Alfu Lela Ulela
JF-Expert Member
- Oct 29, 2010
- 1,255
- 77
Napata uchungu sana napoona serikali yetu ilivyo dhaifu, kiasi hata inashindwa kusimamia maagizo yake.
Serikali ilitoa agizo la kushushwa kwa bei ya mafuta. Tena agizo likasisitiza kuwa wafanyabishara wa mafuta watakaofunga vituo kwa kisingizio chochote watakiona.
Lakini wiki moja imekwisha bila agizo hilo kutekelezwa. Vituo vimefungwa na serikali badala ya kuchukua hatua eti inawaomba wamiliki wa vituo wapunguze bei.
Nimemsikia afisa mmoja wa EWURA akisema "tunatoa wito vituo vyote viuze mafuta." alitoa kauli hii baada ya kutembelea vituo tisa na kukuta ni vitatu tu vyenye kutoa huduma.
Hivi Serikali huwa inatoa wito au huwa inaagiza? Serikali inayoshindwa kutekeleza maagizo yake ni serikali ya hovyo sana.
Jamani, Serikali hii haina sababu ya kuendelea kuwepo.