Rais Kikwete na Waziri Karamagi; wamenunua mgodi?

Hutu ndugu aliyeanzisha hii hoja nafikiri ni kweli amebore. Kuna critical issues zinazoendelea kuhusu haya mambo na migodi na madini

nshomile lete basi hizo crirical issues za madini unazozijua, usilalamike tu mzee mwenzangu, hapa ni talking with freedom ilimradi hujamkosea mtu heshima.



kwa sasa kumhusisha rais Kikwete ni mapema mno
ashomile kumbuka nyota njema.................
tutalala weee tukisubiri tuone matokeo mazuri hadi lini?

tetesi zipo nyingi na labda kelele zetu humu kijiweni kitasaidia kurekebisha mambo pale rais atapojua kuwa alaa kumba kuna watu wako macho na mimi. lets hit the iron when its stil hot, it may help.
 
Mwanakijiji!
Hakuna habari yeyote wala tetesi kwamba hawa jamaa wote wana hisa kwenye kampuzi za madini. Karamangi sijui sana, lakini Rais ninavyoona juhudi zake nafikiri yuko msafi katika hili, na naona amedhamiria kulishughulikia. Si rahisi akaoenekana kuwa makini na muwazi katika kuliwekea mkazo kama anajua ana kasheshe humo. Ningeoma tu tuvute subira tuone outcomes za kamati iliyoundwa. Sasa tutoe maoni yetu kulingana na update zatakazokuwa zinapatika kutoka kwenye kamati teule.
 
Je, Waheshimiwa wanaweza kutueleza kulikua na MVUTO gani pale London kipindi hicho?
halisi hawakawii kutueleza kuwa ilikua mere coincidence simply because ilikuwa ni shopping season. wanasiasa hawakosi excuse bwana.


labda tujiulize zaidi kama kina kapuya wanaweza kumiliki migodi why not hao mabosi wake? and why such a close tie with sinclair? definately hizi suspicions may lead us to believe that something is fishy with JK concerning the whole madini issue.
mwenye ufahamu anisaidia kutoa suspicions hizi.
 
Nshomile! Ulisomea wapi? au siyo tafsiri ya jina lako? Unaijua Tanzania vizuri? Unakumbuka BWM alivyokuwa mkali baadhi ya mambo na kuonyeshwa kuwa anakerwa alivyotoka madarakani uligundua nini?

Nshomile mimi nisiendelee sana nafikiri bado una swali la mwanakijiji tupe tu jibu mkuu!

Test tu iliyokuwa ndogo kuweza kubainisha haya mambo ni Buzwaji, BoT, na juzi tu tulisikia rais kakasirika! kuna action gani?

Nafikiri bado hii mada inahitaji mjadala kwa mapana mno, kusubiri 2010 ni mbali sana tutapigwa bao.
 
Mwanakijiji!
Karamangi sijui sana, lakini Rais ninavyoona juhudi zake nafikiri yuko msafi katika hili, na naona amedhamiria kulishughulikia.

Nshomile watu wa kwenu watakuondolea hilo jina usifikirie kama una data na utetezi wako lete tu. Halafu unajua M/kijiji ametoa mfano mdogo katika Tanzania ya sasa katika Halmashauri nyingi watu/wakurugenzi wana vikampuni vya mifukoni hata makampuni kama TTCL/Tanesco haya yanaweza kuwepo au yapo.

Haya yakiwa yanatokea kwenye makampuni madogo hujue kuna sehemu wanaiga. Kuna sehemu huu mchezo unaanzia hauwezi anzia chini ni juu tu.
 
Ndugu Kakindo, na Mwanakijiji na wengine wote. Mnajibu vizuri lakini msitangulize propaganda. Kama mnawajua basi kwama Kikwete na Karamangi wana lao humo kwenye buzwagi na kadharika, basi twamabie. Mimi nilishasema hakuna, hasa Rais wetu maana hakuna anayeniconvince by providing atleast one evidence. Karamangi naweza kusema labda yawezekana. Lakini Kikwete sidhani. Wanakijiji fanyeni uchunguzi then mtueleze hapa! Mkapa na crew lake hao walieweka. Kila mtu alikuwa na hisia kwamba Mkapa ana lake kuhusu biashara pale Ikulu, kama mnakumbuka habari nyingi zilielekezwa kwa mkewe as controller wa wizi kupitia jina na mme wake. We knew a lot about Mkapa, but for Kikwete you guys are rushing......anyone with convinceable data?????
 
nshomile tetesi si ndio hizi.

embu angalia
mh.rais anakuwa london same hotel na ile aliyokuwa karamagi tena same time wakati mh.karamagi akisaini mkataba. Mh waziri mkuu nae hivyo hivyo

