Rais Kikwete ateua mabalozi wapya. Marmo, Batilda na wengine ndani!

Huyu ndo mnasema ana PHD FEKI?



b16.jpg



JK akiwa na familia ya Dkt. Deodorus B. KAMALA ambaye ameteuliwa kuwa Balozi nchini BELGIUM. Kabla ya hapo Mhe. Kamala alikuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
 
b18.jpg

JK na familia ya Bibi Shamim NYANDUGA ambaye ameteuliwa kuwa Balozi nchini MSUMBIJI. Kabla ya hapo Bibi Nyanduga alikuwa Naibu Mkuu wa Itifaki, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
 
b3.jpg

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano Wizatra ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bw. Assah Mwambene, akipata kumbukumbu kwa iPad 2 yake
 
Hata kama hatutajari sana elimu ya wateuliwa lakini kwa ukaribu tuliona sasa wa kibiashara na china tulipashwa tuwe na balazo kijana pia mwenye elimu ya kibiashara ingeritusaidia sana.
 
Huo ni ujinga wa baadhi ya waliomo humu. Nadhani hawa walikuwa wanapitwa na wasichana darasani ndiyo maana wana chuki namna hii.

MALE CHAUVINIST P*GS
Na huu ndio ujinga wa wanawake kama wewe ambaye kuambiwa ukweli unadhani ni kudhalilishwa. Mie nazungumza mambo ninajua sio wote wanavua chupi lakini wengi mnavua.
Kwa taarifa yako mnajidhalilisha wenyewe.
Ni kweli sikuwa na shida na visichana darasani maana nilikwenda shule kusoma sio kuangalia visichana. Lakini nyie ambao mlikwenda shuleni kusoma masomo yote pamoja na sexing ndio hawa mnaopewa dezo. Sasa unalalamika nini?
 
Na huu ndio ujinga wa wanawake kama wewe ambaye kuambiwa ukweli unadhani ni kudhalilishwa. Mie nazungumza mambo ninajua sio wote wanavua chupi lakini wengi mnavua.
Kwa taarifa yako mnajidhalilisha wenyewe.
Ni kweli sikuwa na shida na visichana darasani maana nilikwenda shule kusoma sio kuangalia visichana. Lakini nyie ambao mlikwenda shuleni kusoma masomo yote pamoja na sexing ndio hawa mnaopewa dezo. Sasa unalalamika nini?

Kumbe nimekupata kweli kweli ndiyo wewe hasaa!

Na hivyo ulivyo react unaonyesha umeathirika kijana. Endelea tu Chauvinists hawataisha katika karne hii. Mungu aliumba na kuwapa akili wote me na ke sawasawa wewe baki hapo hapo tu ukilia kwa maumivu.

Laaaa haulaaaaa!
 
Hongereni sana.

Hongera Ali Saleh kuwa balozi Oman. Tulikufahamu sana tokea ukiwa India na badae Dubai kwa kazi zako njema na kuitanga za Tz.
 
Naupongeza uteuzi wa Mabalozi wapya uliofanywa na Rais Kikwete na kira gazes TBC1 hivi punde.

--------

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, amewateua wafuatao kuwa Mabalozi:-

i) Mhe. Phillip MARMO, ameteuliwa kuwa Balozi nchini CHINA. Kabla ya hapo Mhe. Marmo alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge.

ii) Dkt. Deodorus B. KAMALA, ameteuliwa kuwa Balozi nchini BELGIUM. Kabla ya hapo Mhe. Kamala alikuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

iii) Dkt. Batilda S. BURIAN, ameteuliwa kuwa Balozi nchini KENYA. Kabla ya hapo Mhe. Dkt. Burian alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira).

iv) Dkt. Ladislaus C. KOMBA, ameteuliwa kuwa Balozi nchini UGANDA. Kabla ya hapo Dkt. Komba alikuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii.

v) Bibi Shamim NYANDUGA, ameteuliwa kuwa Balozi nchini MSUMBIJI. Kabla ya hapo Bibi Nyanduga alikuwa Naibu Mkuu wa Itifaki, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

vi) Bibi Grace J.E. MUJUMA, ameteuliwa kuwa Balozi nchini ZAMBIA. Kabla ya hapo Bibi Mujuma alikuwa Kaimu Mkurugenzi, Ushirikiano wa Kikanda (Regional Co-operation), Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

vii) Bwana Mohamed H. HAMZA, ameteuliwa kuwa Balozi nchini MISRI. Kabla ya hapo Bwana Hamza alikuwa Mkurugenzi wa Mambo ya Nje, ZANZIBAR, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

viii) Ndugu Ali A. SALEH, ameteuliwa kuwa Balozi nchini OMAN. Kabla ya hapo Bwana Saleh alikuwa Balozi Mdogo (Consul General) nchini Dubai.

2. Uteuzi huu unaanzia tarehe 12 Oktoba, 2011. Wataapishwa tarehe 19 Desemba, 2011 saa 03.00 Asubuhi.


========================
jk-mabalozi-1.jpg

jk-mabalozi.jpg
Bado naitafta
 
Back
Top Bottom