Rais Kikwete akifungua Hoteli Mpya ya Kitalii ya Bilila Lodge Kempinski

Nimesikia imejengwa eneo la utata kidogo lakini huo tunaita tetesi tuu.. Mi nataka nimjue mmliki haswa wa hii Hotel maana nimesikia leo kuwa jamaa yetu yule hamiliki mali yoyote hapa nchini zaidi ya kuwa kiongozi mkubwa....

Usiweke Hoja kama Huna Hoja!!
Toa hoja kama una hoja kama imechakachuliwa kaa nayo tuuu...
Hili ni swali wala si udhandiki kama MS atakavyofikiria!!

Ni mali ya mwarabu wa kilimanjaro kempinski
 
Panavutia sana ni sehemu nzuri kwenda kupumzisha akili ila kama hawajaajiri Wabongo basi huo ni utata mkubwa sana.
 
Safi bro, ila nimesikitishwa kwa kutoariji mtanzania hapo, naona kama huyu ni mfilipono fulani hivi?

inategemeana watanzania wangapi wana uelewa au wana ujuzi wa massage, massage ni ngumu sana, hivyo kama hujui mfumo wa damu wa mwili unaweza kumkanda mtu ukaziba mishipa yote ya damu au kumsababishia maumivu na kumuua, hiyo sio kazi nzuri hata kidogo, waachieni wataalamu wenyewe, sidhani kama mtanzania anaweza kufanya massage na asipewe kazi, pia angalia aina za massage , kuna indian, chinese, thai, nakuendelea , sidhani kama kwenye menu yao kuna tanzanian massage, ingekuwepo lazima watu wangejaribu kutest kwani watalii wengi hupenda local flavor, ila kama hatuna, na hatujasoma aina za massage zingine, sidhani tutamlaumu nani, najua kwetu watu wa tanga na mwambao wa tanzania wanaweza kuwa na ujuzi wa kazi za massage, na pia ingridients wanazotumia, sijui kama wanaendeleza ujuzi wao kwa kufundisha wengine au vipi?
 
Watanzania wangapi wanaweza kuafford kwenda hapo na kupumzika?

idadi kamili sijui ila wapo, hili ni eneo la kitalii je ni watanzania wangapi ikiwemo wewe una mazoea ya utalii? je ni aina gani ya utalii unafanya? maana zipo nyingi, kuanzia backpacker mpaka business traveler ambayo ndi mwenye faida kuliko mtalii yeyote, kwani anaweza kutoka kwenye kampuni flani kwa ajili ya business namatumizi yake ni makubwa, ambapo anaweza kutumia ukumbi na vingine hivyo atahitaji eneo linaloendana na hadi yake na kampuni anayowakilisha, hivyo maeneo kama hayo , pia kwa kuwa watalii wana mahitaji mbalimbali na kiuchumi pia ni wa aina mbalimbali, kuna hotel za aina mbali mbali pia, yaani kuna zisizo na nyota , nyota moja hadi ya tano kwa tanzania ,ingawa nchi zingine zina mpaka seven stars hotel, eg huko dubai, hivyo mkuu mtanzania yetote ili mradi anatakka aende hapo na ana hela sidhani kama tatizo, kama watanzania hawaruhusiwi maeneo hayo basi ingekuwa balaa, PS hili ni eneo la biashara, kuna wedding boom in tanzania, wedding zinahitaji kumbi, pia maharusi watahitaji eneo kwa ajili ya honeymoo, hayo ndio maeneo mkuu, ukizingatia hela zenyewe huwa ni michango ya watu na maharusi wanataa kutengeneza mkanda mzuri, maeneo kama hayo sasa watz ndio wangetumia mwanya kutengeneza hela zai ya kulamu tutaweza kwenda pale kweli? why dont you try, mfano, kuwa agent kuintroduce kumbi zao kwa wanaotaka kutumia, na kupata cha juu, IMO
 
Safi bro, ila nimesikitishwa kwa kutoariji mtanzania hapo, naona kama huyu ni mfilipono fulani hivi?

mkuu upo? shwari mwana? hii nimeiweka maksudi, labda kwenye massage menu mtalii hakuorder tanzania massage, au local massage, nadhani unajua aina maarufu za massage duniani, na authenticity zake, ukitaka indian, thai au chinese foot massage ili upate authentic flavor lazima iwe na ladha ya kihindi, kithai au kichina kwelikweli
 
inategemeana watanzania wangapi wana uelewa au wana ujuzi wa massage, massage ni ngumu sana, hivyo kama hujui mfumo wa damu wa mwili unaweza kumkanda mtu ukaziba mishipa yote ya damu au kumsababishia maumivu na kumuua
Hata mini nitaogopa... ila wangeweaka utaratibu wa kuwafundisha wazawa.

mkuu upo? shwari mwana? hii nimeiweka maksudi, labda kwenye massage menu mtalii hakuorder tanzania massage, au local massage, nadhani unajua aina maarufu za massage duniani, na authenticity zake, ukitaka indian, thai au chinese foot massage ili upate authentic flavor lazima iwe na ladha ya kihindi, kithai au kichina kwelikweli

Nipo na nimekupata mkuu,
 
Mimi nilikuwa hapo Jmosi na Jpili yaani tar 18-19 Juni. kuna watanzania wengi sana ila upande wa massage wenyewe wanaita SPA ni wafilipino tu kwa sababu ndo wataalam wa hii kitu, watz wanajua lakini kwa sababu hii kitu ni international ndo maana jamaa kaajiri experts from Ufilipino.
Kwa kweli ni pazuri sana, me nilipatazari tu ila natafuta hela ya kujilipia mwenyewe niipileke familia.
 
tunashukuru kwa kushare experience yako, nakutakia kila la kheri upate hela uende tena na familia yako
 
Mimi nilikuwa hapo Jmosi na Jpili yaani tar 18-19 Juni. kuna watanzania wengi sana ila upande wa massage wenyewe wanaita SPA ni wafilipino tu kwa sababu ndo wataalam wa hii kitu, watz wanajua lakini kwa sababu hii kitu ni international ndo maana jamaa kaajiri experts from Ufilipino.
Kwa kweli ni pazuri sana, me nilipatazari tu ila natafuta hela ya kujilipia mwenyewe niipileke familia.

Tupe rate zake mkuu, manake vitu vingine kwa mtazamo wake tu tunaogopa hata kufikiria mara mbili. Hela ya kuunga unga si unaijua ndugu yangu?
 
Tupe rate zake mkuu, manake vitu vingine kwa mtazamo wake tu tunaogopa hata kufikiria mara mbili. Hela ya kuunga unga si unaijua ndugu yangu?
Kuna rate za wabongo na za wageni, ila nikuanzia dola 299 mpaka dola 10,000 kwa ile presidential suite.
but hata hiyo ya dola 299 pia kwa mTZ ni negotiable kutegemeana na season nayo hiyo room ni nzuri mno na inacover value for money, hutajutia hela yako.
 
Nashangaa toka zianze nyuzi za Kempinski mpaka leo hakuna aliyeanza kuroga kuwa hizo ni ya Mwaarabu tena Muislaam. Vipi tofauti yake huyu na Dowans na OBC?Inashangaza! au anatuweka deka? Zinakaangwa mbuyu kuwaacha wenye meno watafune?
 
Back
Top Bottom