The mining Guru sinclair ni best friend wa mh rais
kumbuka huyu mtu tulimzungumzia sana humu na tetesi zilisema kuwa sinclair anaown the geenstone belt ie mwanza, shinyanga, geita etc na ikumbukwe kuwa huyu ni Tanzanian Royalty chairman and chief executive officer .
Kumbuka kuwa kuwa hawa ni mabesti na yeye ndiye alikuwa kati ya watu muhimu kualikwa ikulu mara tu baada ya raisi kuapishwa.
sasa tetesi tunazo tunashihitaji ni mwenye facts ili ijulikane tetesi zina ukweli au la
 
Ndugu Kinyau. Hicho mimi ndo nacho hitaji. Hapo tunaelewana. Hizi ni tetesi ambazo zinahitaji utafiti. Na kweli matokea yanaweza kuwa ni kweli au si kweli, ila kuwa waandikaji wengine wakisisitiza jambo utafikiri labda tayari wana infor za uhakika, na sisi kama wachangiaji mada kama hizi tunakuwa na mumkari wa kujua ukweli ulipo ili kwa kupitia mtandao huu basi tuuanike ukweli huu hadi kieleweke. Haya uliyoyaeleza nilishayasikia na bado nayafanyia uchunguzi kujua uhusiano wake na agenda hii. Bado kuna mchanganyiko wa ukweli kama Karamangi alikuwa Hotel moja Rais....na PM alikwenda baadaye naye kuwa hotelini humo? Habari nilizota hivi karibuni kutoka kwa mseamji msiri wa wa wizara ya mambo ya nje zinaonyesha taarifa zinazopingana kuhusu hotel walipofikia hawa jamaa!
 
Nshomile pengine hujaielewa trend ya uwekezaji wa vigogo tz. Well zamani (Enzi za Nyerere) hawa jamaa walikuwa malizao wanaziweka kwa wafanyabiashara wakubwa hivyo kucamouflage kabisa ushiriki wao. Mfano ni RIP Amon Nsekela na Ghana Builders, Mheshimiwa mmoja aliyekuwa GM wa TBL Arusha bahati mbaya nimemsahau jina, huyu alishirikiana na Fresh ya shamba, n.k hawa jamaa wengi walizimwa mali zao baada ya kustaafu na hivyo kukumbana na premature deaths.

Anyway Baada ya azimio la zanzibar hawa waheshimiwa wakaanza kuingia front wenyewe na ndio maana ukienda brela data za kina chenge, Rutabanzibwa, Gray mgonja na BWM zinapatikana kirahisi tu.

Kwa hoja ya mwanakijiji ni kwamba lazima hawa jamaa watakuwa na mbinu mpya sasa ya uwekezaji ambayo tracing inaweza kuwa ngumu kidogo maana BRELA ni kwa moto sasa hivi. Kuna sheria ambayo inaruhusu BRELA kudisclose information za wamiliki wa kampuni yoyote iliyosajiliwa pale tena nadhani ni kwa buku mbili tu.

Hivyo basi wana JF wanataka kudokezwa sasa kama kuna mtu ana info za mkuu na karamagi kumiliki kampuni, kama hujui is wiser kukaa kimya. Let those with information wachangie.
 
Hivi si kulikuwa na thread au post kama hii kwenye issue ya Sinclair or Barrick? mchangiaji mmoja alisema anatafuta ushahidi au anao ushahidi anasubiria wakati muafaka ili auweke hapa.
 
tatizo wanafikiri tunasema toka hewani.... mimi nawapa nafasi wajisafishe; Nshomile.. wenzio tunajua vinavyojulikana.... Hilo la mgodi ni stretch ya argument tu.. lakini la hisa za madini... kuna triangle ya ajabu sana.
 
Leo 29/11/2007. Hasara yuko wapi muda tuliowapa umekwisha na hamna lolote.
 
Forum imeshaanza kutoa habari za Udaku? Habari nyingi hazina ushahidi. Kuna hatari kwa forum hii kupoteza credibility
 
Forum imeshaanza kutoa habari za Udaku? Habari nyingi hazina ushahidi. Kuna hatari kwa forum hii kupoteza credibility

Dotori,

Mambo mengi makubwa huanza kwa udaku.

Nakupa mifano michache ya Marekani:

- Suala la uzinzi wa Clinton lilianza kama udaku.

- Suala la kuivamia Iraq lilianza kama udaku.

- Suala la sasa la kubomu Iran ni udaku lakini give it time.

