezo wake wa kutimiza ahadi (Campaign promises), walk the talk.
 
Ushasema rais kivuli - hasiye na madaraka kamili kama rais mwenyewe.
Sasa huyo kivuli atafanya nini kama rais mwenyewe mwenye makali na madaraka yote kunyoosha watumishi wa umma anashindwa?!

Chifu rais ni mchemsho - amechemsha na anazidi kuchemsha kila kukicha. Ashukuru watanzania wengi bado wapo kwenye giza, la sivyo...

Alieshindwa ndio mwenye madaraka anaeweza ndio hana madaraka! kwi kwi kwi teh teh teh.
 
Alieshindwa ndio mwenye madaraka anaeweza ndio hana madaraka! kwi kwi kwi teh teh teh.

Huyu ameshaonekana ameshindwa mazima...hana namna ya kujitetea wala kukikimbia kivuli chake cha kushindwa..
 
Na marais wote waliomtangulia katika suala la uwajibikaji na nidhamu kwa watumishi wa umma

Kwa mara ya kwanza Tanzania katika utawala wa Jakaya Mrisho Kikwete imejipatia tuzo za Kimataifa za utawala bora, demokrasia na nyinginezo:

"United Nations Foundation wametupa tuzo ijulikanayo kama “2011 Social Good Award” kwa kuendeleza midia jamii na kutumia teknolojia ya kisasa kukabili changamoto za maendeleo ikiwa ni pamoja na huduma ya afya ya kina mama. Pili,tumepewa tuzo ya the South-South News Award kutokana na mafanikio tunayoyapata katika kuboresha afya nchini na kwa kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano kwa ajili hiyo. Pia, kwa kutambua mchango tunaoutoa kwa maendeleo ya dunia. Na tatu, kutoka Soko la Mitaji la NASDAQ tumepewa tuzo kwa kutambua mchango wangu na mafanikio tunayoyapata katika kupunguza vifo vya kina mama na watoto."

Umeshaziona hizo Tanzania hii kabla ya Kikwete, hususan hiyo ya utawala bora? Bila "nidhamu kwa watumishi wa umma" utapewa hiyo?

Kikwete hakisii, anafanya kweli, na kwa hilo la "nidhamu kwa watumishi wa umma", si mimi nnaesema hayo, ni Mataifa yaliyoipa Serikali yake tuzo ya utawala bora. Kuna uongozi wa Rais wa kabla yake uliopata hiyo tuzo au ya Umoja wa Mataifa au japo inayofanana nayo?
 
Ritz,

Kwa hayo hayo ndio Kikwete hapendeki. Ukitazama wengi wa wanaoleta chuki na kejeli utakuta wengi ni wale wale waliozibiwa mianya ya wizi kwa mara ya kwanza toka hii nchi ipate Uhuru katika kipindi hiki cha Kikwete.

Baada ya muda mfupi, Kikwete anaanza kushughulikia fedha zilizowekwa nje ya nchi na hawa wizi wa mali za umma. Ni kazi ngumu sana, lakini ipo njiani inakuja, tutaona chuki zikizidi. Ukitazama kijuu juu tu hata bila ya uchunguzi wa kina utakuta wote wenye chuki ni wale wale 83%. Hao ndio "wasomi" bila kuelimika, hao ndio walioifikisha nchi ilipofika na hao ndio wezi wakubwa.

Tunamtakia kila la heri Kikwete kwa hii kazi ngumu aifanyayo sasa, na matokeo tunayaona. Na hapo ndiyo eti "dhaifu".

Subiri uone majibu sifuri sasa hivi.

Mkuu kama kweli alishindwa kushughulikia maswala ya EPA na KAgoda sidhani kama ataweza kushughulikia swala la akaunti za uswisi, tena inawezekana yeye ni mmoja wa waliweka fedha hizo huko uswisi. Kikwete atendelea kuongoza hadi muda wake utakapokwisha simple because mtaji wa CCM ni mkubwa, kama unakumbuka Profesa Baregu alitaja vizuri kuwa CCM ina mtaji wake inaotegemea.
 
