Rais Kikwete, toa tamko kuhusu mafuta: Tunaumia wananchi!

Alfu Lela Ulela

JF-Expert Member
Oct 29, 2010
1,255
77
Napata uchungu sana napoona serikali yetu ilivyo dhaifu, kiasi hata inashindwa kusimamia maagizo yake.

Serikali ilitoa agizo la kushushwa kwa bei ya mafuta. Tena agizo likasisitiza kuwa wafanyabishara wa mafuta watakaofunga vituo kwa kisingizio chochote watakiona.

Lakini wiki moja imekwisha bila agizo hilo kutekelezwa. Vituo vimefungwa na serikali badala ya kuchukua hatua eti inawaomba wamiliki wa vituo wapunguze bei.

Nimemsikia afisa mmoja wa EWURA akisema "tunatoa wito vituo vyote viuze mafuta." alitoa kauli hii baada ya kutembelea vituo tisa na kukuta ni vitatu tu vyenye kutoa huduma.

Hivi Serikali huwa inatoa wito au huwa inaagiza? Serikali inayoshindwa kutekeleza maagizo yake ni serikali ya hovyo sana.

Jamani, Serikali hii haina sababu ya kuendelea kuwepo.
 
Mheshimiwa tunaumia sana, Ni aibu tupu huku mtaani, ajali mbaya zinatokea kutokana na magari kuzima yakiwa njiani kutafuta mafuta,

Mzee, mbona uko kimya, mbona U.S au U.K chochote kikitokea utaona mara moja Raisi anatolea ufafanuzi. TZ kuna nini?
Editor please send this message to top Leaders,


Kesho itakuwaje kwenda ofisini
 
kwa hiyo mkusanyiko uanzie wapi kesho?napendekeza viwanja vya gymkhana-nyuma ya zamani movenpick hotel
 
Unataka atoe malalamiko au tamko.

Hivi ulishaona mtu mlalamishi anakemea au kuwa na msimamo, msitegemee atoe tamko, akijitahidi sana atajitokeza na kulalamika, huku akidai anasikitishwa sana na hiii hali.

Mimi wala sitegemei jipya, yupo yupo tuu.
 
Ina maana hajasikia ynayotokea egypt,malawi na nchi zinginezo? Anafikiri yeye ni special saaana ee.
 
well,
nani kakuambia JK ana matatizo ya mafuta?
hii imekula kwetu na hakitoa kauli atasema '
WATU WANASEMA KUNA TATIZO LA MAFUTA, KWANI MIMI NI MUUZA MAFUTA? LINI NIMESEMA NINAMILIKI PETRO STATION HE HE HE HE HE HE,
SERIKALI HAINA VITUO VYA MAFUTA, HATA WAKATI WA NYERERE MIGOMO ILIKUWEPO, WAKATI WA MWINYI PIA, NA WAKATI WA MKAPA, SIO KULALAMIKA TU, UCHUMI WA NCHI UNAKUA NA NIMEJENGA BARABARA NYINGI KULIKO RAISI YEYOTE,
HACHENI KUTUMI MEDIA VIBAYA, TENA USIKUTE NYIE MANAOLALAMIKA NI CHADEMA MKIONGOZWA NA DR SLAA

mimi huyu raisi na serikali yake nilisha mtoa akilini sana hatakuletea magonjwa ya moyo tu
 
Nimemuona anafuturu na watoto yatima na leo yupo na mashekhe wengine wakila futari.......mambo mepesi mepesi
 
mhhh......twende zetu kule kwenye tabia za wanyama mpenzi......hapa sio kabisa

oh Yeeesss sugarpie ! Pls twende kule kwanza muda wenyewe ndiyo huu huku kwenye siasa stress tupu.

Ah kiongozi wangu!
Haya fuata ushauri wa Preta..
Tukutane kule kwenye Njiwa, Mende, Nyuki... lol

JouneGwalu,

Ha ha haaa,hata wewe mkuu? Haya natangulia kule mkuu....
 
Korogwe- Tanga petrol inauzwa in a black market Tshs. 2,500
badala ya Tshs. 1,950 kama serikali inavyotaka.
but none defend us.
Tanzania kwisha kabisa
 
Unataka atoe malalamiko au tamko.
Hivi ulishaona mtu mlalamishi anakemea au kuwa na msimamo, msitegemee atoe tamko, akijitahidi sana atajitokeza na kulalamika,
huku akidai anasikitishwa sana na hiii hali.
Mimi wala sitegemei jipya, yupo yupo tuu.

tena malalamiko yenyewe hata yatoa kavaa suti yake ya jeans
Ndio maana wazee kama msuya wanasema wazi wazi watampigia kampeni LOWASA kama
akichukua form maana haoni tofauti ya huyu mpangaji wetu wa magogoni.

kuna mchezo mmoja siku hizi ukiwambia ukweli wao wanaongelea barabara vimejengwa nyingi
hii inakuwa hatua moja mbele hatua kumi nyuma sijui kama uwanja utatosha lazima tutoke nje ya geti la karni 21

yaani tuna migao mingi UMEME, MAJI, SASA MAFUTA KILA GARI LITA 5, MGAO WA KEKI YA TAIFA ( HAPA NI WANA MAGAMBA TU),
MGAO WA URAISI ( ZANZIBAR NA BARA/ DINI ), MGAO WA BARABARA NA SASA JK VYEO ANATOA KWA MGAO DINI UMEZINGATIWA
 
nimemuona anafuturu na watoto yatima na leo yupo na mashekhe wengine wakila futari.......mambo mepesi mepesi

Wanasafiri vipi na mafuta hakuna, si magari ya ikulu nasikia yanajaza sheli za uswahili, sasa wamepata wapi mafuta
 
Watanzania tunadhani kuwa huduma muhimu ni favor, Na tukizipata tunaona ni tunasaidiwa. Kama kweli watu wanajali, basi tuchukue hatua. Sio kulalamika.

Kikwete hawezi tena kutatua matatizo ya nchi hii. Hana ujasiri wakuwakoromea hawa watu hana. Pamoja na wabunge wake wa ccm(wengi wao) ambao wamekuwa wakiitetea serekali kana kwambwa wanaishi nje ya Tanzania.

Tusitegemee solution yoyote kutoka kwenye serekali legelege.
Baada ya muda watajitokeza na kuamua kusalimu amri kwa hawa jamaa, kama walivyo
 
Kuna kitu Mungu anataka kukifanya Nchi hii. Hata kama watanzania hawawezi kufanya chochote kwa serikali iliyoshindwa,
 
Huyu jamaa yupo yupo tu hawez kutatua tatizo lolote, yan hamna kitu anafanya... Ngoja tusubiri tuone ila Tanzania itakombolewa na Watanzania wenye uchungu na nchi yao na sio Jk
 
Back
Top Bottom