Nyambala
JF-Expert Member
- Oct 10, 2007
- 4,465
- 1,170
Napata uchungu sana napoona serikali yetu ilivyo dhaifu, kiasi hata inashindwa kusimamia maagizo yake.
Serikali ilitoa agizo la kushushwa kwa bei ya mafuta. Tena agizo likasisitiza kuwa wafanyabishara wa mafuta watakaofunga vituo kwa kisingizio chochote watakiona.
Lakini wiki moja imekwisha bila agizo hilo kutekelezwa. Vituo vimefungwa na serikali badala ya kuchukua hatua eti inawaomba wamiliki wa vituo wapunguze bei.
Nimemsikia afisa mmoja wa EWURA akisema "tunatoa wito vituo vyote viuze mafuta." alitoa kauli hii baada ya kutembelea vituo tisa na kukuta ni vitatu tu vyenye kutoa huduma.
Hivi Serikali huwa inatoa wito au huwa inaagiza? Serikali inayoshindwa kutekeleza maagizo yake ni serikali ya hovyo sana.
Jamani, Serikali hii haina sababu ya kuendelea kuwepo.
Bei za mafuta haziwezi kushushwa kwa matamko, serikali lazima ishughulikie uchumi. Katika karne hii uchumi hauongozwi kwa matamko ya Nape NNauye na CCM! Ikiwa shilingi inadhoofika kila kukicha, waagizaji mafuta lazima wauze bei itakayowawezesha kuagiza stock nyingine.
Bei za mafuta hazifuati kodi tu, au bei iliyopo sokoni bali inatazama mwelekeo wa shilingi dhidi ya fedha za kigeni! Inachotakiwa serikali sio kutoa maagizo bali kushughulikia uchumi, kudhibiti mfumuko wa bei, na kuifanya shilingi stable ili waagizaji wa mafuta waweze kukadiria gharama na faida na hapo ndipo bei zita-stabilize.
Sasa matamko ya wakina Nape, kulazimisha serikali kushusha bei huku wakijua kuwa uchumi uko taabani matokeo yake ndiyo hayo! Total chaos! Watanzania tusikubali kudanganywa na matapeli wa CCM. Uchumi wa zamani wa Chama kushika hatamu na kutoa matamko hauwezekani tena kwa sasa!
Kiasi Fulani uko sawa,
Serikali ni ya CCM, sisiem imeilalamikia serikali kuhusu tatzizo la umeme, mwenyekiti wa sisiem ndiye rais wa Tanzania na ndiye Kiongozi mkuu wa serikali, na alikuwepo kwenye kikao hicho cha Kamati kuu ya CCM. Kazi ya chama ni kupanga sera ambazo serikali huzitekeleza, sera mbovu hudumuza uchumi.
EWURA ni mamlaka iliyo chini ya serikali, serikali ambayo inaundwa na CCM.Kodi zimezidi kwenye mafuta, kama ilivyo ada serikali kupitia TRA Kila mwaka imekuwa na tabia ya kupandisha PAYE, Kodi ya Magari, Kodi ya Mafuta, Sigara na Bia .Kwa Mtaji huu uchumi utakuwa kweli????
Rais yuko busy akizunguka zunguka uku na uko akiombaomba misaada, nchi haiwezi kuendelea kwa misaada!!
Wala wawekezaji!! hawa ni wanyonyaji tu.
Mliopo huko mjini hali ya mafuta leo asubuhi ni vipi?
mhhh......twende zetu kule kwenye tabia za wanyama mpenzi......hapa sio kabisa