Kwa mara ya kwanza Tanzania katika utawala wa Jakaya Mrisho Kikwete imejipatia tuzo za Kimataifa za utawala bora, demokrasia na nyinginezo:

"United Nations Foundation wametupa tuzo ijulikanayo kama “2011 Social Good Award” kwa kuendeleza midia jamii na kutumia teknolojia ya kisasa kukabili changamoto za maendeleo ikiwa ni pamoja na huduma ya afya ya kina mama. Pili,tumepewa tuzo ya the South-South News Award kutokana na mafanikio tunayoyapata katika kuboresha afya nchini na kwa kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano kwa ajili hiyo. Pia, kwa kutambua mchango tunaoutoa kwa maendeleo ya dunia. Na tatu, kutoka Soko la Mitaji la NASDAQ tumepewa tuzo kwa kutambua mchango wangu na mafanikio tunayoyapata katika kupunguza vifo vya kina mama na watoto."

Umeshaziona hizo Tanzania hii kabla ya Kikwete, hususan hiyo ya utawala bora? Bila "nidhamu kwa watumishi wa umma" utapewa hiyo?

Kikwete hakisii, anafanya kweli, na kwa hilo la "nidhamu kwa watumishi wa umma", si mimi nnaesema hayo, ni Mataifa yaliyoipa Serikali yake tuzo ya utawala bora. Kuna uongozi wa Rais wa kabla yake uliopata hiyo tuzo au ya Umoja wa Mataifa au japo inayofanana nayo?

Utawala bora Tanzania? What is your definition of utawala bora, kuna maendeleo gani ya IT tanzania ambayo serikali ya JK inaweza kupewa credit, hata kama yapo yamewasaidia watanzania wangapi?
 
Utawala bora Tanzania? What is your definition of utawala bora, kuna maendeleo gani ya IT tanzania ambayo serikali ya JK inaweza kupewa credit, hata kama yapo yamewasaidia watanzania wangapi?

Bongolander, Mnadanganywa na media za nje za Marekani n.k. , umesoma historia au ni hisia zako tu zinakutuma kuwa ni rahisi tu kurukia maendeleo? Natamani tukupe Uraisi mtu kama wewe uone watakachokufanya. Shida mnalalamika tuuu wa-=Tanzania lini mtakuwa na constructive ideas even if you are not happy? Semeni basi tunye nini solutions kwa nchi hii, mnabana kusema kwa faida ya nani? basi kama mna ideas na hamsemi mtakuwa walewale wanaotaka kufaidika binafsi na si kwa Taifa hili. Wengi mnataka kufanyiwa tuambieni mnafanya nini nyinyi wenyewe. Natamani 2015 ifike, na natamani Mungu atuweke hai wengi wenu, hakika hili ninalosema litathibitika, sio rahisi kutawala.
 
Utawala bora Tanzania? What is your definition of utawala bora, kuna maendeleo gani ya IT tanzania ambayo serikali ya JK inaweza kupewa credit, hata kama yapo yamewasaidia watanzania wangapi?

Wewe una macho au huna? hivi ingekuwa hakuna maendeleo ya IT sasa hivi tungekuwa hapa JF?

Halafu umesahau kuhusu kitu inaitwa "mkonga wa Taifa"? Hili la IT usiseme kijana, tuko mbali sana na tulipokuwa miaka 7 nyuma.
 
Mkuu kama kweli alishindwa kushughulikia maswala ya EPA na KAgoda sidhani kama ataweza kushughulikia swala la akaunti za uswisi, tena inawezekana yeye ni mmoja wa waliweka fedha hizo huko uswisi. Kikwete atendelea kuongoza hadi muda wake utakapokwisha simple because mtaji wa CCM ni mkubwa, kama unakumbuka Profesa Baregu alitaja vizuri kuwa CCM ina mtaji wake inaotegemea.

Kwanza EPA huijui, unaisikia tu. Walioweza kushtakika kwa EPA wameshtakika na wapo jela. Waliokuwa wanaijuwa vizuri sheria ya EPA wakatumia njia zote za kisheria mwanzoni kabisa (kabla hata hili sakata halijaibuliwa) na hao kisheria walikuwa hawana makosa na usingeweza kuwafunga wala kuwanyang'anya mali zao, yangekugeukia kama yalivyogeuka ya Dowans kwenye mahakama za Kimataifa. Kuna wapo ambao mpaka leo hiyo ndio biashara (kama EPA kwa majina mengine) yao kubwa. Ungekuwa una ufahamu kidogo wa "hedge accounting" ungenielewa nnasema nini. Mfano mzuri ni Mzee Sabodo (mfadhili wa Chadema na kada wa CCM), huyu ni mtaalaam wa biashara kama za EPA (hedge accounting) na anategeneza fedha nyingi sana Kimataifa, mpaka kesho.