Nakupa mifano mambo ya Tanzania:

- Suala la Karamagi kusaini mkataba hotelini lilianza kama udaku

- Suala la mama Mkapa kusajili kampuni kwa anwani ya ikulu

- Suala la uhusiano wa karibu wa Rostam Aziz na Kikwete

- Suala la Richmonduli na familia ya Lowasa

- Kumbuka jina Richmonduli limeanza hapa JF kama utani

- Suala la .......

Nitaandika mengi sana hapa!

Huu udaku ndio huwa ukifanyiwa kazi unaleta mambo mengi sana.
 
MwK, hapo ndipo unaponifanya niwe nazimia.. maana mantiki yako haihitaji mtu awe anafanya kazi NASA...
 
mwanakjj weka hio Triagle ya MADINI wengine tuijuie... ila ninachokiangalia wakuu wengi wana kampuni nyingi...mie nina kanuni moja ya MSINGI kila mtu namfikiria ni mtu MZURI hadi hapo ushahidi utakapokamilika...sina uhakika na madini, lkn the way nchi inavyokwenda inatisha..HALI za WANA_NCHI ZINAZIDI KUWA MBAYA SIKU HADI SIKU>>UPORAJI>>>Ujambazi..WIZI...maana MJJ leo ukija TZ ukiwa na mali watu wanaweza kukusafisha siku moja tu...hapo ndipo utakapoona nchi hii mbaya..
 
mwanakjj weka hio Triagle ya MADINI wengine tuijuie... ila ninachokiangalia wakuu wengi wana kampuni nyingi...mie nina kanuni moja ya MSINGI kila mtu namfikiria ni mtu MZURI hadi hapo ushahidi utakapokamilika..

Chuma, Kanuni yako katika ulimwengu wa kufikirika ni nzuri; lakini kwa watu ambao tumejifunza tabia ya viongozi wetu kusubiri hadi watu prove otherwise ni hatari. Kutoka kwenye kasheshe ya Mkapa na Yona, mwenzio nimejianzishia kanuni yangu "shuku kila mtu hadi wajithibitishe vinginevyo". Hivyo nikiona tumeingia mkataba fulani nashuku kuna tatizo mahali fulani ili nijiridhishe...nikiridhisha basi ninaamini. Of course kanuni yangu hii inahusu zaidi kwenye public service na politics...
 
mwanakjj weka hio Triagle ya MADINI wengine tuijuie... ila ninachokiangalia wakuu wengi wana kampuni nyingi...mie nina kanuni moja ya MSINGI kila mtu namfikiria ni mtu MZURI hadi hapo ushahidi utakapokamilika...sina uhakika na madini, lkn the way nchi inavyokwenda inatisha..HALI za WANA_NCHI ZINAZIDI KUWA MBAYA SIKU HADI SIKU>>UPORAJI>>>Ujambazi..WIZI...maana MJJ leo ukija TZ ukiwa na mali watu wanaweza kukusafisha siku moja tu...hapo ndipo utakapoona nchi hii mbaya..

Fuatilia mada hii unaweza kupata jibu.
 
Ningeoma tu tuvute subira tuone outcomes za kamati iliyoundwa.

Matokeo ya tume ya MOI ni kuundwa tume nyingine, matokeo ya Takukuru ktk Richmond ni kuundwa tume
Na matokeo ya kamati hii ni kuundwa tume ya madini
 
Hutu ndugu aliyeanzisha hii hoja nafikiri ni kweli amebore. Kuna critical issues zinazoendelea kuhusu haya mambo na migodi na madini yake ambayo kwa sasa kumhusisha rais Kikwete ni mapema mno. Mzee wa waatu hii ni tume ya pili ameunda; ngoja tusubiri tuone matunda yake. Si vizuri kuanza kumpaka matope wakati tunaona juhudi zake kwenye hili. Ndugu yangu kwa upande wangu bado naona kuwa Kikwete amelivalia njuga jambo hili, na akili yangu bado iko mbali kabisa kumhusisha na mambo ya ku-own migodi.

Ni sawa hiyo ni tume ya pili ambayo JK ameiunda, baada ya ile ya Masha 2006.
Nini matokeo ya tume ya Masha? Buzwagi.

Nini matokeo ya tume tatu zilizotangulia (Mboma 2002, Brigedia 2003 na Dr. Kapokola 2005); Bulyahunlu, Buhemba, Geita, Kahama, n.k.

Nini faida kwa Tanzania kutokana na matokeo ya hizo tume zote; More Buzwagis (or better yet, ask Nshomile na atasema subirini tu)!

Fool me once, shame on you. Fool me twice, shame on me. Tanzania has been fooled 100+ times, shame on us all and our offsprings.
 
Back
Top Bottom