Usione Mzee Sabodo kuwa anapoifadhili CHADEMA hajui anachokifanya, hiyo misaada kwa CHADEMA inatokana pia na uzoefu wake mkubwa wa "hedge accounting", anajuwa kutumia pande mbili zenye misuguano katika kujitengenezea yeye faida. Kama si kimapato basi hata kinadharia. Jee, hayo huyaoni?

Mara nyingi, huwa mnatumiwa na wanasiasa wachache wenye uchu wa madaraka kuaminishwa yasiyo kuwepo kwa kutumia yaliyokuwepo. Mfano mzuri ni huu wa EPA au Dowans. EPA ilikuwa ni biashara halali kabisa kama ilivyo kwa Dowans. Na waliofanya makosa (kinyume na sheria na makubaliano) kwenye EPA wako jela (kina Farijala Brothers, au hujui hilo?), waliofanya "transactions" za EPA kisheria hauna njia ya kuwafunga, hawana kosa, ukiwaburuza mahakamani kwa jazba tu, utaishia kuwalipa fedha nyingi sana, ujute. Kama ilivyo kwa Dowans, umekurupuka na kuwafungia mkataba wao, wakaenda mahakama ya kimataifa kama mikataba inavyosema, ukaamriwa kuwa unawalipa kila haki yao na ziada.

Kuhusu Kagoda. Hili lilijadiliwa bungeni, na ikaonekana pia kuna watu wanakurupuka, hawajui kinachoendelea. Wao hutafuta chochote na kukikuza waonekane kuwa wanafanya kazi nzuri sana, kijana hao hawana ila kujitafutia madaraka kwa utashi wao na njia zao na wanakutumia mtu kama wewe usiyependa kujifunza ukweli. Si umeona bajeti ya juzi walivyo aibika?
 
Utawala bora Tanzania? What is your definition of utawala bora, kuna maendeleo gani ya IT tanzania ambayo serikali ya JK inaweza kupewa credit, hata kama yapo yamewasaidia watanzania wangapi?

Kwa nini usiwaulize waliotoa tuzo kwa Serikali ya Tanzania ya awamu hii kuwa ni watawala bora, walitumia vigezo vipi?

Kwa upande wangu, ungejuwa jinsi Serikali ilivyokuwa inatenda kazi kabla ya Kikwete, kuanzia wakati wa Nyerere mpaka Mkapa, ungejuwa utawala bora ni nini.

Nakuuliza hivi, umeshawahi kukimbizana na gari ya kugawa chakula madukani bila kujuwa leo kutakuwa na unga, au mchele au sukari na au ukakaa foleni kuanzia saa 9 za usiku bila kujuwa leo utapata nini dukani? Ungeyawahi hayo, ungejuwa utawala bora ni nini.
 
Mara nyingi, huwa mnatumiwa na wanasiasa wachache wenye uchu wa madaraka kuaminishwa yasiyo kuwepo kwa kutumia yaliyokuwepo. Mfano mzuri ni huu wa EPA au Dowans. EPA ilikuwa ni biashara halali kabisa kama ilivyo kwa Dowans. Na waliofanya makosa (kinyume na sheria na makubaliano) kwenye EPA wako jela (kina Farijala Brothers, au hujui hilo?), waliofanya "transactions" za EPA kisheria hauna njia ya kuwafunga, hawana kosa, ukiwaburuza mahakamani kwa jazba tu, utaishia kuwalipa fedha nyingi sana, ujute. Kama ilivyo kwa Dowans, umekurupuka na kuwafungia mkataba wao, wakaenda mahakama ya kimataifa kama mikataba inavyosema, ukaamriwa kuwa unawalipa kila haki yao na ziada.

Duh! Sasa chifu, mbona rais Kikwete alisema watakaorudisha pesa za EPA atawasamehe?!
Kama ilikuwa biashara halali kulikuwa na haja gani ya rais kutoa kauli kama ile?!

Hao aliowasamehe rais ndiyo wako wapi vile?! Jela? Mtaani? TIB?!
 
Back
Top Bottom